Tuesday, July 30, 2013



MTIHANI WA UWAKALA WA WACHEZAJI, MECHI SEPT 26
Mtihani wa uwakala wa wachezaji (players agent) na uwakala wa mechi (match agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Septemba 26 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kutakuwa na jumla ya maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana na kanuni za kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF kuhusiana na kanuni mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.

Kwa ambao wangependa kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza ambayo ni moja kati ya lugha nne rasmi za FIFA wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga.

Mtihani huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi, na muda wa kufanya mtihani hautazidi dakika 90.

Mpaka sasa Tanzania ina mawakala watano wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.

WAAMUZI VPL KUFANYA MTIHANI WA UTIMAMU WA MWILI
Waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 wanatakiwa kuhudhuria mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) utakaofanyika katika vituo viwili.

Mtihani huo utafanyika Agosti 12,13 na14 mwaka huu katika vituo vya Dar es Salaam na Morogoro. Kituo cha Mwanza kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.

Kituo cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.

Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo. Pia waamuzi waliofungiwa (sio maisha) wanatakiwa kushiriki katika mtihani huo.

RATIBA LIGI DARAJA LA KWANZA AGOSTI 14
Ratiba ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2013/2014 inayoshirikisha timu 24 zilizo katika makundi matatu zikicheza kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini) inatarajiwa kutolewa Agosti 14 mwaka huu.

Kundi A linaundwa na timu za Burkina Moro ya Morogoro, JKT Mlale (Ruvuma), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mufindi (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mkamba Rangers (Morogoro), Polisi (Iringa) na Polisi (Morogoro).

African Lyon (Dar es Salaam), Friends Rangers (Dar es Salaam), Green Warriors (Dar es Salaam), Ndanda (Mtwara), Polisi (Dar es Salaam), Tessema (Dar es Salaam), Transit Camp (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam) zinaunda kundi B.

Timu za kundi C ni JKT Kanembwa (Kigoma), Mwadui (Shinyanga), Pamba (Mwanza), Polisi (Dodoma), Polisi (Mara), Polisi (Tabora), Stand United (Shinyanga) na Toto Africans (Mwanza).

Tunapenda kukumbusha kuwa dirisha la usajili kwa madaraja yote ni moja ambapo usajili wa hatua ya kwanza ni kuanzia Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka huu wakati hatua ya pili ni Agosti 14 hadi 29 mwaka huu. Dirisha dogo litafunguliwa Novemba 15 hadi Desemba 15 mwaka huu.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Friday, July 26, 2013

HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI



WACHEZAJI wa TAIFA STARS leo wanaingia katika uwanja wa NAMBOOLE nchini UGANDA kucheza na THE CRANES katika mchezo wa kufa ama kupona.
Mchezo huo ni wa mwisho kwa timu hizo ambazo zinatafuta tiketi ya kucheza fainali za mashindano ya wachezaji wanaocheza soka la ndani ya CHAN.
Kocha KIM PAULSEN amewaelekeza wachezaji wa TAIFA STARS kucheza kwa kushambulia muda mwingi ili waweze kufikia azma ya kucheza fainali hizo zitakazochezwa mwakani nchini AFRIKA KUSINI.
Katika mchezo wa awali uliochezwa wiki mbili zilizopita TAIFA STARS ilichapwa goli MOJA kwa BILA na THE CRANES na hivyo kutakiwa kupata ushindi wa zaidi ya magoli MAWILI kwa BILA ili iweze kusonga mbele na mashindano ya CHAN.
Hii ni fursa ya mwisho kwa TAIFA STARS kwani ina mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba wa kombe la dunia dhidi ya GAMBIA utakaochezwa mwezi Septemba.
Mchezo huo utaanza saa kumi jioni kwa saa za Afrika mashariki na utachezeshwa na mwamuzi kutoka MADAGASCA KANOSO ABDUL OHABEE.
TAIFA STARS jana jioni imefanya mazoezi katika uwanja wa NAMBOOLE tayari kwa mchezo huo ambao TBC ONE utakuletea moja kwa moja mchezo huo kutoka nchini UGANDA.
 == == = =

