Saturday, March 28, 2015



Bondia MOHAMED MATUMLA, SNAKE BOY JUNIOR amewatoa watanzania kimasomaso baada ya kutandika bondia WANG XIN HUA kutoka CHINA na kuibuka na ubingwa wa WBF UZANI wa BANTAM katika pambano lilofanyika katika ukumbi wa DIAMOND JUBLIEE jijini DSM.
Katika pambano hilo ambalo lilikuwa na ushindani wa hali ya juu, MATUMLA, amemchapa WANG XIN HUA kwa ALAMA.
Kwa usindi huo MATUMLA amepata nafasi ya kucheza pambano la utangulizi wakati wa pambano kati ya FLOYD MAYWEATHER, dhidi ya MANNY PACQUIAO utakaochezwa MAY MBILI nchini MAREKANI.
=====
Wakati huo huo bondia MADA MAUGO ametoa kichapo cha mwaka baada ya kumtandika bila huruma kwa KO Mpizani wake JAPHET KASEMBA katika mzunguko wa NANE.

=====
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo HERMAN MWASOKO aliomba shirika la hifadhi ya jamii NSSF kubadili mfumo wa mashindano ya kuwania KOMBE LA NSSF kutoka kwenye mtindo wa mtoano hadi ligi ili kuongeza ushindani.
MWASOKO aliyasema hayo baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi ,huku nahodha wa TBC WARRIORS, JAMES MAPEPELE na Habari Zanzibar AMRI MAKAME wamesema walijiandaa vyema ndio maana wakaibuka na ushindi

TIMU ya TBC WARRIORS imenyakua nafasi ya tatu, IPP MEDIA imeshika nafasi ya pili wakati HABARI ZANZIBAR ndio mabingwa michuano katika soka kwa mwaka huu.
====
TIMU ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS kesho inashuka dimbani kuibili timu ya taifa ya Malawi the flames katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utaochezwa katika uwanja wa CCM KIRUMBA mjini MWANZA.
TAYARI KIKOSI cha wachezaji wa timu ya Taifa ya MALAWI, THE FLAMES kimewasili jijini MWANZA  kwa mchezo dhidi ya TAIFA STARS.

Mbali na wachezaji walioitwa na kocha wa MALAWI wanaocheza soka la ndani ya nchi yao pia amewajumuisha wachezaji wanaocheza soka la kulipwa  katika nchi za AFRIKA KUSINI,  JAMHURI ya KIDEMOKRASIA ya CONGO,  MSUMBIJI na ZIMBABWE.
====
STARS TAYARI KUWAKABILI MALAWI KESHO CCM KIRUMBA
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo asubuhi imefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya taifa ya Malawi (The Flames) mchezo utakaochezwa kesho jumapili saa 10.30 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Tiketi za mchezo tayari zimeshaanza kuuzwa katika vituo vya Uwanja wa Nyamagana na uwanja wa CCM Kirumba kwa bei za sh. 5,000 kwa mzunguko, sh. 12,000 kwa jukwaa kuu na sh.20,000 kwa viti vya jukwaa kuu maalum.

Taifa Stars inashika nafasi ya 100 katika msimamo wa viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi Machi, huku Malawi (The Flames) wakishika wakiwa nafasi ya 91 kwenye vinago hivyo.

Akiongea na waandishi wa habari leo kaika hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri , na sasa kilichobakia ni mchezo wenyewe wa kesho.

Mayanga amesema vijana wake wote 22 waliopo kambini wapo fiti, wamefanya mazoezi kwa siku tano katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wachezaji wapo kwenye ari na morali ya juu, kikubwa wanachosubiri ni kesho tu kushuka dimbani kusaka ushindi.

Aidha Mayanga amewaomba wapenzi wa mpira wa miguu waliopo jijini Mwanza na mikoa ya jirani ya kanda ya ziwa, kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani kuja kuwapa sapoti vijana kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo.

Tayari waamuzi na kamishina wa mchezo wameshawasili jijini Mwanza, mwamuzi wa kati atakua ni Munyazinza Gervais kutoka nchini Rwanda, akisaidiwa na mshika kibendera wa kwanza Hakizimana Ambroise (Rwanda), mshika kibendera wa pili Niyitegeka Bosco (Rwanda), mwamuzi wa akiba  Martin Saanya kutoka Morogoro huku na Kamishina wa mchezo ni Afred Rwiza kutoka Mwanza.
Mshambuliaji wa TAIFA STARS ,MBWANA SAMATTA AKISHANGILIA BAO