Monday, November 29, 2010

Michezo ya leo

Uganda na Ethiopia,KENYA na Malawi michuano ya CECAFA.
Michuano ya CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP inaendelea mchana wa leo katika kundi la C, kwa mabingwa watetezi UGANDA kupepetana na ETHIOPIA huku KENYA ikiteremka dimbani dhidi ya MALAWI meche zote mbili zinachezwa kwenye dimba la TAIFA jijini DSM.
Katika michezo ya jana ya kundi la B, ZANZIBAR HEROES ilianza vyema michuano hiyo baada ya kuichapa SUNDAN kwa mabao MAWILI kwa bila yote yakifungwa na mshambuliaji ALLY AHMED SHIBOLI.
Mchezo mwingine wa kundi B, RWANDA wakaichapa wababe kutoka Afrika ya Magharibi IVORY COAST kwa mabao MAWILI kwa MOJA.
BURUNDI ilitoke kifua mbele baada ya kuifunga SOMALIA kwa mabao MAWILI kwa BILA.
katika mchezo wa kiporo wa kundi la A, ulichezwa jana katika dimba la KARUME,
===
Chelsea na LIVERPOOL zashindwa kutamba ligi kuu ya ENGLAND
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya ENGELAND CHELSEA jana walishindwa kurundi kileleni mwa ligi hiyo baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao moja kwa moja na NEWCASTLE UNITED katika uwanja wa ST JAMES PARK.

