Tuesday, July 27, 2010


Ujenzi wa barabara ya mandela unaendelea vyema

MANDELA ROAD



Ujenzi wa barabara Mandela unandelea

Netball kiwanjani


Ubingwa wa taifa netball



NETBALL KIWANJANI TCC CHANGOMBE

Kozi ya uongozi katika michezo


Washiriki wa semina ya uongozi katika michezo wamesema mafunzo wanayoyapata yataleta mapinduzi katika maendeleo ya michezo hapa nchini.
RAIS wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchini BFT, JOAN MINJA na kocha wa mchezo wa tenisi BOAZI MWAKUSA wamesema wamejifunza mambo mbalimbali ya kiongozi katika michezo kama vile kuandaa mpango mkakati wa maendeleo wa muda mfupi na muda mrefu ambao awali walikua hawajui njisi ya kufanya hivyo.

Semina hiyo ya uongozi katika michezo inaendeshwa na kamati ya Olympiki Tanzania kwa ushirikiano na OLYMPIC SOLIDARITY ikiwa na lengo la kuwapiga msasa viongozi wa vyama vya michezo Tanzania na inafanyika katika uwanja wa Uhuru jijini DSM.

USAFI DAR


Hii ni garaji bubu katika eneo la mwembechai,vipi usalama wa mazingira katika eneo lake? kwa bali ni Hotel ya ITUMBI ambayo pia wachezaji wa timu ya taifa ya vijana NGORONGORO HEROES waliweka kambi kabla ya kuivaa Ivory Coast mwishoni mwa wiki

VIFAA VYA MAZOEZI


JE VIFAA HIVI VINAVIWANGO?

Hupiti hapa


Wachezaji Jeshi stars na polisi dar wakiwania mpira

Netball


Kutokana na kutokuwa na uzoefu wa mashindano makubwa baadhi ya wachezaji wa timu za NETBALL zinazoshiriki mashindano ya klabu bingwa ya TAIFA wameanza kukata tamaa kwa timu zao kutwa ubingwa.

Wachezaji hao ROSE ISRAE wa EMIMA ambayo imeshapoteza michezo yote iliyocheza anasema uzoefu umewaangusha huku JAMILA ISSA wa RAS LINDI akisema timu za mikoani hazina uzoefu wa kutosha wa kutwa ubingwa huo.

Baadhi ya michezo iliyochezwa leo asubuhi timu ya RAS LINDI imeilaza SIFA kwa mabao 35 kwa 12,FBS ikapokea kipigo cha mabao 25 kwa 17 toka kwa MAGEREZA,JESHI STARS imeifunga POLISI DAR ES SALAAM kwa mabao 24 kwa 18 huku TUMBAKU MOROROGO ikiifunga EMIMA magoli 44 kwa 14.
Katika michezo mingine MAPINDUZI imefungwa na POLISI MBEYA kwa mabao 18 kwa 14 na timu ya MAGANGA haikutokea uwanjani kucheza na POLISI MWANZA kwamaana hiyo POLISI MWANZA wamepata ushindi wa mezani wa mabao 40 kwa bila.

Michezo hiyo ya klabu bingwa ya Netball inafanyika katika viwanja vya TCC CHANG’OMBE jijini DSM

Monday, July 26, 2010

SIMBA KUMEKUCHA


Jengo la makao makuu ya klabu ya simba likifanyiwa ukarabati kwa kupakwa rangi,linapendeza,jengo hili linafaa hata kuishi wachezaji wa klabu hiyo au kufanyiwa biashara na kuingizia kipato.

Mitindo katika ujenzi


Hii siyo meli bali ni jengo la makao makuu ya kampuni ya simu ya Zain lililopo katiba barabara ya moroko jijini DSM,linavutia kwa kuliangalia.

Ujenzi ndani ya kariakoo


Mafundi na vibarua katika eneo la soko la kariakoo wakimwaga zege katika jengo la ghorofa linaloendelea kujengwa.magorofa mengi yamekua yakiendelea kujengwa katika eneo hilo mengi yakiwa ni ya kibiashara.