Bingwa mara sita wa riadha katika mashindano ya OLYMPIC USAIN BOLT jana ameendeleza ubabe wake katika mbio za mita 100 za michezo ya kuadhimisha mwaka mmoja wa OLYMPIC yaliyofanyika LONDON kwenye viwanja vya OLYMPIC
Mwaka mmoja baada ya mashindano ya OLYMPIC kufanyika LONDON mwaka 2012 BOLT amekimbia sekunde 9.85 kwenye mashindano hayo hapo jana.
Mwingereza JAMES DASALU alijiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho kutokana na kupata majeraha.
BOLT alianza taratibu lakini bingwa huyo wa OLYMPIC aliwashinda wapinzani wake kwenye hatua za mwisho MICHAEL RODGERS aliyekamata nafasi ya pili.
NESTA CARTER wa JAMAICA yeye alikamata nafasi ya tatu akitumia muda wa sekunde 9.99 wakati DWAIN CHAMBERS mwingereza pekee aliyekua amesalia kwenye mbio hizo baada ya DASALU kujitoa alikamata nafasi ya tano kwa kutumia muda wa sekunde 10.10.
BOLT ambaye sasa atatazamia kurejesha ubingwa wa dunia mwezi katika mashindano yatakayofanyika MOSCOW mwezi ujao amefurahishwa na kiwango alichokionesha jana mbele ya mashabiki ELFU SITINI.
 == = == == =
Tukiangazia mashindano ya LANGALANGA hapo jana dereva wa RED BULL SEBASTIAN VETTEL alitawala mashindano ya majaribio ya HUNGARIAN GRAND PRIX
Bingwa huyo wa dunia wa mashindano ya FORMULA ONE alimzidi dereva mwenzake MARK WEBBER BILA shida yoyote katika raundi zote.
Dereva wa LOTUS ROMAIN GROSJEAN alikamata nafasi ya tatu akiwazidi FERNANDO ALONSON na FELIPE MASSA wa timu ya FERRARI pamoja na dereva wa MERCEDES LEWIS HAMILTON na NICO ROSBERG.
KIMI RAIKONEN wa LOTUS ambaye anafukuzia ubingwa wa dunia alikimata nafasi ya nane baada ya kuzidiwa na dereva wa MCLAREN JENSON BUTTON.
VETTEL aliwazidi madereva wa timu ya FORCE INDIA ADRIAN SUTIL na PAUL DI RESTA.
 = === ==
Katika masuala ya usajili kwenye soka klabu ya MANCHESTER UNITED jana imepata habari mbaya baada ya klabu ya BARCELONA kuendelea kusisitiza kuwa kiungo wao CESC FABREGAS hatouzwa kwa gharama yoyote.
Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo JOSEP MARIA BARTOMEU amesema hayo jana kuwa CESC hatouzwa kwa gharama yoyote.
Siku ya Alhamisi meneja wa UNITED DAVID MOYES alisema kuwa mazungumzo kwa ajili ya dili la kumsajili FABREGAS yanaendelea lakini jana klabu hiyo ya LA LIGA imesema kuwa hakuna offer itakayokubaliwa kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26.
BARTOMEU amesema kuwa nia ya UNITED kutaka kumsajili CESC iko wazi kwa kuwa ni mchezaji mzuri lakini nia hiyo haiwasumbui wao BARCELONA.
Makamu huyo wa mwenyekiti akaendelea kusema kuwa haitojalisha kiasi gani watatoa kwa kiungo huyo kwa kuwa hawatomuuza.
Mabingwa wa ligi ya ENGLAND wameshindwa na offer mbili walizotoa kwa BARCA huku ofa ya mwisho ikiripotiwa kuwa pauni milioni 30 na maongezo.
Naye meneja mpya wa klabu hiyo GERALDO TATA MARTINO akaendeleza msimamo wa klabu hiyo kwa kusema kuwa kwa kuwa klabu imekataa ofa mbili za CESC basi yeye atakataa ofa ya tatu itakayokuja kwa ajili ya kiungo huyo.
 = = == = = == =
Wakati huohuo timu hiyo ya MANCHESTER UNITED jana imeambulia sare ya bao mbili kwa mbili shukrani kwa WILFRED ZAHA aliyefunga bao la kusawazisha kwenye dakika za majeruhi.
KENYU NUGIMOTO alianza kuipatia timu yake ya CEREZO OSAKA bao la kuongoza kwenye dakika ya 33 ya mchezo bao ambalo lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko.
Katika kipindi cha pili SHINJI KAGAWA ambaye ni mzawa wa JAPAN aliisawazishia UNITED akiunganisha vizuri krosi ya mkongwe RYAN GIGGS kwenye dakika ya 54.
UNITED ilipata nafasi ya kusawazisha lakini penati iliyopigwa na SHINJI KAGAWA iliokolewa na kipa wa CEREZO.
CEREZO OSAKA walizidi kuweka ngumu kwa MANCHESTER kwani kwenye dakika ya 64 shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni lilipigwa na TAKUMI MINAMINO.
Lakini kwenye dakika ya 91 WILFRED ZAHA kwa mara ya kwanza aliingia kwenye orodha ya wafungaji wa mabao wa UNITED kwa mwaka huu kwenye michezo ya kujipima nguvu kwa kuipatia UNITED bao la pili na la kusawazisha.
UNITED imeshacheza michezo minne ambapo imefungwa michezo miwili na kushinda mmoja na kutoka sare mmoja hapo jana.
 == =====
ARSENAL jana imemaliza ziara yake barani ASIA kwa ushindi wa bao mbili kwa moja katika dhidi ya URAWA DIAMONDS ya JAPAN ukiwa ni ushindi wa nne katika michezo minne iliyocheza timu hiyo.
Katika kipindi cha kwanza timu hizo mbili zilichoshana nguvu baada ya kumaliza kipindi hicho pasipo kufungana.
LUKAS PODOLSKI ambaye aliingia kipindi cha pili alianza kuipatia ARSENAL bao la kuongoza kwenye dakika ya 49.
Aidha URAWA walifanikiwa kusawasiaha bao hilo kwenye dakika ya 59 kupitia kwa YUKI ABE.
THE GUNNERS ilijipatia bao la ushindi kupitia kwa mshambuliaji mwingine aliyeingia kipindi cha pili CHUBA AKPOM aliyetumia vizuri makosa ya mlinzi wa URAWA DIAMONDS ya kurudisha mpira vibaya kwa kipa wake kwenye dakika ya 83.
THE GUNNERS sasa watarejea nyumbani kwa ajili ya michuano ya kombe la EMIRATES yatakayoanza wiki ijayo ambapo watakutana na NAPOLI na GALATASARY.
 = ==  === =

RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
















 
  TANZANIA FOOTBALL FEDERATION





    Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA





    Karume Memorial Stadium, Uhuru/Shaurimoyo Rd – Ilala





    P.O. Box 1574, Dar Es Salaam, Tanzania





    Telefax: +255 22 2861815, Email: tanfootball@tff.or.tz, Website: www.tff.or.tz





FIRST ROUND TANZANIA PREMIER LEAGUE 





VODACOM PREMIER LEAGUE (VPL) FIXTURE 2013/2014





24th AUGUST. 2013 - 03rd NOVEMBER, 2013.





NO DATE No.  HOME TEAM AWAY TEAM STADIUM REGION





1 24.08.2013 1 YOUNG AFRICANS ASHANTI UNITED NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  24.08.2013 2 MTIBWA SUGAR AZAM FC MANUNGU MOROGORO





  24.08.2013 3 JKT OLJORO COASTAL UNION SH. AMRI ABEID ARUSHA





  24.08.2013 4 MGAMBO JKT JKT RUVU  MKWAKWANI TANGA





  24.08.2013 5 RHINO RANGERS SIMBA SC A.H. MWINYI TABORA





  24.08.2013 6 MBEYA CITY KAGERA SUGAR SOKOINE MBEYA





  24.08.2013 7 RUVU SHOOTINGS TANZANIA PRISONS MABATINI PWANI





 