NEWCASTLE UNITED ndio walionza kuzifumania nyavu za CHELSEA kupitia kwa mshambuliaji chipukizi wa klabu hiyo ANDY CARROLL baada ya kuuwahi mpira uliorejeshwa na mabaki wa CHELSEA kwa kipa wao PETER CHEKI.
Bao la CHELSEA likapachikwa wavuni na Salomon Kalou kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na MFARANSA FLORENT MALOUDA.
LIVERPOOL nao wakaendelea kuchechemea baada ya kukubali kichapo cha mabao MAWALI kwa MOJA kutoka kwa mahasimu wao TOTTENHAM HOTSPUR mchezo ulichezwa kwenye dimba la WHITE HART LANE.
Goli lililozima ndoto za LIVERPOOL za kuondoka na angalao na Alama moja ugenini lilikwamishwa wavuni ni chipukizi AARON LENNON katika dakika za nyongeza baada ya kuwazidi mbio mabeki wa LIVERPOOL na kuutumbukiza mpira wavuni.
MANCHESTR UNITED wapo kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na Alama 31 baada ya kuichapa BLACKBURN ROVERS mabao 7-1 mwishoni mwa wiki.
CHELSEA wapo katika nafasi ya pili ikiwa na ALAMA 29 sawa na ARSENAL, lakini ARSENAL wanashika nafasi ya tatu kutokana na tofauti ya mabao ya kufunga.
Manchester City wapo katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo wakiwa na ALAMA 26 baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao MOJA kwa MOJA Stoke City wakati SPURS wapo katika nafasi ya tano wakiwa na ALAMA 25.
===
BARCELONA uso kwa uso na REAL MADRID LA LIGA.
Leo ni leo katika ligi kuu ya HISPANIA maarufu kama LA LIGA wakati REAL MADRID watakapomenyana na BARCELONA katika mchezo unaitwa EL-CLASICO mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Nou Camp.
Kocha wa REAL MADRID MRENO JOSE MOURINHO anajivunia kurejea kwa wachezaji wake kutoka kwenye majeruhi GONZALO HIGUAIN na SAMI KHEDIRA baada ya kuumia katika mchezo wa ligi hiyo dhidi ya ATHLETIC BILBAO wiki iliyopita.
REAL MADRID haijapoteza mchezo wowote katika michuano mbalimbali na katika LA LIGA imeshinda michezo KUMI na kutoka sare MARA MBILI katika msimu huu.
Mechi mbili za msimu kati ya REAL MADRID na BARCELONA ndiyo zinategemewa kuamua ni nani bingwa kwatika ligi hiyo ya HISPANIA LA LIGA na timu itakaoshinda mechi ya leo itakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa LA LIGA mwishoni mwa msimu.
Katika mchezo wa leo safu za ushambuliaji za timu zote mbili ndio zitaumua timu ipi itaondoka na ushindi.
REAL MADRID inawategemea washambuliaji wake Cristiano Ronaldo, Higuain, Ozil na Angel Di Maria,wakati mabingwa watetezi BARCELONA wao watawategemea zaidi Lionel Messi, David Villa, Pedro na Andres Iniesta.
== ==
Valencia yashinda LA LIGA
Katika michezo ya ligi kuu ya HISPANIA LA LIGA iliyochezwa jana VALENCIA imeibuka kidedea baada ya kuifunga ALMERIA kwa mabao MAWILI kwa MOJA.
Mabao ya VALENCIA yakipachikwa wavuni na ROBERTO SOLDADO,katika mchezo mwingine ulipigwa jana ESPANYOL imepaa hadi nafasi ya nne baada ya hiyo jana kuifunga ATLETICO MADRID mabao MATATU kwa MAWILI.
VILLARREAL nao wameibuka kidedea baada ya kuwafunga REAL ZARAGOZA kwa mabao MATATU kwa BILA wakati . ATHLETIC BILBAO wao wakiibuka na ushinmdi wa bao MOJA kwa BILA dhidi ya OSASUNA.
Msimamo wa ligi hiyo unaonyesha kwamba REAL MADRID inaongoza wakiwa na ALAMA 32, BARECELONA wapo katika nafasi ya pili wakiwa na ALAMA 31, VILLARREAL wapo katika nafasi ya TATU wakiwa na ALAMA 27, wakati ESPANYOL wapo katika nafasi ya NNE wakiwa na ALAMA 25.
===
LIVERPOOL kumenyana na MAN UNITED FA CUP
MANCHESTER UNITED itaikabili LIVERPOOL katika mchezo wa kuwania ubingwa kombe la FA mzunguko wa tatu, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la OLD TRAFFORD JANURY mwakani.
ARSENAL wao wamepangiwa vibonde LEEDS UNITED huku CHELSEA wakicheza na IPSWICH.
STEVENAGE itaikabili NEWCASTLE, vijana WA SVEN-GORAN ERIKSSON timu ya LEICESTER wao watakua na kazi ngumu ya kuikabili timu iliwahi kufundishwa na Eriksson, Manchester City.
Michezo hiyo ya kuwania KOMBE LA FA mzunguko wa tatu itachezwa mwezi JANUARY mwakani kati ya tarehe nane na tisa huku mchezo ukaovuta hisia za mashabiki wengi wa soka duniani ukiwa kati ya MAN UNITED na LIVERPOOL.
==
Roger Federer anyakua ubingwa wa ATP World Tour
Katika tenesi mchezaji namba mbili kwa ubora wa tenesi dunia ROGER FEDERER amefanikiwa kunyakua ubingwa wa ATP WORLD TOUR baada ya kuchapa RAFAEL NADAL kwa seti mbili kwa moja ya ushindi wa 6-3, 3-6, 6-1 mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa O2 ARENA jijini LONDON.
FEDERER amenyakua ubingwa huo katika mchezo ulidumu kwa muda wa saa moja na dakika thelathini na SABA dhidi ya mpizani wake Rafael Nadal.
Huu utakua ni ushindi wa pili mkubwa kwa FEDERER kwa mwaka huu baada ya kunyakua taji la AUSTRALIAN OPEN mwezi January mwaka huu na sasa amenyakua taji la ATP World Tour katika fainali iliyokua inashirikisha wachezaji NANE nyota duniani kwa upande wa wanaume.

Katika michezo ya nusu fainali NADAL alimufunga ANDY MURRAY huku FEDERER akimchapa NOVAK DJOKOVIC.
===

