Tuesday, December 28, 2010

MICHEZO YA LEO


TAIFA STARS USO KWA USO NA UGANDA ALL AFRICA GAMES
Timu ya taifa ya Tanzania, TAIFA STARS imepangwa kucheza na UGANDA mwezi APRIL mwakani, katika mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki mashindano ya ALL AFRICA GAMES yatakayofanyika MAPUTO MSUMBIJI mwezi SEPTEMBA 2011.

Kaimu katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF SUNDAY KAYUNI amesema jijini DSM hii leo kwamba
TAIFA STARS imepangwa katika hatua ya mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo na shirikisho la soka barani Afrika CAF kutokana na kiwango chake kuwa cha kuridhisha.

KAYUNI amesema michezo ya awali ya michuano hiyo itaanza kutimua vumbi mwezi JANUARI mwakani. TANZANIA ipo katika kanda ya TANO ikiwa na timu za Eritrea, Kenya, Uganda.

Wakati huo huo KAYUNI amesema Kiungo mshambuliaji wa klabu ya soka ya SIMBA RASHID GUMBO ameitwa kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya Tanzania, TAIFA STARS inayojiandaa na mashindano ya maalumu ya NILE BASIN kuziba pengo la HENRY JOSEPH.

KAYUNI amesema HENRY JOSEPH ameshindwa kujiunga na kambi ya taimu ya taifa kutokana na matatizo ya kifaimilia hiyo kocha msadidizi SYLVESTER MASHI ameamua kumuita GUMBO ili kuziba pengo lake.
STARS inajiandaa na michuano maalumu ya NILE BASIN yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao kwa kuzishirikisha timu za Uganda,SUNDAN na wenyeji MISRI.

===

KOCHA WA YANGA ASISITIZA KUWAHITAJI WACHEZAJI WAKE WALIOKO STARS
Kocha mkuu wa klabu Yanga KOSTADIN PAPIC amesema itakuwa ni vigumu kwake kuiandaa timu yake kwa michuano ya kombe la shirikisho kiukamilifu baada ya wachezaji wake SABA kujiunga na mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS inayojiandaa na mshindano maalum NILE BASIN.
Akizumgumza na TBC baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu yake katika uwanja wa kaunda jijini DSM PAPIC amesema michuano hiyo isiyotabulika na shirikisho la soka dunia FIFA wa la CAF kwa kiasi kikubwa imevurunga mpagilio wa programme zake za mazoezi.
Kwa upande wao wachezaji NSA JOB na FRED MBUNA wameesema wao wanajiandaa vyema kuyakabili mashindano yaliyo mbele yao.
Yanga inaendelea na mazoezi yake kujiandaa na michuano ya ligi kuu Tanzania Bara na Kombe la shirikisho jijini DSM.

===

KENNETH MKAPA AWALAUMU WASHAMBULIAJI WAKE
Kocha wa timu ya YANGA B, KENNETH MKAPA amesema kutoka sare kwa timu yake dhidi ya AFRIKA LYON ni uzembe wa washambuliaji wake ambao hawakuwa makini wakati wa umaliziaji.
Amesema mechi hiyo ilikuwa ya msingi kwao kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi katika mashindano ya UHAI CUP lakini pia amesema wanaendelea kujipanga zaidi ili kushinda mechi zinazofuata.
Katika mchezo huo timu ya YANGA imetoka sare ya bila kufungana na timu ya AFRIKA LYON katika mashindano yanaoendelea ya UHAI CUP kwa timu za vijana za ligi kuu Tanzania bara mchezo ulipingwa kwenye uwanja wa KARUME hii leo.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwenye dimba hilo hilo la KARUME kwa mechi mbili kuchezwa, MTIBWA SUKARI watateremka dimbani dhidi ya MAJIMAJI nyakati za asubuhi,huku jioni KAGERA SUKARI wakiikabili JKT RUVU.

====

ZAITUNI HUNT atwaa taji la Urembo Australia
MTANAZANIA anayeishi nchini AUSTRALIA, ZAITUNI HUNT, amenyakua taji la urembo wa AFRIKA baada ya kuwashinda warembo wengine ISHIRINI katika shindano la urembo la MISS AFRICA AUSTRALIA QUEENSLAND 2010.
Katika shindano hilo lililofanyika katika jiji la BRISBANE ZAITUNI ambaye amezaliwa ZANZIBAR na kuhamia AUSTRALIA pamoja na mama yake AMINA BIRAL alitangazwa kunyakuwa taji hilo huku akiwa aamini ushindi wake
Nchi nyingine zilizotowa wawakilishi katika shindano hilo ni KENYA, SUDAN, ETHIOPIA, NIGERIA ZIMBAMBWE na ERITREA.