Sikukuu ya mashujaa yafana DSM


Sikukuu ya kukumbuka mashujaa ilifanyika jana jijini dsm huku Amir Jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Rais Jakaya Kikwete akipokea saluti kutoka kwa askari cha jeshi la wanachi wa Tanzania.
Sherehe hizo zilifanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini DSM hiyo jana.

NGORONGORO HEROES yafungwa Ivory Coast


Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 NGORONGORO HEROES imeanza vibaya mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana baada ya hiyo jana kuzabwa bao moja kwa bila na timu ya taifa ya vijana ya IVORY COAST mjini ABJAN.
NGORONGORO HEROES itabidi ifanye kazi ya ziada kuhakikisha inapata ushindi nyumbani kama inataka kusonga mbele katika michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika nchini LIBYA mwakani.Mchezo wa marundiano utachezwa baada ya wiki mbili zijazo jijini DSM

Thursday, July 22, 2010

Daraja la mto wami


Hilo ni daraja la mto wami lilopo katika barabara ya Dar-Tanga-Arusha,madereva wanatakiwa kuendesha kwa ungalifu magari yao katika eneo hilo.

NGORONGORO HEROES


Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 maarufu kama ngorongoro heroes imeondoka leo kwenda Abjan Ivory Coast tayari kuivaa timu ya taifa ya vijana ya nchi hiyo siku ya jumapili.

Mambo ya bangamoyo


Njedengwa alipotembelea bangamoyo

Wednesday, July 21, 2010

TBL yamwaga vifaa kwa Simba na Yanga


Msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara,hatimaye timu za Simba na Yanga zapewa vifaa na mdhamini wao kampuni ya bia ya TBL vyenye thamani ya shilingi milioni 64 tayari kwa msimu wa ligi ya kuu tanzania bara ambao unaanza kutimua vumbi AUGUST 21 kote nchini

KUSAKA VIPAJI kwa vutia wamarekani


Mambo ya kusaka vipaji,HABESHA TANZANIA yaziduliwa kwa ajili ya kusaka vipaji vya vijana katika fani ya mziki wa BONGO FLEVA.

Kazi imewaka moto


Wapinga picha wakifanya vitu vyao,waangalie walivyo makini kupinga picha nzuri.

YANGA wapewa vifaa


VIFAA SIMBA


Simba na Yanga zapewa vifaa tayari kwa ligi kuu Tanzania bara.
Watani wa jadi katika soka la Tanzania Simba na Yanga leo wamekabidhiwa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 64 na wadhamini wao kampuni ya bia ya TBL tayari kwa mikiki mikiki ya ligi kuu Tanzania bara ambayo inaanza kutimu vumbi kuanzia AGUST 21.
Maneje wa bia ya Kilimanjaro GEORGE KAVISHE amesema wametoa vifaa hivyo kama mkataba wao na vilabu hivyo unavyosema
Kwa upandea wao mkamu mwenyekiti wa SIMBA GEOFREY NYANGE maarufu kama KAMBURU na mwenyekiti wa YANGA LLOYD NCHUNGA wamesema vifaa hivyo watavitumia kwa ajili ya kuendeleza soka la Tanzania. (VOX POPS)Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara wao wanateremka dimbani kuivaa African Lyon nyumbani kwenye dimba la UHURU jijini DSM wakati watani wao YANGA watasafiri hadi DODOMA kupepetana na POLISI DODOMA katika dimba la Jamhuri

NGORONGORO HEROES YAANGWA


Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana wakimsikilaza mgeni rasmi wakati wa sherehe kuwaanga kabla hawajaivaa Ivory Coast siku ya jumapili.