Thursday, November 25, 2010

michezo ya leo


CECAFA yaendelea kuwafua waamuzi
Waamuzi KUMI na TANO ambao watachezesha mashindano ya CECAFA TUSKER CHALENJI kwa mwaka huu wameanza kupatiwa mafunzo ambayo yatadumu kwa kipindi chote cha mashindano hayo yanayoanza jumamosi hii katika uwanja wa TAIFA jijini DSM.
Aliyekuwa mwamuzi wa soka nchini , OMAR ABDULKADIR amesema huo ni utaratibu waliojiwekea kila asubuhi kukutana ili kuondokana na makosa ya mara kwa mara mchezoni.
Timu ya ZANZIBAR HEROES na MALAWI zimepangwa kuwasili leo , huku timu nyingine zikitarajia kuwasili nchini kesho tayari kwa mashindano hayo yaliyopangwa kufunguliwa kwa mchezo kati ya KILIMANJARO STARS na ZAMBIA.
= =
BFT yawataka mabondia kupima ukimwi
Shirikihso la ngumi za ridhaa nchini BFT,limekiri kuwa sera ya kupima virusi vya ukimwi kwa mabondia wake ni nzuri ijapokuwa kwa sasa sera hiyo haifuatiliwi.
Katibu mkuu wa BFT, MAKORE MASHAGA ameaysema hayo wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa TBC kuhusiana na mabondia wengi kuwa katika hali ya hatari ya maambukizi kama suala hilo halitajidiliwa na kuwa na sera inayokubalika michezoni.
Amesema kuwa endapo watagundua kuna bondia ana tatizo hilo, watampa ushauri wa namna gani kuendeela na mchezo huo au ikibidi kumweleza kuachana kabisa na mchezo huo .
Katika hatua nyingine, MASHAGA amevitaka vyama vya michezo huo vya mikoa kuhakikisha uthibitsho wao wa mashindano ya taifa yatakayofanyika mwakani ambayo yatapata wachezaji wa timu ya taifa.
= =
BMT yaunda kamati kuendesha SHIMISETA
Baraza la michezo nchini BMT limeundwa kamati maalumu ya kuratibu michezo ya wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania.
baada ya kugundua kuwa viongozi waliokuwepo wamemaliza muda na wanaongoza shirikisho hilo kinyemela.
Afisa habari mwandamizi wa baraza la michezo (BMT) JOHN CHALUKULU amesema kwa sasa jukumu la kusimamia michezo litakuwa chini ya kamati teule na kuzitaka halmashauri kuendelea na maandalizi huku katibu mkuu wa kamati ya muda SALEH LUBANA akisema tayari wameandaa rasimu ya katiba na inatarajiwa kupitishwa na mkutano mkuu utakaofanyika kipindi cha michuano hiyo
Michuano hiyo itakayofanyika mjini MOROGORO itaanza kutimua vumbi NOVEMBA 27 na itafikia tamati yake desemba 5 mwaka huu.
= =
ZANZIBAR HEROES yaichapa DAR ALL STARS
Hapo jana katika Dimba la Amani huko kisiwani Zanzibar kulikuwa na Mechi ya kirafiki kati ya Zanzibar Heroes na Dar es salaam All Star mchezo uliopigwa majira ya usiku na hadi ya kipenga cha mwisho kinapulizwa znz Heroes ilitoka kifua mbele kwa kuichapa Dar All Star Goli moja kwa sifuri.
Ndani ya dakika ya kumi ya mchezo mchezaji wa ZNZ HEROES Ally Ahmed alichezewa vibaya ndani ya eneo la hatari na Meshark Abeir na kupelekea mwamuzi wa mchezo huo kutoa penati kwa znz heroes na kupigwa na Hamis Ncha lakini mlinda mlango wa Dar all star Ivo Mapunda akaipangua penati hiyo kisha ktk piga nikupige mchezaji Suleiman Kassim wa znz heroes akapiga kichwa na mojakwa moja kikaingia kimyani na kuiyandikia znz goli la kuongoza hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa znz heroea 1 Dar All Star 0.

Hii ni mechi ya marudiano kati ya znz heroes na Dar All Star mechi ya kwanza walitoka bila ya kufungana huko jijini Dar na mechi hizi imewajenga vizuri znz heroes ktk kujiandaa na michuano ya challenge cup itakayofanyika huko Dar.
= =
Music Dance competition yazinduliwa Dar
Shindano la kusaka wanamuziki wadansi chipukizi linalojulikana kama MUSIC DANCE COMPETITION limetambulisha leo jijini DSM, ambapo washindi watakaopatikana watazawadiwa zawadi mbali mbali.

Akizungumza jijini DSM,mratibu SULEIMAN MATHEW pamoja na mmmoja wasanii muziki wa dansi EMANUEL FIRI maarufu kama BOB KISSA wamesema kuwa shindano hilo litasaidia kukuza vijapi vya muziki wa dansi.

MATHEW amesema kuwa vikundi mbali mbali vitashindwanishwa na baadaye kupata watakaoingia fainali ambayo itakuwa mwezi wa tatu mwakani .