==
ARSENAL yaichabanga CHELSEA
USIKU wa kuamkia leo kumefanyika mchezo mmoja wa ligi kuu soka nchini UINGEREZA, EPL kati ya wenyeji ARSENAL dhidi ya bingwa mtetezi CHELSEA mchezo uliochezwa katika uwanja wa EMIRATES.
ARSENAL waliingia dimbani katika mechi hiyo wakiwa wanyonge kwa CHELSEA katika mechi TANO zilizopita ambazo zote walikuwa wamefungwa huku DIDIER DROGBA akiwa mwiba mkali kwao.
Jana mtazamaji ilikuwa ni mechi ya 148 kwa timu hizi kukutana katika ligi huko ENGLAND,wakiwa wametoka sare mechi 44,CHELSEA wakishinda mechi 44 na ARSENAL wakiwa wameshinda mechi 59 na jana ni ya 60 baada ya kuibugiza CHELSEA magoli MATATU kwa MOJA wakitumia dakika TISA tu katika mchezo huo kuifanyizia CHELSEA.
Mambo yalianza katika dakika ya 44, ambapo ALEXANDER SONG aliipachikia timu yake goli la kwanza.
Goli la pili la ARSENAL lilifungwa katika dakika ya 51 kulikutokana na uzembe wa walinzi wa CHELSEA ukaipa ARSENAL goli la pili lililofungwa na CECS FABREGAS baada ya kupenyezewa pasi na THEO WALCOT.
Na dakika mbili baadaye THEO WALCOT akamalizia hesabu za ARSENAL kwa kupachika bao la tatu,kisha BRANISLAV IVANOVIC akaipatia CHESLEA bao la kufuta machozi.
Ushindi huu mnono wa ARSENAL umewarejesha katika nafasi ya pili kimsimamo wakiwa na alama 35 zikiwa ni alama MBILI tu nyuma ya vinara MANCHESTER UNITED, HUKU CHELSEA wakiporomoka hadi nafasi ya NNE.
===
WENGER na ANCELLOTI wazungumza
Mara baada ya mechi yenyewe makocha wa timu zote mbili walikuwa na yao ya kunena huku tabasamu kubwa zaidi likiwa kwa kocha ARSENE WENGER wa ARSENAL.
WENGER anasema nidhamu ya vijana wake katika kucheza kitimu na kujituma ndio kumepelkea ushindi huo na anasema ushindi huo umezidi kuwatia imani kuwa wanaweza kutimiza malengo yao ya ubingwa na lamsingi kwao sasa ni KUtizama mbele tu.

CARLO ANCELLOTI yeye kwanza amewapongeza ARSENAL kwa ushindi huo na anasema hakika hajafurahishwa kabisa na matokeo hayo na japo vijana wake wamejitahidi lkn haikuwa siku nzuri kwao.

CARLO anasema wana wakati mgumu sana katika kutetea ubingwa wao lakn wangali wanapambana.

===
EPL kuendelea usiku leo na kesho
MFULULIZO wa Ligi hiyo unaendelea tena leo kwa michezo kadhaa ambapo moja kati ya mechi ya kutizamwa zaidi ni ya vinara MANCHESTER UNITED wanasafiri kuwafuata BIRMINGHAM CITY.
MAN wao wanajivunia ushindi wao wa juzi dhidi ya SUINDERLAND na watakuwa na nia moja tu ya kuendeleza ushindi katika mechi hiyo.
BIRMINGHAM nao sio wa kubeza,na japo kuwa hawakucheza mechi yao ya jumapili dhidi ya EVERTON kutokana na hali mbaya ya hewa,kocha wao ALEX MCLEISH anasema wamejipanga vyema kwa ajili ya kutoa upinzani kwa MAN U na kupata alama tatu muhimu.
A
Mechi nyingine za leo ni kati ya MAN CITY dhidi ya ASTON VILLA,stoke city na FULHAM,SUNDERKAND na BLACKPOOL,TOTENHAM dhidi ya NEWCASTLE,WESTBROMWICH ALBION na BLACKBURN na WAGONGANYUNDO WA LONDON-WESTHAM UNITED wakiwa dhofli hali wanawaaliaka EVERTON.

Kesho ni CHELSEA na BOLTON, LIVERPOOL na WOLVERHAMPTON WANDERERS na ARSENAL watakuwa wageni wa WIGAN ATHLETIC.

==


Monday, December 20, 2010


picha ya pamoja ya timu ya mpira wa pete ya KILUVYA na wapinzani wao

Timu ya netboli ya KILUVYA VETERAN ikiwa uwanjani

TENESI


Wachezaji chipukizi wa tenesi wakiapata mafunzo katika uwanja wa KIJITONYAMA jijini DSM

Mshindi wa BSS


Mshindi wa BSS MARIAM MOHMED

BSS


Washiriki wa Bongo Stars Search wakipiga picha ya pamoja mbele ya hudi ya shilingi milioni thelathini,fedha hizo zilinyakuliwa na Mariam Mohamed baada ya kushinda shindano hilo kwa kishindo

Waadishi siku walipokutana wao kwa wao


wachezaji wa timu ya waandishi habari wa michezo wa TASWA wakiwa katika picha ya pamoja na wezao wa Afrika ya mashariki na kati baada ya mchezo wao wa kirafiki ulichezwa kwenye viwanja vya GYKHANA jijini Dsm.

Katika mchezo huo TASWA ilishinda kwa mabao manane kwa moja.waandishi hao walikua nchini kuripoti mashindano ya CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP ambapo KILI STARS ubingwa kwa kuwafunga Ivory Coast kwa bao moja kwa bila

MICHEZO LEO

Marefu wafunzu mafunzo FIBA

Washiriki wanane wa kozi ya ukufunzi ya urefa wa mpira wa kikapu iliyokua inafanywa na shirikisho la mchezo huo dunia FIBA leo wanakabidhiwa vyeti vyao baada ya kufunzu mafunzo hayo na kuwa wakufunzi wa kitaifa.