NGORONGORO HEROES YAANGWA


Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 maarufu kama ngorongoro heroes inaendela na kampeni yake ya kutafuta tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la mataifa ya AFRIKA na inashuka dimbani dhidi ya IVORY COAST siku ya jumapili kwenye dimba la FELEX HOUPHOUET BOIGNY mjini ABJAN.
Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa NGORONGORO HEROES mkurungezi wa michezo katika wizara ya habari utamaduni na michezo LEORNARD THADEO amewataka vijana hao kucheza kwa bidii na nidhamu ya hali juu ili kushinda mchezo huo ugenini na kufanya kazi iwe rahisi wataporundiana jijini DSM wiki baada ya wiki mbili zijazo.
Kocha mkuu wa NGORONGORO HEROES, RODRIGO STROCKELER na nahodha wa timu hiyo HIMID MAO wamesema wao ni jeshi la uhakika na wemejiandaa vyema kushinda mchezo huo.
Msafara wa wachezaji 20 na viongozi saba NGORONGORO HEROES unaondoka alfajiri ya kesho tayari kuikabili timu ya taifa ya vijana ya IVORY COAST siku ya jumapili.NGORONGORO HEROES iwapo itashinda mchezo huo itakutana na mshindi kati ya timu ya taifa ya vijana ya NGAMBIA ambayo inateremka dimbani kuivaa SERE LEONE,fainali za AFRIKA kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 zitafanyika nchni LIBYA mwakani

Monday, July 19, 2010

Ushirikiano


Timu ya kriket ya Export Trading ikishangilia ubingwa wao katika mashindano ya kimataifa ya kriketi kati ya Tanzania na Pakstan.

Uchaguzi Yanga


Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Joel Bendera akisisitiza jambo kwa wanachama wa Yanga kabla ya kufanyika kwa uchanguzi wa klabu hiyo juzi

Uchaguzi Yanga


Mwenyekiti wa kamati ya uchanguzi wa Yanga Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo kabla ya uchnguzi hiyo juzi katika ukumbi wa PTA sabasaba Jijini DSM.

Msafara


Hizi ndizo heka heka za misafara ya Viongozi wetu

Uchaguzi Yanga


LLYORD CHUNGA ndiye mwnyekiti mpya wa YANGA baada ya kushinda Uchanguzi.
Mwasheria LLYORD CHUNGA ndiye mwenyekiti mpya wa klabu ya YANGA baada hiyo jana kuchanguliwa na wanachama wa YANGA katika uchanguzi uliofanyika katika ukumbi wa PTA sasaba jijini DSM
Afisa habari wa YANGA LUIS SEDEU amesema CHUNGA ameibuka kidedea baada ya kujinyakulia kura 1437 baada ya kuwabwanga washindani wake EDIGAR CHIBULA, FRANCIS KIFUKWE, ABEDI ABEDI na MBARAKA IGANGULA.
SEDEU amesema DAVIS MOSHA amechanguliwa kama makamu mwenyekiti baada ya kupata kura 2142 na kumshinda mpinzania wake COSTANTINTINE MALIGO aliyejinyakulia kura 55
Katika nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji SEDEU amewataja walichanguliwa kuwa ni mchezaji wa zamani wa YANGA na Taifa Stars ALLY MAYAYI,SARA RAMADHANI,MOHAMED BINDA,CHARLES MGONDO,SALUM RUPIA,TITO OSORO TINESI RUTASHABORWA na mwimbaji maarufu wa taarabu nchini MZEE YUSUFU
Viongozi waliochanguliwa wanachukua nafasi ya uongozi wa YANGA uliomalizia muda wake ambao ulikuwa chini ya mwenyekiti IMAN MADEGA.
=

Thursday, July 15, 2010

NGUMI MAZOEZINI


Wachezaji wa timu ya taifa ya ngumi waendelea na mazoezi katika uwanja wa ndani wa taifa.
timu hiyo ipo kambini kwa muda sasa ikijiweka sawa na mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika india mwezi OCTOBA.

Mwakalebele baibai TFF


Ajira ya katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF FREDRICK MWAKALEBELA yafikia ukingoni na sasa bosi mpya ajira yake kutangazwa JULY 17.katika picha kulia ni Rais wa TFF LEODIGAR TENGA na kushoto kwake ni katibu aliyemaliza muda wake FREDRICK MWAKALEBELA,Mwakalebela ametangaza nia ya kungombea Ubunge jimbo la IRINGA mjini.