Na hawa ni moja ya wasaniii ambao wameshaunad kundi lao ambalo litaingia katika shindano hilo na hapa wanatoa burudani ya mwimbo kutoka bendi ya MSONDO NGOMA.
==
Mwanamuziki GYPTIAN awasili nchini
Nyota wa muziki wa Raggae na Dancehall toka Jamaica, Windel Beneto Edwards maarufu kama Gyptian, amewasili nchini jana usiku na kuwaomba wanachuo na wapenzi wa muziki kujitokeza kwa wingi kesho katika tamasha la muziki lijulikanalo kama Str8Muzik Festival Inter-College Special 2010.

Akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, msanii huyo amewataka mashabiki kufurika kwa wingi kuona burudani aliyonayo na hapa Gyptian mwenyewe akatoa kionjo cha burudani.

Tamasha hilo litafanyika viwanja vya TTCL Kijitonyama jijini DSM
= =
Wachezaji wa ARSENAL CESC na EBOUE nje baada ya kuumia
Matumaini ya Arsenal kusonga mbele hatua ya timu 16 ya kuwania Ubingwa wa soka wa Ulaya, yalizidi kuingia mashakani baaday wachezaji wake wakutumainiwa, nahodha Cesc Fabregas na Emmanuel Eboue kuumia wakati wa mchezo .
Nahodha Fabregas aliumia misuli ya paja, wakati Eboue ameumia goti.
Kwa mujibu wa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger Huenda ikamchukua wiki mbili au tatu Fabregas kupona. Aliongeza Nilibahatisha kumchezesha na sasa mambo yameharibika
Wenger alimchagua Fabregas kucheza licha ya kiungo huyo kutokuwa katika hali yake ya kawaida. Amesema ni tatizo la msuli wa paja katika mguu mwengine, ni vigumu sana kutabiri kwa muda gani Cesc hatacheza.
Arsenal ilikuwa inahitaji pointi kuweza kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele hatua ya mtoano, lakini wakazembea na kuruhusu mabao mawili yaliyofungwa na Matheus dakika ya 83 na jingine kutoka kwa Mbrazil huyo katika dakika za nyongeza kwenye uwanja wa Estadio Municipal.

===.
SERENA kutoshiri mashindano ya wazi ya AUSTRALIAN.

Mchezaji wa tenesi kwa upande wa wanawake SERENA WILLAMS hatashiriki mashindano ya wazi ya AUSTRALIAN kutokana na kusumbuliwa na goti .

Mchezaji huyo ambaye anashikiria nafasi nzuri kwa bora DUNIANI katika mchezo wa tenesi amesema hatashiriki mashindano hayo bado anaendelea kutibu goti lake.

Mpaka sasa WILLIAMS anaendelea kuuguza goti lake huku akiendelea na mazoezi mapesi .

Mahindano ya tenesi ya AUSTRALIAN yanategemewa kuanza janualy 17 hadi 30 mwakani.

===.

Nadal ambwaga Djokovic
Mchezaji RAFAEL NADAL amejiweka katika nafazi nzuri ya kufuzu kucheza hatua ya mtoano ya mashindano ya tennis ya ATP WORLD TOUR baada ya kuibuka na ushindi wa seti mbili dhidi ya NOVAK DJOKOVIC.

Baada ya seti ya kwanza kuanza DJOKOVIC alipata matatizo ya jicho na hivyo ilimlazimu atoke nje ya uwanja na baada ya kurudi uwanjani hakuwa mchezaji yule yule wa mara ya kwanza tena.

NADAL alimshinda DJOKOVIC kwa seti mbili zenye matokeo ya 7-5 6-2 katika muda wa saa moja na dakika 51 na hivyo kuongoza kundi A kwa kuwa ameshinda michezo miwili, wakati DJOKOVIC yeye yupo sawa na TOMAS BEDYCH kwa ushindi wa mchezo mmoja baada ya BEDRYCH kushinda katika mchezo wake uliochezwa jana mchana dhidi ya ANDY RODDICK.
= = = = =

Tuesday, November 9, 2010

Images from the 2010 Channel O Video Awards


Images from the 2010 Channel O Video Awards

Images from the 2010 Channel O Video Awards


Images from the 2010 Channel O Video Awards

TFF yang'ang'ana na Kaseja

Shirikisho la soka nchini TFF kupitia kwa kaimu katibu mkuu wake SUNDAY KAYUNI limetoa ufafanuzi kuhusu utata wa suala la kufungiwa kipa wa Simba Juma Kaseja kwa kusema adhabu ya mchezaji huyo ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS iko pale pale ingawa maelezo ya awali yalikosewa.