Kwa upande wake mkufunzi wa FIBA aliyeendesha mafunzo hayo FIBA ZULFIKA amesema ana matumaini makubwa na wakufunzi hao na kuwataka watumie taaluma waliyoipata kufundisha waamuzi wengine.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania TBF PHARES MAGESA amesema mafunzo haya yaliyotolewa na FIBA yatasaidia kuongeza idadi ya waamuzi wa mchezo wa kikapu hapa nchini kwasababu wahitimu wa mafunzo haya nao watawafundisha wenzao.

===

MWANAMZIKI WA TWANGA ABUU SEMHANDO AZIKWA TANGA

Aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa bendi ya muziki wa dansi ya TWANGA PEPETA- ABUU SEMHANDO amezikwa jana huko MUHEZA mkoani TANGA ambapo maziko hayo yamehudhuriwa na mamia ya watu.

Marehemu ABUU SEMHANDO amezikwa kijijini kwao KIBANDA wilayani MUHEZA.

Ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzake wa wanamuelezea marehemu ABUU SEMHANDO kuwa alikuwa mchapakazi, mtu wa watu na alikuwa mfano wa kuigwa.

Marehemu SEMHANDO alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi kwa kugonjwa na gari ndogo aina ya MERCEDEZ BENZ wakati akiwa anaendesha pikipiki huko MBEZI-TANGI BOVU jijini DSM.

MAREHEMU -ABUU SEMHANDO amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 68 na ameacha mjane na watoto.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMINA.

= = =

CAF KUTOA TUZO MBALIMBALI LEO

SHIRIKISHO LA soka barani afrika CAF leo linaendesha zoezi la utoaji wa tuzo mbalimbali za wachezaji bora,timu bora na kocha bora wa AFRIKA huko CAIRO,MISRI.

Tuzo hizo zimegawanywa katika vipengele NANE.

Vipengele hivyo ni MWANASOKA BORA WA AFRIKA,MWANASOKA BORA ANAYECHEZA AFRIKA,MCHEZAJI BORA WA KIKE,MCHEZAJI BORA ANYECHIPUKIA,KLABU BORA YA MWAKA,TIMU BORA YA TAIFA YA MWAKA,TIMU BORA YA TAIFA YA WANAWAKE YA MWAKA na KOCHA BORA WA MWAKA.

Mshambuliaji wa timu ya INTER MILAN ya ITALIA na CAMEROON- SAMUEL ETOO anapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji la mwanasoka bora barani AFRIKA ikiwa ni kwa mara ya NNE kwake.

ETOO ametwaa taji hilo mwaka 2003, 2004 na 2005.

Wengine wanaopewa nafasi hiyo ni pamoja na mtetezi wa tuzo hiyo DIDIER DROGBA ambaye ametwaa tuzo hiyo mara MBILI na ASAMOAH GYAN wa GHANA anayewania tuzo hiyo kwa mara ya kwanza.

Pia leo ndio ratiba ya michuano ya vilabu barani AFRIKA itatolewa huko CAIRO.

====

Real Madrid waibuka kidedea la liga

LIGI KUU ya HISPANIA maarufu kama LA LIGA iliendelea jana kwa michezo mitatu kucheza katika viwanja tofauti.

REAL MADRID wakiwa katika dimba lao la SANTIAGO BERNABEU walitoka kifua mbele baada ya kuichapa SEVILLA kwa bao MOJA kwa BILA.

Goli pekee la REAL lilipachikwa wavuni na muargeritina ANGEL DI MARIA

Mchezo mwingine ulishuhudia ALMERIA ikilala baada ya kukubali kipingo cha mabao MATATU kwa MAWILI kutoka kwa GETAFE.

ATLETICO MADRID ikaifunga MALAGA magoli MATATU kwa BILA na OSASUNA ikienda suluhu dhidi ya REAL ZARAGOZA.

Mabigwa watetezi BARCELONA bado wanaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na alama 43 akifuatiwa na REAL yenye alama 41, Villarreal inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 33, Valencia ipo katika nafasi ya nne ikiwa na alama 28.

===

BAYERN MUNICH yatamba BUNDES LIGA

Ligi kuu ya UJERUMANI BUNDES LIGA mabingwa watetezi wa ligi hiyo BAYERN MUNICH waliteremka dimbani dhidi ya VFB STUTTGART katika uwanja wa MERCEDEZ BENZ ARENA.

Katika mchezo huo BAYERN MUNICH wakaibuka kidedea kwa ushindi mnono wa mabao MATANO kwa MATATU dhidi ya VFB STUTTGART

Mabao ya BAYERN yalifungwa na MARIO GOMEZ THOMAS MULLER na FRANK RIBBERY.

Katika muchezo mwingine Bayer Leverkusen ikatoka sare ya kufungana mabao mawili kwa mawili na Freiburg

Lakini pamoja na ushindi huo bado BAYERN wapo katika nafasi ya TANO katika msimamao wa ligi hiyo wakati BORUSSIA DORTMUND inaongoza ikiwa na alama 43 na kufuatiwa na Mainz yenye alama 33.

===

CARLOS TEVEZ kutimuliwa unahodha MANCHESTER CITY.