2 28.08.2013 8 MTIBWA SUGAR KAGERA SUGAR MANUNGU MOROGORO





  28.08.2013 9 RHINO RANGERS AZAM FC A.H. MWINYI TABORA





  28.08.2013 10 JKT RUVU TANZANIA PRISONS MABATINI PWANI





  28.08.2013 11 MBEYA CITY RUVU SHOOTINGS SOKOINE MBEYA





  28.08.2013 12 MGAMBO JKT ASHANTI UNITED MKWAKWANI TANGA





  28.08.2013 13 JKT OLJORO SIMBA SC SH. AMRI ABEID ARUSHA





  28.08.2013 14 YOUNG AFRICANS COASTAL UNION NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





(29.August-09.Sept. National Team Camp for WCQ against Gambia away)





3 14.09.2013 15 SIMBA SC MTIBWA SUGAR NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  14.09.2013 16 COASTAL UNION TANZANIA PRISONS MKWAKWANI TANGA





  14.09.2013 17 RUVU SHOOTINGS MGAMBO JKT MABATINI  PWANI





  14.09.2013 18 JKT OLJORO RHINO RANGERS SH. AMRI ABEID ARUSHA





  14.09.2013 19 MBEYA CITY YOUNG AFRICANS SOKOINE MBEYA





  14.09.2013 20 KAGERA SUGAR AZAM FC KAITABA KAGERA





  14.09.2013 21 ASHANTI UNITED JKT RUVU AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





 





4 18.09.2013 22 TANZANIA PRISONS YOUNG AFRICANS SOKOINE MBEYA





  18.09.2013 23 SIMBA SC MGAMBO JKT NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  18.09.2013 24 KAGERA SUGAR  JKT OLJORO KAITABA KAGERA





  18.09.2013 25 AZAM FC ASHANTI UNITED AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





  18.09.2013 26 COASTAL UNION RHINO RANGERS MKWAKWANI TANGA





  18.09.2013 27 MTIBWA SUGAR MBEYA CITY MANUNGU MOROGORO





  18.09.2013 28 RUVU SHOOTINGS JKT RUVU MABATINI PWANI





 





5 21.09.2013 29 MGAMBO JKT RHINO RANGERS MKWAKWANI  TANGA





  21.09.2013 30 TANZANIA PRISONS MTIBWA SUGAR SOKOINE MBEYA





  22.09.2013 31 JKT RUVU JKT OLJORO AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





  21.09.2013 32 SIMBA SC MBEYA CITY NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  22.09.2013 33 AZAM FC YOUNG AFRICANS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  21.09.2013 34 KAGERA SUGAR ASHANTI UNITED KAITABA KAGERA





  22.09.2013 35 COASTAL UNION RUVU SHOOTINGS MKWAKWANI  TANGA





     





6 28.09.2013 36 YOUNG AFRICANS RUVU SHOOTINGS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  28.09.2013 37 RHINO RANGERS KAGERA SUGAR A. H. MWINYI TABORA





  29.09.2013 38 ASHANTI UNITED MTIBWA SUGAR AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





  28.09.2013 39 MBEYA CITY COASTAL UNION SOKOINE MBEYA





  28.09.2013 40 MGAMBO JKT JKT OLJORO MKWAKWANI TANGA





  29.09.2013 41 JKT RUVU SIMBA SC NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  29.09.2013 42 TANZANIA PRISONS AZAM FC SOKOINE MBEYA





 





7 05.10.2013 43 RUVU SHOOTINGS SIMBA SC NATIONAL STADIUM DAR ES  SALAAM





  05.10.2013 44 JKT RUVU KAGERA SUGAR AZAM COMPLEX DAR ES  SALAAM





  05.10.2013 45 COASTAL UNION AZAM FC MKWAKWANI TANGA





  05.10.2013 46 JKT OLJORO MBEYA CITY SH. AMRI ABEID ARUSHA





  25.09.2013 47 RHINO RANGERS ASHANTI UNITED A. H. MWINYI TABORA





  06.10.2013 48 MGAMBO JKT  TANZANIA PRISONS MKWAKWANI TANGA





  06.10.2013 49 YOUNG AFRICANS MTIBWA SUGAR NATIONAL STADIUM DAR ES  SALAAM





 