Kayuni amedai kuwa ni kweli Kaseja alipeana mikono na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mechi kati ya simba na Yanga iliyofanyika mwezi uliopita jijini Mwanza lakini alikwepa kupeana mikono na wachezaji wa Yanga.

Katika maelezo ya awali TFF ilidai kuwa Kaseja alikwepa kupeana mikono na Mkuu wa Mkoa wa Mawanza Abbass Kandoro jambo ambalo lilikanushwa kwa picha na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.



VYUO VIKUU NA MZIKI


Katika burundani wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo katika mikoa ya DSM, MOROGORO na DODOMA wanatarajiwa kupata burundani ya mziki kutoka kwa wanamziki mahiri wa kimataifa na Afrika ya mashariki kwenye tamasha la STR8MUZIK FESTIVAL litakalofanyika katika tarehe za 13, 20 na 27 mwezi huu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo kwa mwaka huu MENEJA MSAIDIZI wa singara ya SM ISAMBA KASAKA amesema wanafunzi wa vyuo vikuu wategemee kupata burundani murua itakayokonga nyoyo zao mwaka huu.

KASAKA amewataja wanamziki wakakao jimwaka jukwaani kutumbuiza katika tamasha hilo kuwa ni wanamziki wa kimataifa T PAIN,ELEPHANT MAN,GYPTIAN na MIMS wakati kutoka Afrika ya mashariki ni MICHAEL ROSS kutoka UGANDA,FID Q,MWANA FA,JOH MAKINI,CHEGE na SAM WA Ukweli.


Kili stars hadharani


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars JAN PAULSEN ametangaza kikosi cha wachezaji 22 wa timu hiyo tayari kujiandaa na mashindano ya CECAFA TUSTER CHALLENGE CUP na kusema TANZANIA kuwakilishwa na timu mbili za KILIMANAJARO STARS na ZANZIBAR HEROES katika mashindano hayo kuna hasara.

Akizungumza wakati wa kutangaza kikosi hicho jijini dsm hii leo kocha wa KILIMANAJARO STARS ambaye pia ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS JAN PAULSEN ametaja baadhi ya hasara ni kuwakosa wachezaji mahiri aliokwisha waandaa wakati wakitumikia TAIFA STARS hali inayopunguza nafasi ya Tanzania kunyakua kombe la CHALENGE.

Hata hiyo PAULSEN amekiri kuwa mfumo huo wa kuwa na timu mbili katika mashindano ya CECAFA TUSTER CHALLENGE CUP kunatoa fursa ya kuibua wachezaji wapya ambao ni faida kwa TAIFA STARS.

Katika kikosi cha KILIMANJARO STARS kilichotangazwa na kocha huyo kinachotarajiwa kujipima nguvu tarehe 17 mwezi huu na kati ya timu ya taifa ya ETHIOPIA au KENYA kina sura mpya ambazo ni pamoja na GAUDENCE MWAIKIMBA, JUMA NOYSO, KIGI MAKASI na THOMAS ULIMWENGU amayecheza soka la kulipwa huko SWEDEN.

KILIMANJARO STARS imepangwa katika katika kuindi A kwenye mashindano ya CECAFA TUSTER CHALLENGE CUP na itaanza kutupa karata yake ya kwanza dhidi ya ZAMBIA katika mchezo wa ufunguzi NOVEMBA 27 kabla ya kuzikabili SOMALI NOVEMBA 30 na BURUNDI DECEMBA 4.


Simba kidedea


Basi la mashabiki wa simba wakirejea kutoka SONGEA ambapo timu hiyo ilicheza na majimaji mwishoni mwa wiki na kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila

Monday, November 8, 2010

twiga kurejea mikono mitupu


Timu ya taifa ta wanawake ya tanzani TWIGA STARS kurejea kesho nchini kutoka AFRIKA KUSINI baada ya kutolewa katika fainali za kombe la matifa ya AFRIKA baada ya jana kufungwa na NIGERIA mabao Matatu kwa BILA

Thursday, November 4, 2010

Twiga yafungwa na Mali

Twiga stars yafungwa na Mali mabao matatu kwa mawili na kuyaanga mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake yanayofanyika Afrika kusini.