Kocha wa timu ya MANCHESTER CITY ya ENGLAND ROBERTO MANCINI huenda akamyang’anya unahodha wa timu hiyo CARLOS TEVEZ.

KWA mujibu wa habari zilizonukuliwa katika tovuti ya shirika la utangazaji nchini UINGEREZA-BBC,MANCINI na TEVEZ walikutana kwa mazungumzo siku ya ijumaa katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo ili kujadili juu ya ombi la TEVEZ la kutaka kuihama timu hiyo.

MAN CITY wanavaana na EVERTON leo katika mechi ya ligi kuu ya ENGLAND na MANCINI anajiandaa kumnyang’anya kitambaa cha unahodha TEVEZ na kumkabidhi nahodha msaidizi KOLO TOURE au VINCENT KOMPANY.

Mancini bado hajauarifu uongozi wa klabu hiyo juu ya maamuzi yake hayo ingawa tayari habari hizo zimeufikia uongozi japo si rasmi.

KOLO TOURE alikuwa nahodha wa MAN CITY wakati ikiwa na kocha MARK HUGHES lakini akanyang’anywa nafasi hiyo na kupewa TEVEZ kwa nia ya kumshawishi nyota huyo kubakia katika timu hiyo.

===

ERNIE ANYAKUA UBINGWA WA gofu

Katika GOFU Ernie Els amenyakua ubingwa wa wazi wa GOFU wa AFRIKA KUSINI hiyo jana baada ya kumaliza mzunguko wa nne akiwa mshindi katika uwanja wa DURBAN COUNTRY CLUB.

Ernie Els huu utakua ni ubingwa wake wa tano katika mashindano hayo na alimshinda mpizanai wake wakaribu Retief Goosen.

Ernie Els alimaliza mzunguko wa mwisho kwa 25-under-par alipofanikiwa kupinga mpira vyema katika shimo la nne.

Mchezo huo ulihusisha mashimo 36 na wachezaji walishindana kwa muda wa siku nne.

Tuesday, December 14, 2010

MICHEZO YA LEO


TFF yamteua JAMHURI KIWELO kufundiasha SERENGETI BOYS
Shirikisho la soka nchini TFF limemteua kocha wa zamani wa SIMBA,JAMHURI KIWELO maarufu JULIO kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, SERENGETI BOYS kinacho jiandaa kushiriki michuano ya CECAFA yatakayoshirikisha nchi za TANZANIA, KENYA na wenyeji RWANDA yatakayoanza kutimua vumbi DECEMBA 17 jijini KINGALI.
Akizungumza jijini DSM kaimu katibu mkuu wa TFF SUNDAY KAYUNI amesema SERENGETI BOYS itacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya wenyeji RWANDA Desemba 17 kabla ya kumaliza na KENYA DESEMBA 22.
KAYUNI pia amewaalika wenyeviti na makatibu wa vilibu vya ligi kuu kufanya mkutano siku ya jumamosi kwa ajili ya maadalizi ya michuano ya UHAI CUP ambayo yanashirikisha timu za vijana chini ya umri wa miaka 20 ya vilabu vya ligi kuu Tanzania bara ili kupanga tarehe ya kuanza kwa michuano hiyo.
Wakati huo huo KAYUNI amevitangaza vilabu TISA vitakavyoshiriki fainali ya ligi daraja la kwanza ambayo fainali zake zitanza kutimua vumbi January 15 mwakani.
Vilabu hiyo kutoka kundi A ni TEMEKE UNITED,VILLA SQUAD, na MORO UNITED,kutoka kundi B ni TANZANIA PRISONS,COASTAL UNION na MORAN FC wakati kutoka kundi C ni JKT OLJORO FC,POLISI MORO,RHINO RANGERS.
==
WANAHABARI WATOA MAONI JUU YA WAJIRIWA TFF
Baada ya kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa TFF ANGETILE ASEAH pamoja na msemaji BONIFACE WAMBURA baadhi ya waandihsi wa habari wamewataka viongozi hao kutenda kazi yao kwa umakini ili kuwapa imani wapenzi wa soka hapa nchini.
Wakizungumza Jijini DSM ALEX LUAMBANO, ZENA CHANDE pamoja na msemaji wa SIMBA CLIFORD NDIMBO wamesema wanaimani na OSEAH pamoja na WAMBURA kwa kuwa walikuwa wafanyakazi waadilifu katika ofisi zao.
OSEAH ameshika nafasi ya ukatibu mkuu baada ya aliyekuwakuu wa TFF FREDRICK MWAKALEBELA kumaliza muda wake huku WAMBURA akishika nafasi ya KAIJAGE ambaye alikuwa msemaji .
Lakini baada ya kuchaguliwa OSEAH amesema anakabiliwa na changamoto nyingi ambazo imejipanga kukabiliana nazo ili kuhakikisha kazi yake anaifanya vizuri.
====
simba na Yanga waunganisha nguvu mashindano ya kimataifa
Vilabu vikongwe vya soka hapa nchini SIMBA na YANGA vimeamua kuunganisha nguvu zao katika michuano ya kimataifa ili kuhakikisha vilabu hivyo vinafanya vyema katika mashindano ya kimataifa.
Wakizunguza kwa pamoja maafisa habari wa vilabu hivyo CLIFFORD MARIO NDIMBO kwa upande wa SIMBA ,na LUIS SENDEU wa YANGA wamesema wameamua kuunganisha nguvu zao kwa vile wanakabiliwa na michuano ya vilabu bingwa barani Afrika na kombe la shirikisho.
NDIMBO na SENDEU wamesema hivi sasa vilabu hivyo vimeweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha mashabiki wao wanaipa nguvu timu ya taifa ama timu yoyote inayoliwakilisha taifa uwanjani bila ya kujali itikadi za mashabiki hao ,hata kama mojawapo ya timu hiyo itakuwa SIMBA ama YANGA.
SIMBA italiwakilisha Taifa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika wakati YANGA ikiiiwalisha TANZANIA katika michuano ya kombe la shirikisho barani AFRIKA michuano hiyo itanza kutimua vumbi mwezi MARCH mwakani.
===
Waziri wanchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa -TAMISEMI-Kapteni GORGE MKUCHIKA amezindua rasmi mashindano ya michezo ya shule za msingi UMITASHUMTA na kuwaagiza wakurugenzi wa halamsahauri za wilaya kote nchini kutenga bajeti itakayoziwezesha shule zote za msingi kushiriki mashindano hayo hapo mwakani.
Uzinduzi wa mashindano ya michezo kwa umoja wa shule za misingi yanafanyika ikiwa imepita miaka kumi tangu aliyekuwa waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi JOSEPH MUNGAI ayafute mwaka 2000 mkoani MOROGORO Mwandishi wetu Joseph Chewale aliyeko mkoani PWANI amehudhuria uzinduzi huo na hii hapa ni taarifa yake…

