Wednesday, October 10, 2012


Klabu ya SIMBA yawasili jijini TANGA.
KATIKA hatua nyingine mabingwa wa soka nchini SIMBA ya DSM imewasili mjini TANGA tayari kwa mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya wenyeji wa COSTAL UNION mchezo utakaochezwa katika uwanja wa MKWAKWANI mjini humo siku ya jumamosi.
Msemaji wa klabu ya SIMBA, EZEKIEL KAMWAGA amewataka mashabiki wa klabu hiyo kutojiingiza katika vitendo vitakavyosababisha klabu hiyo kutozwa faini.
Kiungo wa simba RAMADHANI CHOMBO REDONDO hakuondoka na kikosi cha SIMBA kwenda TANGA kwa kuwa anasubuliwa na MALARIA,lakini akaeleza kurejea kwa mshambuliaji wa timu hiyo MRISHO NGASSA ambaye atacheza katika mchezo huo.
Michezo mingine itakayochezwa jumamosi ni katika uwanja wa JAMHURI mjini MOROGORO ambapo POLISI MORO itacheza na AZAM FC, TANZANIA PRISONS itacheza na JKT OLJORO.
Michezo mingine RUVU SHOOTING itacheza na AFRICA LYON na MTIBWA SUGAR itacheza na MGAMBO JKT.
====
Wagombea sita soka la wanawake wapingwa
WAGOMBEA sita wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) wamewekewa pingamizi na wadau wa mchezo huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, wagombea hao ni JOAN MINJA anayewania nafasi ya Mwenyekiti ambaye amewekwa pingamizi na wadau sita. Pia ISABELLAH KAPERA ambaye anagombea uenyekiti amewekewa pingamizi moja.

Wagombea watatu wa nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nao wamewekewa pingamizi.

Wagombea hao ni JULLIET MNDEME ana pingamizi sita , Zena Chande ana pingamizi NNE na Jasmin Soud mwenye pingamizi tatu.

Naye Rahim Maguza anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji amewekewa pingamizi moja.

Licha ya pingamizi hizo, wagombea wote wanatakiwa kuhudhuria usaili wakiwa na vyeti vyao halisi vya kitaaluma utakaofanyika Oktoba 12, 13 na 14 mwaka huu kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi.
 ===

JOKATE azindua ubunifu mpya wa mitindo.
MWANAMITINDO na MBUNIFU nchini JOKATE MWEGELO amezindua aina nyingine ya mitindo ya NYWELE inayokwenda sambamba na mitindo ya ubunifu wa nguo.
JOKETI ambaye pia aliwahi kuwa mshindi wa pili katika shindano la Taifa kwa mwaka 2006 amesema nia yake ni kutaka kutanua wigo wa ubunifu kwa kutumia fani ya urembo.
Akizundua kampuni hiyo JOKATE akaeleza kwa nini ameiita jina la KIDOTI.
Kisha akaeleza madhumuni  ya kuazisha kampuni  hiyo katika tasinia ya urembo,ubunifu na mitindo hapa nchini.
Baada ya hapo warembo wakajimwanga jukwaani kuonyesha mitindo ya nywele


CHEKA kuwania ubingwa wa DUNIA dhidi ya mjerumani.
BINGWA wa ngumi za kulipwa nchini anayetambuliwa na shirikisho la ngumi la dunia (UBO) FRANCIS CHEKA amesaini mkataba wa kucheza pambano la kuwania ubingwa unaotambuliwa na shirikisho la ngumi la IBF uzito wa kati.
Katika pambano hilo CHEKA ambaye hivi karibuni alimchakaza KARAMA NYILAWILA kwa KO na kupata ubingwa wa UBO sasa atacheza na bondia kutoka nchini JERUMAN, BENARD SIMON katika pambano litakalochezwa nchini UJERUMAN NOVEMBA 17 mwaka huu.
BONDIA, CHEKA anasaini mkataba kwaajili ya kucheza pambano dhidi ya mjerumani BERNARD SIMON.
Pambano hilo limetafutwa na promota mpya wa FRANCIS CHEKA, JUMA MABAKILA mwenyewe akisema anataka, kila baada ya miezi miwili bondia CHEKA kupanda ulingoni.
Rais wa shirikisho la ngumi, IBF AFRICA ONESMO NGOWI naye akazungumzia pambano jingine la OMAN ambalo FRANCIS CHEKA atazichapa baada ya pambano na MJERUMAN
Tayari FRANCIS CHEKA amejizolewa sifa nyingi katika masumbwi nchini baada ya kuwachapa mabondia mashuhuri kama KARAMA NYILAWILA, MADA MAUGO na RASHID MATUMLA.