8 09.10.2013 50 RHINO RANGERS MBEYA CITY A. H. MWINYI TABORA





  09.10.2013 51 JKT OLJORO RUVU SHOOTINGS SH. AMRI ABEID ARUSHA





  09.10.2013 52 AZAM FC MGAMBO JKT AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





  09.10.2013 53 MTIBWA SUGAR JKT RUVU MANUNGU MOROGORO





  12.10.2013 54 KAGERA SUGAR YOUNG AFRICANS KAITABA KAGERA





  12.10.2013 55 SIMBA SC TANZANIA PRISONS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  13.10.2013 56 ASHANTI UNITED COASTAL UNION AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





     





9 13.10.2013 57 RUVU SHOOTINGS RHINO RANGERS MABATINI PWANI





  13.10.2013 58 MGAMBO JKT MBEYA CITY MKWAKWANI TANGA





  13.10.2013 59 AZAM FC JKT RUVU AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





  13.10.2013 60 MTIBWA SUGAR JKT OLJORO MANUNGU MOROGORO





  16.10.2013 61 ASHANTI UNITED TANZANIA PRISONS AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





  19.10.2013 62 KAGERA SUGAR COASTAL UNION KAITABA KAGERA





  20.10.2013 63 SIMBA SC  YOUNG AFRICANS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





 





10 19.10.2013 64 JKT OLJORO AZAM FC SH. AMRI ABEID ARUSHA





  19.10.2013 65 MTIBWA SUGAR MGAMBO JKT MANUNGU MOROGORO





  19.10.2013 66 MBEYA CITY JKT RUVU SOKOINE MBEYA





  19.10.2013 67 ASHANTI UNITED RUVU SHOOTINGS AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





  23.10.2013 68 COASTAL UNION SIMBA SC MKWAKWANI TANGA





  23.10.2013 69 TANZANIA PRISONS KAGERA SUGAR SOKOINE MBEYA





  23.10.2013 70 YOUNG AFRICANS RHINO RANGERS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





 





11 26.10.2013 71 TANZANIA PRISONS MBEYA CITY SOKOINE MBEYA





  26.10.2013 72 COASTAL UNION MTIBWA SUGAR MKWAKWANI TANGA





  26.10.2013 73 JKT OLJORO ASHANTI UNITED SH. AMRI ABEID ARUSHA





  26.10.2013 74 YOUNG AFRICANS MGAMBO JKT NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  27.10.2013 75 RUVU SHOOTINGS  KAGERA SUGAR MABATINI PWANI





  27.10.2013 76 SIMBA SC AZAM FC NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  27.10.2013 77 RHINO RANGERS JKT RUVU A. H. MWINYI TABORA





 





12 30.10.2013 78 MGAMBO JKT  COASTAL UNION MKWAKWANI TANGA





  30.10.2013 79 TANZANIA PRISONS JKT OLJORO SOKOINE  MBEYA





  30.10.2013 80 AZAM FC RUVU SHOOTINGS AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





  30.10.2013 81 SIMBA SC KAGERA SUGAR NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  30.10.2013 82 MTIBWA SUGAR RHINO RANGERS MANUNGU MOROGORO





  30.10.2013 83 MBEYA CITY ASHANTI UNITED SOKOINE  MBEYA





  31.10.2013 84 JKT RUVU YOUNG AFRICANS NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





 





13 02.11.2013 85 JKT RUVU COASTAL UNION AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





  02.11.2013 86 ASHANTI UNITED SIMBA SC NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM





  03.11.2013 87 KAGERA SUGAR MGAMBO JKT KAITABA KAGERA





  03.11.2013 88 AZAM FC MBEYA CITY AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM





  03.11.2013 89 RHINO RANGERS TANZANIA PRISONS A. H. MWINYI TABORA





  03.11.2013 90 RUVU SHOOTINGS MTIBWA SUGAR MABATINI PWANI





  03.11.2013 91 YOUNG AFRICANS JKT OLJORO NATIONAL STADIUM DAR ES SALAAM