Wednesday, March 24, 2010

TBC SPORT KAZINI


Waandishi wa habari za michezo wa TBC wakizungumza na mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Thomas Ulimwengu katika uwanja wa Karume jijini DSM,kutoka kulia JANE JOHN,CHARLES MWEBEA na EVANCE MHANDO.

Thomas Ulimwengu tumaini jipya kwa Stars


Mshambuliaji chipukizi wa timu ya taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 Thomas Ulimwengu kulia akipewa mawaidha na makocha wake,kocha msaidizi Mohamed Adolf Rishard kushoto na Kocha mkuu wa timu hiyo Mbrazil Rodrigo Strockeler kwenye uwanja wa karume jijini DSM hivi karibuni.

Stars na Ngorongoro Heroes kibaruani Afrika

Timu za taifa ile ya wakubwa Taifa Stars na timu ya taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 zinakibarua kingumu katika kutafuta tiketi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Taifa Stars yenyewe inashuka dimbani siku ya jumamosi kupepetana na Somalia kwenye uwanja wa Uhuru katika kutafuta tiketi ya kucheza katika fainali za Kombe la mataifa bingwa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani maarufu kama CHAN.

Wakatika kwa upande wa Ngorongoro Heroes wao wanajiandaa kumenyana na MALAWI April 17 ugenini katika kuwania kutafuta tiketi ya kucheza fainali za vijana wenye umri huo ambazo zitafanyika Libya mwakani

Monday, March 15, 2010

NGORONGORO HEROES KAZINI DHIDI YA MALAWI

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 tayari imeanza kambi ya mazoezi ya mwezi mmoja kabla ya kuivaa timu ya taifa ya Malawi.

mchezo wa kwanza utakuwa ugenini nchini MALAWI kati ya tarehe 17 na kumi na nane mwezi wa April,na mchezo wa marudiano utafanyika May jijini Dar es Salaam na kama itashinda itaivaa Ivory Coast na iwapo itavuzu itakuwa imekata tiketi ya kushiriki michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka ishirini zitakazofanyika nchini Libya mwaka 2011

Monday, March 8, 2010

Kazi ni kazi mradi mkono uende kinywani


Mkazi mmoja ambaye jina lake halikujulikana akifuta kioo cha daladala aina ya DCM katika kituo cha mwenge,ujira wake ni shilingi mia moja ambayo si haba akifanya kazi hiyo kwa kutwa nzima.

Kocha wa Taifa Stars Marcio Maximo


Kocha wa timu ya taifa Taifa Stars Marcio Maximo akiongea na waandishi wa habari,Kulia ni rais wa TFF Tenga.

RIADHA

Nilibahatika kuhudhuria mashindano ya mwaka huu ya Kili Marathon,nasikitika kusema kwamba inatisha kuona Wakenya wanaendelea kutamba katika riadha na sisi tukiendelea kusuasua, sijui hali hii itaisha lini,na swali la kujiuliza ni je watanzania tupo tayari kushindana katika riadha? je vyama husika vinafanya nini kuhakikisha mchezo huu unakuja juu kama ilivyokua miaka ya 1970