Up sound….
Wimbo wa taifa ndio ulioanza kuashiria uzalendo kwa mamia ya wanafunzi wa shule za msingi kutoka mikoa kumi na moja TANZANIA BARA ambao wwamekusanyika katika viwanja vya shirika la elimu KIBAHA kushuhudia uzinduzi wa umoja wa michezo kwa shule za misingi UMITASHUMTA ambapo mara baada ya wimbo huo waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa -TAMISEMA -kapteni GORGE MKUCHIKA anatoa maagizo ya serikali kwa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya juu ya kufufua michezo kwa vijana(PAUSE)
Pamoja na na maagizo hayo waziri MKUCHIKA pia hakusita kuinyoshea kidole wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi huku akiitaka isitoe vibali vya kusajili shule ambazo hazina viwanja vya michezo

Mashindano ya umoja wa shule za msingi UMITASHUMTA yanazinduliwa tena ikiwa imepita miaka kumi kamili tangu yafutwe mjini MOROGORO na aliyekuwa waziri wa elimu na ufundi wakati huo JOSEPH MUNGAI kwa madai kuwa yalikuwa yanawanyima muda wa kusoma wanafunzi.
Mwisho
==
Watano kuchuana fainali BONGO STARS SEARCH
Katika burundani waandaaji wa BONGO STARS SEARCH BENCHMARK PRODUCTION wametangaza wanamziki watano chipukizi wataochuana katika fainali ya shindano hilo ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni thelathini,fainali hiyo inafanyika siku ya ijumaa desemba 17 katika ukumbi wa MLIMANI CITY jijini DSM.
Wakizungumza wakati wa kutangaza majina hayo mkurungezi wa BENCHMARK PRODUCTION RITA POULSEN ambao ndio waandaaji wa shindano hilo na meneja wa bia ya KILIMANJARO GEORGE KAVISHE ambao ni wadhamini wa shindano hilo wamesema lengo la shindano hilo ni kuibua vipaji kwa wanamziki chipukizi na kuvifikisha katika kilele cha mafanikio.(VOX POPS)
Vijana waliongia katika fainali hiyo ni MARIAM MOHAMED, JAMES MARTIN, WAZIRI SALUM, BELLA KOMBA na JOSEPH PAYNE,na hapa wakaonyesha vipaji vyao kwa kuimba, hebu pata uhondo.
Katika fainali hiyo pia kutakua na wanamziki kwa ajili ya kutoa burundani kwa mashambiki watakaohudhuria kushuhudia fainali hiyo ambao ni pamoja na wanamziki wa kizazi kipya DIAMOND,TEMBA na CHEGE,MWASITI,JOHNMAKINI,IMANI,MARLAW,KIBONDE na CINDY kutoka UGANDA.
==
Mazishi ya Mwanamuziki REMMY kufanyika kesho kutwa
Mazishi ya Mwanamuziki mkongwe nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya CONGO DRC, RAMADHAN MTORO ONGALA maarufu Dokta REMMY aliyefariki dunia jana usiku yanatarajiwa kufanyika kesho kutwa siku ya ALHAMIS jijini DSM.

