Tuesday, May 10, 2011

MERY NAALI atamba kuendeleza kipaji chake.

MWANARIADHA bora wa kike kwa mwaka 2010, MERY NAALI amesema ataendelea kujitahidi kufanya mazoezi zaidi ili aliwakilishe vizuri taifa katika mashindano ya kimataifa.

Kauli ya MERY imekuja baada ya kuwa miongoni mwa wanariadha watakaoiwakilisha TANZANIA katika mashindano ya afrika mashariki na kati ambapo TANZANIA itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Akiwa na umri wa miaka KUMI na MITANO, MERY NAALI alifanikiwa kushiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya riadha ya Taifa ambayo yalifanyika mkoani SINGIDA na alifanikiwa kushika nafasi ya tatu katika mbio za kilometa 5,000 na kuibuka mshindi kwenye mbio za kilometa 10,000.

Pamoja na mbio hizo na nyingine za kimataifa, kumemfanya mwanariadha huyo kushinda tuzo za chama cha waandishi wa habari za michezo kwa mwaka 2010

==
NIZAR anyimwa ruhusa

MCHEZAJI wa kimataifa wa Taifa STARS anayechezea soka lake katika klabu ya VANCOUVER WHITECAPS, ya CANADA imemnyima ruhusa NIZAR KHALFAN kuja nchini kucheza mchezo dhidi ya BAFANA BAFANA.

Taarifa ya ofisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF, BONIFACE WAMBURA amesema klabu yake imenyima ruhusa hiyo NIZAR kwa kuwa Mei KUMI na TANO mwaka huu , timu yake itacheza mechi muhimu ya ligi.

Hata hivyo wachezaji wengine kama IDRISSA RAJAB, HENRY JOSEPH, ABDI KASSIM, DAN MRWANDA na ATHUMAN MACHUPA bado unafuatiliwa na shirikisho hilo.

Tiketi kwa ajili ya mchezo huo zitaanza kuuzwa keshokutwa

==
MOSIMANE asema mchezo wa TAIFA STARS utakuwa mgumu.

KOCHA wa timu ya taifa ya AFRIKA KUSINI, BAFANA BAFANA, PITSO MOSIMANE amesema anauchukulia kwa uzito mkubwa mchezo wa kirafiki kati ya timu yake na TANZANIA utakaochezwa jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini DSM.

MOSIMANE amezungumza hayo wakati timu yake ikiwa kambini kujiandaa na mchezo huo ambao utakuwa ni wa kirafiki kwa timu zote mbili zinazojiandaa na michezo ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani yatkayofanyika GABON na EQUTORIAL GUINEA .

Katika kikosi cha BAFANA BAFANA, kiungo wa timu ya
KAIZER CHIEFS, SIPHIWE TSHABALALA ndiye atakuwa nahodha.

BAFANA BAFANA, inajiandaa kucheza na MISRI wakati TAIFA STARS inajiandaa na mchezo dhidi ya Jamhuri ya kati.

==
BANYANA BANYANA nayo yaingia kambini.

Nayo timu ya taifa ya wanawake ya AFRIKA KUSINI, BANYANA BANYANA ipo kambini kujiandaa na mchezo wake dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya BOTSWANA, mchezo utakaochezwa mjini GABORONE, jumapili hii.

Mchezo huu ni wa kutafuta tiketi ya kucheza mashindano ya kombe la ALL AFRICA GAMES ambayo tayari Tanzania imepata tiketi ya kucheza fainali hizo baada ya SUDAN kujitoa na hivyo kuipa nafasi TWIGA STARS kushiriki moja kwa moja mashindano hayo.

Katika mchezo wa awali BANYANA BANYANA ilishinda goli MOJA kwa SIFURI.

==
Katika NBA , IKIWA katika uwanja wake wa nyumbani timu ya LOS ANGELS LAKERS imepokea kipigo cha vikapu 86 kwa vikapu 122 vya timu ya MAVERICKS .

Matokeo mengine timu ya OKLAHOMA imefanikiwa kuichapa timu ya MEMPHIS kwa vikapu 133 kwa 123.

Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya MIAM HEAT ambayo ilicheza na timu ya BOSTON na katika mchezo huo timu ya MIAMI ikiwa nyumbani imeweza kuichapa BOSTON vikapu 98 kwa 90.
==

Kareti mafunzoni

Wachezaji mia moja wa mchezo wa karete wapata mafunzo ya kimataifa

Zaidi ya wachezaji mia moja kutoka katika klabu za karete za jijini DSM wanahudhuria mafunzo ya siku mbili yayoendeshwa na mkufunzi wa shirikisho la karete dunia kutoka Japan MANABU MURAKAMI, mafunzo hayo yanafanyika katika uwanja wa ndani wa taifa jijini DSM.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo kocha wa Shotokan Karete Tanzania Phillipo Chikoko amesema mafunzo hayo yameadaliwa kwa ajili ya kunyanyua kiwangao cha mchezo huo nchini.

Chikoko amesema mafunzo hayo pia yatasaidia pia kupata timu ya taifa ambayo itashiriki katika mashindano ya dunia yatakayofanyika mwakani nchini AUSTRALIA.

Bamigham city ndani ya uwanja wa taifa.

Kocha mkuu wa Bamigham city Adrew Watson akikagua uwanja wa taifa kabla ya timu yake kutembelea tanzania kwa ziara ya kimichezo mwezi July.timu hiyo itacheza na SIMBA na YANGA.