Twiga Stars imesalia na mchezo mmoja kwa kukamilisha ratiba dhidi ya Nigeria mchezo ambao utachezwa Novemba saba.

Katika mchezo wa kwanza katika kundia la A Twiga ililala mbele ya wenyeji Banyana banayana baada ya kufungwa mabao mawli kwa moja.

===

Timu ya taifa ya wanawake ya Afrika Kusini BANYANA BANYANA imefungwa magoli mawili kwa moja na wanawake wa Nigeria, Super Falcons katika mchezo wa kundi A uliopigwa katika dimba la Sinaba mjini Daveyton.

Magoli ya Nigeria yamewekwa kimiani na Perpetua Nkwocha dakika ya 14 na dakika nane baadae Nkwocha aliongeza goli la pili kwa kichwa.

Banyana Banyana walifuta machozi kwa goli la Janine van Wyk aliyepiga mpira wa adhabu ndogo uliojaa moja kwa moja wavuni na kumshinda mlinga mlango wa Nigeria Uzoaru Dede.

Baada ya mchezo, kocha wa Banyana Banyana Augustine Makalakalane amesema vijana wake wameonesha kiwango kizuri na ana faraja kuwa watafika mbali licha ya kichapo hicho na wanataraji kufanya vema mchezo ujao dhidi ya Mali

Katika michezo yao ya kwanza Banyana Banyana iliifunga Tanzania magoli mawili kwa moja huku Nigeria ikitoa kichapo kwa Mali cha magoli matano kwa bila

Michezo ya leo

Simba kujenga uwanja wake wa kisasa

KLABU ya SIMBA imeanza mchakato wa kuwa na kiwanja chake ambapo katika taratibu za awali kamati ya utendaji ya klabu hiyo imeamu kufanya mazungumzo na kampuni ya ujenzi wa uwanja ya GIDAS kutoka nchini UTURUKI.

Akizungumza na waandishi wa habari , Mwenyekiti wa klabu hiyo , ISMAIL ADEN RAGE amesema ujenzi wa kiwanja hicho unatarajiwa kukamilika kipindi cha miaka miwili na kitakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki ELFU THELATHINI.

Uwanja huo wa SIMBA ambao RAGE ameutaja kama ni uwanja wa kisasa utajengwa katika maeneo ya BUNJU na utakuwa na maduka makubwa.

Katika hatua nyingine, klabu ya SIMBA imempa madaraka zaidi kocha wake PATRICK PHIRI ambapo yeye atakuwa mkuu wa benchi la ufundi la klabu ya SIMBA.

==

VODACOM yatoa MILIONI 17 kwa mchezo wa Baiskeli

KAMPUNI ya simu za mkononi nchini VODACOM imetoa shilingi MILIONI 17.4 kama zawadi kwa washindi tofauti katika mashindano ya wazi ya mchezo huo yaliyopangwa kufanyika kuanzia NOVEMBA 12 hadi 13 jijini MWANZA.

Afisa mdhamini na matukio wa kampuni hiyo, RUKIA MTINGWA amesema kampuni yake imeamua kutoa msaada huo ili kufanikisha mashindano hayo ambayo pia yatakuwa ni chachu ya kupata timu ya taifa.

Katika mashindano hayo , upande wa wanaume watakimbia kwa kilometa 196 ambapo zawadi ya mshindi wa kwanza itakuwa ni shilingi milioni MOJA na NUSU , mshindi wa pili MILIONI MOJA na mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi laki SABA.

Upande wa wanawake watakimbia kwa mita 80 ambapo mshindi wa kwanza atapata milioni MOJA, mshindi wa pili laki nane na watatu atajipatia laki sita.

Aidha, kutakuwa na mbio za kilometa KUMI ambazo zitawashirikisha watu wenye ulemavu ambapo zawadi zao ni shilingi laki NNE.

==

Tamasha la SWAHILI FASHION WEEK laanza jijini

Wakati tamasha la wabunifu wa mavazi maarufu SWAHILI FASHION SHOW likiwa limeanza katika viwanja vya KARIMJEE jijini DSM wabunifu hao wameelezea changamoto mbalimbali zitakazotokana na onesho hilo

Mbunifu wa Tanzania Ailinda Sawe, John Kavele na Samira Jeizan kutoka Kenya wamesema onesho hilo linatoa fursa kwa wabunifu wachanga kujitangaza kimataifa hatua itakayowainua kiuchumi.