Marehemu Dokta REMY alifariki dunia katika hospitali ya Regency baada ya kuzidiwa ikiwa ni siku mbili tu tangu kuondolewa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alilazwa.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake SINZA KWA REMI ambapo Taarifa zaidi kuhusu mazishi zitatolewa baadaye.
Upsound wimbo wa kifo
= =
Waanza kuponda QATAR kuandaa kombe la dunia
RAIS wa shirikisho la soka duniani FIFA, SEPP BLATTER ameshindwa kuzungumzia suala la mashabiki wa soka wanaume wenye jinsia moja wanaojihusisha na mapenzi kutokuwa na nafasi ya kwenda nchini QATAR wakati wa mashindano ya kombe la dunia 2022.
Kulingana na sheria za QATAR, watu hao hawaruhusiwi kujihusisha na mahusiano pindi watakapokuwepo nchini humo humo.
Mbali na hilo pia choko choko nyingine zimejitokeza kwa kupinga QATAR kuandaa mashindano hayo zikidai kuwa wakati wa mwezi wa mashindano hayo kwa kawaida joto linakuwa na sentigredi AROBAINI hadi HAMSINI na kwa sheria ya sasa ya QATAR inakataza watu kutokunywa pombe hadhari.
Desemba Mbili mwaka huu wajumbe wa FIFA waliichagua QATAR kuandaa mashindano hayo ya dunia ya 2022, kwa kuzishinda nchi za AUSTRALIA, JAPAN, SOUTH KOREA na UNITED STATES.
==
TP MAZEMBE kucheza nusu fainali.
MABINGWA wa AFRIKA, TP MAZEMBE leo wanacheza mchezo wao wa nusu fainali ya mashindano ya FIFA ngazi ya vilabu kutoka mabara tofauti ulimwenguni.
MAZEMBE itacheza na timu ya INTERNATIONAL ya BRAZIL baada ya TP MAZEMBE ya CONGO kuirarua timu ya PACHUCA ya MEXICO.
Wadadisi wa soka tayari wamebainsha kuwa kiwango cha TP Mazembe katika mashindano hayo kimekuwa cha juu kwani timu hiyo imeweka rekoditangu iwekwe mara tatu na timu nyingine za Afrika kwenye mashindano hayo kama AL-AHLY 2006 na ETOILE DU SAHEL ya TUNISIA mwaka 2007.
==
MANCHESTER UNITED yairarua ARSENAL
BAADA ya kipigo cha goli MOJA kwa SIFURI dhidi ya MANCHESTER UNITED, kocha wa timu ya ARSENAL, ARSENE WENGER amekosoa uwanja wa OLD TRAFFORD eneo la kuchezea PITCH kuwa ni moja ya sababu iliyosabaisha wachezaji wake kufanya vibaya katika mchezo huo.
Mchezaji JI-SUNG PARK wa MANCHESTER UNITED ndiye aliyepachika goli pekee katika mchezo huo.
Katika mchezo huo ARSENAL kupitia kwa mchezaji wake MAROUANE CHAMAKH,waliweza kukosa nafasi kadhaa za kupachika magoli .

==
HISIA za makocha katika mashindano ya CECAFA
Ama kwa hakika mashindano ya CECAFA TUSKER CHALENJI yaligubikwa na kashi kashi nyingi hususani za makocha.
Nimefuatilia makocha hawa walivyokuwa wakihamasisha timu zao wakati wa mechi zao
==
OBAMA akutana na LOS ANGELES
RAIS wa MAREKANI, BARACK OBAMA amekutana na kikosi cha timu ya LOS ANGELES inayoshiriki ligi ya mchezo wa kikapu ya NBA ya MAREKANI akiwemo KOBE BRYANT.
Hiyo ilikuwa ni ziara ya pili kwa kikosi cha LOS ANGELES kumtembelea rais OBAMA na safari hii walikutana na wasichana na wavulana wadogo waliopo katika eneo la WASHINGTON DC.
Rais Obama ambaye ni shabiki mkubwa wa timu ya CHICAGO BULLS ameipongeza timu hiyo kwa kutumia muda wake mwingine kusaidia katika huduma za kijamii.
Mbali na Kobe Bryant pia OBAMA alikutana na wachezaji wengine wa sasa na wazamani .
Hii ni moja ya huduma ambayo LOS ANGELS inafanya baada ya kunyakuwa kombe la NBA mwaka huu na inakadiriwa zaidi ya mashabiki MILIONI MOJA na NUSU walikusanyika kuishangilia timu hiyo.
==



