Saturday, April 21, 2012

NGORONGORO HEROES yaichapa SUDAN

Katika michezo tuanzie na taarifa ya hapa nyumbani ambapo TIMU ya Taifa ya vijana NGORONGORO HEROES jana imefanikiwa kuanza vizuri hazma yake ya kutaka kucheza fainali za mashindano ya mataifa ya Afrika kwa kuichapa timu ya SUDAN mabao MATATU kwa MOJA katika mchezo wa awali uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa Jijini DSM.

Mabao ya Ngorongoro Heroes yamefunga na THOMAS ULIMWENGU,RAMADHAN SINGANO MESSI na SAIMON MSUVA

===

ARSENAL yatoka suluhu na CHELSEA

LIGI kuu ya ENGLAND iliendelea jana ambapo michezo MITANO ilichezwa katika viwanja tofauti.

Katika uwanja wa EMIRATES, uwanja wa ARSENAL, Timu ya ARSENAL ililazimishwa suluhu na CHELSEA.

Katika mchezo huo timu zote zilikosa magoli katika nyakati tofauti ambapo VAN PERSIE alikosa nafasi TATU za kupachika magoli wakati mshambuliaji wa CHELSEA, DANIEL STURIDGE naye akikosa nafasi kadhaa za kupachika magoli.

Kocha DI MATTEO wa CHELSEA hakumchezesha DIDIER DROGBA na badala yake akamchezesha FERNANDO TORRES.

Kutokana na matokeo hayo, ARSENAL imesalia katika nafasi yake ya TATU ikiwa imebakiza michezo yake MITATU ikiwa na pointi 65.huku CHELSEA ikiwa katika nafasi ya SITA na pointi zao 58.

==

NEWCASTLE na FULHAM zashinda

Nayo NEWCASTLE UNITED imeicharaza STOKE CITY magoli MATATU kwa BILA katika mfululizo wa ligi hiyo.

Magoli ya NEWCASTLE UNITED yamepachikwa na YOHAN CABAYE ambaye aliipachikia timu yake magoli MAWILI na goli jingine likafungwa na PAPIS CISSE.

FULHAM ikiwa nyumbani nayo imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa magoli MAWILI kwa MOJA dhidi ya timu ya WIGAN ATHELETIC.

NEWCASTLE imefikisha pointi 62, wakati FULHAM yenyewe ina pointi 46.

===

Leo MNCHESTER UNITED na EVERTON, MAN CITY na WOLVES

LIGI ya ENGLAND inaendelea leo kwa mchezo kati ya MANCHESTER UNITED itakayocheza na EVERTON.

MANCHESTER UNITED haina majeruhi wapya , na RIO FERDINAND anatarajia kucheza mchezo wa 450 katika historia yake ya kucheza michezo mbalimbali ya soka, huku ASHLEY YOUNG yeye ukiwa ni mchezo wa 200 tangu aanze kucheza soka la kulipwa.

Kwa upande wa EVERTON , wao watamkosa beki wake LEIGHTON BAINES kutokana na kuwa majeruhi aliopata wakati wa mchezo wa wiki iliyopita wa kombe la FA ambao walifungwa na LIVERPOOL .

Pia huenda mchezaji wa kimataifa wa Afrika Kusini STEVEN PIENAAR akacheza mchezo huo dhidi ya MANCHESTER UNITED utakaochezwa katika uwanja wa OLD TRAFFORD.

Michezo mingine LIVERPOOL itacheza na WEST BROM , WOLVES inaikaribisha MANCHESTER CITY.

Msimamo wa ligi ya ENGLAND, MANCHESTER UNITED inaongoza ikiwa na pointi 82 ikifuatiwa na MANCHESTER CITY ambayo nayo ina pointi 77 ikiwa katika nafasi ya pili.

==

Fainali ligi ya taifa ya kikapu ngazi ya vilabu kufanyika leo

LEO ni fainali ya mashindano ya ligi ya taifa , ambapo timu za kikapu za ABC na SAVIO zitaonyeshana kazi kutafuta bingwa wa mashindano hayo upande wa wanaume.

Wakati upande wa wanawake kutafanyika fainali kati ya JESHI STARS na RED LIONS katika michezo itakayochezwa kwenye uwanja wa ndani jijini DSM