Bondia
MOHAMED MATUMLA, SNAKE BOY JUNIOR amewatoa watanzania kimasomaso baada ya
kutandika bondia WANG XIN HUA kutoka CHINA na kuibuka na ubingwa wa WBF UZANI
wa BANTAM katika pambano lilofanyika katika ukumbi wa DIAMOND JUBLIEE jijini
DSM.
Katika
pambano hilo ambalo lilikuwa na ushindani wa hali ya juu, MATUMLA, amemchapa WANG
XIN HUA kwa ALAMA.
Kwa
usindi huo MATUMLA amepata nafasi ya kucheza pambano la utangulizi wakati wa
pambano kati ya FLOYD
MAYWEATHER, dhidi ya MANNY PACQUIAO utakaochezwa MAY MBILI nchini MAREKANI.
=====
Wakati
huo huo bondia MADA MAUGO ametoa kichapo cha mwaka baada ya kumtandika bila
huruma kwa KO Mpizani wake JAPHET KASEMBA katika mzunguko wa NANE.
=====
Mkurugenzi
wa Idara ya Utamaduni kutoka
wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo HERMAN MWASOKO aliomba
shirika la hifadhi ya jamii NSSF kubadili mfumo wa mashindano ya kuwania KOMBE
LA NSSF kutoka kwenye mtindo wa mtoano hadi ligi ili kuongeza ushindani.
MWASOKO aliyasema hayo baada ya kukabidhi zawadi kwa
washindi ,huku nahodha wa TBC WARRIORS, JAMES MAPEPELE na Habari Zanzibar AMRI
MAKAME wamesema walijiandaa vyema ndio maana wakaibuka na ushindi
TIMU ya TBC WARRIORS imenyakua nafasi ya tatu, IPP
MEDIA imeshika nafasi ya pili wakati HABARI ZANZIBAR ndio mabingwa michuano
katika soka kwa mwaka huu.
====
TIMU ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS kesho inashuka
dimbani kuibili timu ya taifa ya Malawi the flames katika mchezo wa kirafiki wa
kimataifa utaochezwa katika uwanja wa CCM KIRUMBA mjini MWANZA.
TAYARI
KIKOSI cha wachezaji wa timu ya Taifa ya MALAWI, THE FLAMES kimewasili jijini
MWANZA kwa mchezo dhidi ya TAIFA STARS.
Mbali
na wachezaji walioitwa na kocha wa MALAWI wanaocheza soka la ndani ya nchi yao
pia amewajumuisha wachezaji wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za AFRIKA KUSINI, JAMHURI ya KIDEMOKRASIA ya CONGO, MSUMBIJI na ZIMBABWE.
====