Saturday, December 11, 2010

michezo ya leo


Kilimanjaro Stars uso kwa uso na Ivory Coast fainali Cecafa.
Timu ya taifa ya TANZANIA BARA The KILIMANJARO STARS kesho inateremka dimbani kuikabili timu ya taifa ya IVORY COAST maarufu kama tembo katika mchezo wa fainali ya cecafa tusker challenge cup utakaofanyika katika dimba la taifa jijini DSM
Akizungumza na waandishi habari jijini dsm hii leo katibu mkuu CECAFA NICOLUS MSONYE amewataka wantazania kujitokeza kwa wingi kuishingilia STARS ili iibuke na ushindi na kulinyakua kombe ambapo pia amesema washindi wa zawadi mbali mbali waliofanya vyema katika michuano hiyo watazawadiwa huku mratibu wa michuano hiyo SAADI KAWEMBA akiombea dua timu ya IVORY COAST kumaliza matatizo yake ya kisiasa yamalizike na warejeee tena kama wataalikwa .
Kabla ya The KILIMANJARO STARS kuivaa IVORY COAST kutakua na mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu kati ya ETHIOPIA ambao walifungwa na IVORY COAST katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya UGANDA ambao wao walitolewa na STARS katika mchezo wa nusu fainali kwa mikwaju MITANO YA PENATI dhidi ya minne.
= =
Michezo ya shule za msingi kuzinduliwa jumanne ijayo
Michezo kwa shule za msingi hapa nchini inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 14 hadi 21 mwezi huu huko KIBAHA mkoani PWANI ambapo rais wa jamuhuri ya muuungano wa TANZANIA,JAKAYA MRISHO KIKWETE atakuwa mgeni rasmi.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wan chi ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI anayeshughulikia ELIMU KASSIM MAJALIWA amesema kuwa michezo inapoanaznia katika shule za msingi ni rahisi kupata wachezaji wenye vipaji kutokana na kufundishwa kuanzia wakiwa na umri mdogo.
MAJALIWA amesema kuwa mikoa kumi kwa kuanzia itashiriki katika michezo hiyo ambayo inatarajiwa kuleta hamasa katika hule mbali mbali za msingi kurejesha hali ya michezo ambayo ilitoweka tangu mwaka 2000.
Amesema michezo itakayochezwa ni pamonja na soka, mpira wa pete, mbio ambazo zitakuwa kuanzia za mita mia moja hadi elfu moja na mia tano.
= =
TARRICK kuwakilisha nchi majahazi MALAYSIA
Kijana TARRICK NIELSEN atakwenda nchini MALYSIA kuwakilisha TANZANIA katika michuano ya majahazi ya dunia itakayofanyika kuanzia terehe 28 mwezi dec hadi januari 12 mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mazoezi yake ya msiho mchezji huyo amesema kuwa amefanya maaandalizi kabbambe ambapoa anaamini antaweza kufanya vyema.
Mchezaji huyo ambaye ana miaka 13 ameanza kujifunza mchezo huo akiwa na miaka saba ambapo ametumia muda wa mwaka mmoja kuajiandaa kwenda ksuhiriki katika amshindano hayo.
= =
SOLOMON aendelea vyema
Msanii wa nyimbo za injili wa nchini ZAIRE anayeishi nchini KENYA SOLOMONI MKUBWA amepata nafuu na amerushusiwa hospitali baada ya kulazwa kutokana na kupata ajali ya gari akiwa anaelekea mpakani mwa TANZANIA na KENYA SIRALI.
Mratibu wa msanii huyo hapa nchini , ALEX MSAMA amesema kuwa msaniii huyo amepata nafuuu na karibuni ataendeelea na huduma yake ya kutoa neon la mungu kupitia nyimbo za injili.
Katika hatua nyingine,MSAMA amesema kuwa kampuni yake kwa sasa inajiandaa na tamsha la injili la PASAKA na si CHRISTMAS kama ilivyozoeleka ambapo amewataka wapenzi wa muziki wa injili kuwa wavumilivu.

Monday, December 6, 2010

Michezo leo

TASWA FC dimbani dhidi ya waandishi wa michezo wa Afrika Mashsriki.

Timu ya waandishi wa habari za michezo ya Tanzania,TASWA FC na ile ya waandishi wa habari wa za michezo wa kimataifa wanoripoti mashindano ya CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP zinateremka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye uwanja wa GYKHANA jijini DSM jioni ya leo.

Mshidi katika mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kali na ya kusisimua atajinyakulia kitita cha shilingi lake NANE huku mshindi wa pili akiondoka na shilingi laki NNE.

Manahodha wa timu zote mbili MAJUTO OMARI wa TASWA FC na FRED AROCHO wa timu ya waandishi wa habari wa kimataifa wote wametamba timu zao kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Mchezo huo umedhaminiwa na wadhamini wa mashindano ya CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP wakishirikiana na MARADI wa kampeni ya kutokomeza Malaria,MALARIA HAIKUBALIKI.

== ==

Robo fainali ya Cecafa Tusker Challenge Cup kuanza kesho

Michezo ya kwanza ya Robo fainali ya Mashindano ya CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP inaanza kesho kwenye dimba la taifa jijini DSM hiyo kesho.

Katika mchezo wa kwanza utakaochezwa majira ya saa nane mchana IVORY COAST itamenyana na MALAWI wakati mchezo wa pili utazikutanisha ETHIOPIA na ZAMBIA.

Michezo ya Robo fainali ya pili itachezwa siku ya jumatano wakati ZANZIBAR HEROES itakapo teremka dimbani kumenyana na UGANDA huku KILIMANJARO STARS ikiikabili RWANDA.

Katika michezo iliyochezwa jana mabingwa watetezi UGANDA walitoka kifua mbele baada ya kuichapa Kenya kwa mabao MAWILI kwa BILA huku timu alikwa katika michuano hiyo IVORY COAST ikiichapa SUDAN kwa magoli MATATU kwa BILA.

= == = === = =

Sunderland yachanua ligi kuu England

Kimataifa,ligi kuu ya ENLANG imeendelea jana kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja viwili tofauti.

SUNDERLAND walitoka kifua mbele kwa ushindi wa BAO MOJA kwa BILA dhidi ya WEST HAM na kupaa hadi katika nafasi ya SABA wakiwa na ALAMA 23 huku wakiwaacha wapinzania wao WEST HAM kuendelea kushika mkia katika ligi hiyo.