Tanzania kufaindika na finali za kombe la dunia


Shirikisho la soka nchini TFF limebainisha kuwa Tanzania itafaidika na michuano ya kombe la Dunia iliyomalizika nchini Afrika Kusini katika Nyanja za ufundi na mbinu za kisoka.Rais wa TFF LEODGAR TENGA amesema alipokuwa nchini Afrika Kusini alikutana na viongozi wa soka wa mataifa mbalimbali ambao wameonesha nia ya kushirikiana na Tanzania kuhakikisha soka la tanzania linasonga mbele hasa kuhakikisha vijana wengi wanacheza soka la kulipwa Ulaya kwa manufaa ya TAIFA STARS

Wednesday, July 14, 2010

AZAM wawaka juu ya NGASSA


Mwenyekiti wa klabu ya AZAM FC Said Mohmed asema suala la mazungumzo na Yanga juu ya Mrisho Ngassa halipo,na tayari msimu wa usajili umemalizika tangu leo.

usajilia YANGA


Kocha mkuu wa YANGA COSTADIN PAPIC akieleza mikakati yake ya usajili unaolenga kuimarisha kikosi kwa ajili ya ligi kuu na michuano ya kimataifa,Yanga ina wachezaji kazaa wanaofanya majaribio kutoka nchi za GHANA na UGANDA.

Heka heka za usajili


Kijana anayesukuma soka la kulipwa huko Marekani DENIS GODFREY asema soka la Tanzania limebadilika ndio maana anapenda kusajiliwa Yanga au timu yeyote ya ligi kuu lego lake pia ni kuichezea TAIFA STARS.

MISS TEMEKE 2010

Miss Temeke GENEVIVA EMMANUEL
akihojiwa na MBOZI KATALA wa TBC,muda mfupi kabla ya kuingia kwenye kinyng'anyiro cha Miss Temeke,hebu angalia urefu wa mrembo huyo,huenda akaibuka kidedea MISS Tanzania 2010

KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI YANGA


Aliyekua mgombea makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Ayabu Nyezi akiwa uso kwa uso na Davis Mosha muda mfupi baada ya kujitoa katika kinyang'anyiro hicho na kumpisha Mosha kwa lego la kuleta umoja katika klabu hiyo.Uchanguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika JULY 18.

Thursday, July 1, 2010

Kazi ni kazi tu

Mwaandishi wa habari za michezo Ndimbo akiendesha gari la Majira ili kuharakisha habari.inafurahisha sana, hapa tunabana matumizi ya kuwa na dereva mwingine, safi sana inapaswa kuingwa na vyombo vingine vya habari TZ

NGUMI


Vijana wakionyeshana ubabe katika masumbwi kuwania ubingwa wa taifa,mashindano hayo yanafanyika katika ukumbi wa DDC Keko jijini DSM.

MATUNDA


Kula matunda kwa afya yako,matunda hayo yanauzwa pembeni ya jengo la MILLENIUM TOWERS,kijitonyama.sahani moja ni shilingi mia tano tu

Gofu


Hivyo ni vifaa vya gofu ambavyo vimekabidhiwa jana kwa Chama cha Gofu Tanzania TGU kwa ajili ya kuendeleza mchezo huo kwa vijana hapa nchini.

Maximo


kocha mkuu wa timu ya taifa ya tanzania Maximo akifurahia zawadi aliyopewa na wadhamini wa Taifa Stars ,Kulia ni Jaji Mark Mbomani na kushoto ni Teddy Mapunda

Maximo atuaga watanzania


Kocha mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars Marcio Maximo ambaye amemaliza muda wake akiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari wa michezo wa TBC,kulia ni Malyo Njedengwa na kushoto ni Mbozi Katala

NGORONGORO HEROES KIBARUANI


Kocha mkuu wa Ngorongoro Heroes Rodrigo akitangaza kikosi cha NGORONGORO HEROES hii leo katika ofisi za TFF jijini DSM,kulia kwake ni Afisa habari wa TFF Florian Kaijage.
Ngorongoro heroes kuingia kambani siku ya jumataa ya wiki ijayo tayari kujiandaa na mchezo dhidi ya IVORY COAST.

NGORONGORO HEROES KIBARUANI


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka ishirini Ngorongoro Heroes RODRIGO STROKELER na msaidizi wake ADOLF RISHARD wakitoa mawaidha kwa mshambuliaji wa timu hiyo THOMAS ULIMWENGU wakati wa mazoezi katika uwanja wa Karume,ULIMWENGU anategemewa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya NGORONGORO HEROES dhidi ya IVORY COAST mwishoni mwa mwezi huu katika kampeni ya kuwania kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwaka huu.