Wednesday, July 9, 2014

SIMBA IMEANZA MAZOEZI



Katibu mkuu wa shirikisho la ngumi za ridhaa nchini BFT, MAKORE MASHANGA ametoa wito kwa wadau wa michezo kuisadia timu ya taifa ya ngumi  iliyopo kambini  KIBAHA  kujiandaa na mashindano ya JUMUIYA ya MADOLA yanayotarajiwa kuanza JULY 23 jijini GLASSGOW, SCONTLAND.
MASHANGA amesema wadau wengi wa michezo hujitokeza kupongeza timu wakati inaporejea kutoka kwenye michezo kwa kutafuta sifa na kuzisahau timu hizo wakati wa maadalizi yake.
Timu ya taifa ya ngumi  imeweka kambi KIBAHA na inanolewa na makocha HASSAN MZONGE na JONATHAN MWAKIPESILE baada kumaliza kambi ya mazoezi nchini CHINA na UTURUKI.
=====
Mkoa wa kimichezo wa TEMEKE umeandaa mashindano ya ngumi ya kimataifa yatakayoshirikisha  mabondia  kutoka nchi za ZAMBIA, KENYA na UGANDA,mashindano hayo yatafanyika mwezi SEPTEMBA jijini DSM.
Mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa kimichezo wa TEMEKE, SAID OMAR maarufu GOGO POA  na kocha wa ngumi kutoka Kenya , MUSSA BENJAMIN wamesema mashindano hayo yanalenga kuimarisha mchezo huo kwa nchi za Afrika mashariki.
Nao mabondia JOHN DAUDI na ALLEN FLEURY wamejigamba kufanya vyema katika mashindano hayo.
====


KLABU ya simba ya jijini DSM imeanza mazoezi yake leo katika GYM iliyoko TEMEKE jijini DSM.
Ofisa Habari wa SIMBA ,ASHA MUHAJI amsema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika msimu ujao ligi kuu ya VODACOM Tanzania Bara.PAUSE
kocha wa  simba  ZDRAVKO LOGARUSIC inatarajiwa kutua nchini siku ya ijumaa tayari kujiunga na timu hiyo kwa maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
====

No comments:

Post a Comment