Katika mchezo mwingine WEST BROM wakiwa katika dimba lao la nyumbani wamechomoza na ushindi wa mabao matuta kwa MOJA dhidi ya NEWCASTLE na kushika nafasi ya NANE ikiwa na Alama 22.

Msimamo wa ligi hiyo unaonyesha ARSENAL inaongoza ikiwa na Alama 32 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao MAWILI kwa MOJA dhidi ya FULHAM siku ya jumamosi.

MANCHESTER UNITED,wao wanashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na ALAMA 31 licha ya mchezo wao dhidi ya BLACKPOOL kuahirishwa kutokana na theluji.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo CHELSEA wao wanashika nafasi ya tatu baada ya juzi kulazimishwa sare ya kufungana bao moja kwa moja na EVERTON.

Leo kuatakuwa na mchezo mmoja wakati LIVERPOOL watakapo wakaribisha ASTON VILLA katika uwanja wake wa nyumbani wa ARNFIELD.

=====

DORTMUND yajikita kileleni Bundesliga

Huko UJERUMANI vinawa wa ligi ya BUNDESLIGA BORUSSIA DORTMUND wameendelea kujikita kileleni kwa pengo la Alama kumi baada ya hiyo jana kuchomoza na ushindi wa mabao MAWILI kwa BILA dhidi ya NUREMBERG.

Mabao ya DORTMUND yakipachikwa wavuni na Mats HUMMELS na ROBERT LEWANDOWSKI

Mahasimu wao ambao wanashika nafasi ya pili timu ya MAINZ yenyewe ilijikuta ikipata kichapo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa FRANKFURT na hiyo kuifanya DORTMUND iendelee kutamba kileleni.

Katika mchezo mwingine uliochezwa jana BAYER LEVERKUSEN ilibuka na ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya COLOGNE.

Msimamo wa ligi hiyo unaonyesha BORUSSIA DORTMUND inaongoza ikiwa na ALAMA 40, MAINZ wapo katika nafasi ya pili wakiwa na ALAMA 30 wakati BAYER LEVERKUSEN inashika nafasi ya tatu ikiwa na ALAMA 29

====

Villarreal na Espanyol zatamba LA LIGA

Huko HISPANIA katika ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama LA LIGA VILLARREAL na ESPANYOL zimeibuka kidedea hiyo jana na kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo.

VILLARREAL wameibuka na ushindi wa bao MOJA kwa BILA dhidi ya SEVILLA na kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa katika uwanja wake wa nyumbani.

ESPANYOL wao wakaibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya SPORTING GIJON.

Mabingwa watetezi BARCELONA wao wanaongoza ligi hiyo wakiwa na 37 baada ya siku ya jumamosi kuibuka na ushindi wa mbao matatu kwa bila dhidi ya OSASUNA.

Mahasimu wao katika LA LIGA REAL MADRID bado wanashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na ALAMA 35 baada ya kuichapa VALENCIA kwa mabao mawili kwa bila.

VILLARREAL wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 30 wakati ESPANYOL wapo katika nafasi ya nne wakiwa na 28 huku VALENCIA wakiwa katika nafasi ya tano wakiwa na alama 24.

====

Seriba mabingwa kombe la DAVIS

SERBIA imenyakua ubingwa wa tenisi wa DAVIS CUP baada ya kuifunga UFARANSA katika fainali iliyochezwa jana mjini BELGRADE.

Shujaa wa SERBIA alikua ni VICTOR TROICKI ambaye alimfunga Mfaransa MICHAEL LLODRA wa UFARANSA kwa seti tatu kwa bila ya ushindi wa 6-2 6-2 6-3.

Katika mchezo wa mwanzo mchezaji wa tennis namba tatu duniani NOVAK DJOKOVIC aliweza kuirudisha SERBIA sawa kwa ushindi wa 6-2 6-2 6-4 dhidi ya GAEL MONFILS wa UFARANSA.

SERBIA ilianza mashindano hayo ya DAVIS kwa mara ya kwanza mwaka 1995 na wote DJOKOVIC na OBRADOVIC walisema kabla ya fainali kuwa ushindi wa taji hilo utailetea SERBIA mafanikio makubwa katika historia ya michezo ya nchi hiyo.

= = = == = = = = =

.

Ndoto za mchezaji nambari mbili kwa ubora wa GOFU duniani TIGER WOODS kuibuka na ubingwa wa kwanza zimezimwa na GRAEME McDOWELL hiyo jana baada ya GRAEME McDOWELL kuibuka na ubingwa wa dunia wa CHEVRON kufuatia mchezo mkali wa marudiano.

McDOWELL aliianza siku akiwa shot nne nyuma lakini alifanikiwa kuweka mambo sawa na kwenda sawa na TIGER WOODS katika hatua ya mwisho hatimaye kuweza kuibuka na ushindi.

Pamoja na WOODS kushindwa katika hatua ya mwisho katika mashinmdano hayo lakini dalili zinaonyesha kwamba ameanza kurejea katika kiwango chake cha uchezaji wa GOFU.

Kwa upande mwingine McDOWELL huu nishindi wake wa nne mwaka huu ikiwa ni pamoja na kunyakua mashindano ya wazi ya golf yaMAREKANI na taji la RYDER ambalo ni taji la kukumbukwa zaidi kwa mwaka mzima kwa McDOWELL.

== = = == = =