Wabunifu hao kutoka nchi za Afrika mahsraiki wataonesha mavazi mbalimbali ya asili yanayovalia na jamii za Afrika mashariki ambayo pia yanatokana na mali ghafi za Afrika, litafikia kilele chake siku ya Jumapili.

==

Heskey nje kutoka na kuumia goti

MSHAMBULIAJI wa Aston Villa Emile Heskey atakuwa nje ya dimba kwa wiki kadhaa kutoka na kuumia goti .

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32- mchezaji wa zamani wa ENGLAND ambaye amefunga magoli mnne katika msimu huu anatafanyiwa upasuaji wa goti lake.

Heskey amekuwa akionyesha kiwango kizuri katika timu yake baada ya mchezaji Gerard Houllier, kuhama timu hiyo ya ASTON VILLA.

Baada ya mchezaji huyo kuumia sasa amebakia mchezaji mmoja mkongwe katika klabu ya ASTON VILLA John Carew ambaye atacheza siku ya jumamosi.

Kuumia kwa Heskey kumekuja baada wakati mchezaji wa kimatifa wa ENGLAND Gabriel Agbonlahor anaendelea kuuguza maumivu yake.

Heskey alimumia wakati wa mazoezi tore.

===

Wachezaji wa Ghana hawajalipwa bonasi

Mafanikio ya kufika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia yamezua mzozo unaohusu malipo ya ziada waliyoahidiwa wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana.

Hakuna mchezaji hata mmoja aliyelipwa dola 63,000 alizoahidiwa kila mchezaji wa Black Stars kwa sababu taratibu za malipo katika benki ya Ghana.

Benki Kuu ya Ghana inasisitiza kuwalipa wachezaji hao kwa kuwawekea pesa katika akaunti zao.

Lakini wachezaji wamekuja juu kwa vile wanataka walipwe fedha taslimu mkononi kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Taarifa ya Benki Kuu ya Ghana imesema benki hiyo hufanya kazi zake za kuwahudumia wateja kwa taratibu zilizopo na kutofanya hivyo ni kwenda kinyume na shughuli za uendeshaji benki ambapo wakiwalipa fedha taslimu zinaweza kuzidi kwa zaidi ya dola elfu kumi.

Benki Kuu ya Ghana imeiambia Wizara ya Vijana na Michezo watawalipa wachezaji wa Black Stars kwa fedha za kigeni kupitia akaunti zao au kwa hundi.

Mzozo huo wa malipo ya wachezaji uligubika pambano la kufuzu katika michezo ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Sudan.

Tarehe ya mwisho ya kulipwa wachezaji hao ilikuwa 15 mwezi wa Oktoba na hakuna senti hata moja waliyolipwa wachezaji hao.

===

MOURINHO akerwa na sare.

Kocha wa timu ya REAL MADRID Jose Mourinho amefurahiswa na kikosi chake kwa kutofungwa na timu yoyote ile katika michuano ya ligi ya mabingwa lakini hakufurahia sare ya kufungana mbili mbili na timu ya AC MILAN.

MOURINHO amesema kama kikosi chake kingecheza vizuri katika kipindi cha pili wangeibuka na ushindi..

Amesema matokeo ya sare hajamfurahisha kwa sababu timu hiyo ilikuwa na nafasi nyingi za kufunga lakini imeshindw akutumia nafasi hizo..

Katika mchezo huo REAL MADRID walianza vizuri wakafunga goli kupitia kwa GONZALO HIGUAN, kazi nzuri ya DI MARIA.

Kipindi cha pili AC MILAN wakafanya mabadiliko wakamwingiza mkongwe PHILIPPO INZAGI PEOPLE, ambaye akabadilisha hali ya mchezo, akasawazisha goli, kazi nzuri ikifanywa na ZLATAN IBRAHIMOVIC.

PHILIP INZAGI akaendelea kuwaonesha REAL MADRID kwamba yeye si mzee, akapachika goli la pili.

Kimuhemuhe kikamuingia kocha JOSE MOURIHNO,lakini vijana wake wakatulia, na kijana asiyetajwa sana pale BERNABEAU PETRO LEON akampiga doba mlinda mlango wa AC MILAN na kusawazisha goli hilo.

REAL MADRID wamejikatia tiketi ya kucheza hatua ya mtoano.

==