Tuesday, January 11, 2011

LIGI KUU RUHUSA KUCHEZWA UWANJA WA TAIFA
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limetangaza uwanja wa taifa jijini DSM kuwa utatumiwa na timu za ligi kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili baada ya kupata baraka kutoka kwa Wizara ya Habari, Utamaduni,Vijana na michezo.
Akizungunza na waadishi habari jijini DSM katibu mkuu wa TFF ANGETILE OSIAH amesema uwanja upo huru kutumiwa na timu za SIMBA, YANGA, AZAM FC, JKT RUVU na RUVU SHOOTING kama uwanja wao wa nyumbani kwa mechi za ligi kuu Tanzania bara mzunguko wa pili.
Vilabu vya SIMBA, YANGA, AZAM FC, JKT RUVU na RUVU SHOOTING vilikua vikitumia uwanja wa UHURU kama uwanja wao nyumbani kabla ya kufungwa kwa mategenezo na vikalazimika kutumia viwanja vya CCM KIRUMBA, JAMHURI MOROGORO na MKWAKWANI TANGA.
Wakati huo huo OSIAH amesema ni marufuku kuchezwa michezo ya kirafiki ya kimataifa kuanzia siku ya jumamosi ambapo mzunguko wa pili wa ligi kuu utakua umeanza ili kulinda kalenda ya TFF ambayo vilabu vyote na wadau mbalimbali wa soka wanayo nakala yake.

==
UPENDO kumvaa mganda kutetea ubingwa wake
Bingwa wa KICK BOXING wa AFRIKA ya Mashariki na kati UPENDO JAU amekabidhiwa vifaa vya mazoezi na mbuge wa KINONDONI IDD AZAN tayari kujindaa na pambano lake la kuetetea mkanda wake dhidi ya Mganda mwezi march na pia michezo ya kimataifa huko JAPAN.
Akikabidhi msaada huo Mbunge AZAN amesema ameamua kutoa vifaa hivyo ili kuhakikisha Upendo anafanya vyema katika michezo yake ya kimataifa.
kwa upande wao UPENDO NJAU na JAPHET KASEBA wameshukuru AZAN kwa kutoa vifaa hivyo ambayo vitakua ni kichochezo kwa wanawake wengine kujiunga na mchezo huo nchini.
UPENDO katika kujiandaa na pambano lake la kuetea ubingwa wa Afrika ya MASHARIKI dhidi ya Mganda na safari yake ya kwenda kupigana JAPAN atapiga kambi ya mazoezi jijini NAIROBI.

==

KOCHA wa timu za taifa za riadha na ngumi kutoka CUBA wameiomba serikali ikutane na vyama vya olympiki yani TOC , ngumi za ridhaa na shirikisho la mchezo wa riadha nchini kwa kuwa kuna uhaba wa vifaa kwa wachezaji wake.
Kocha ANDREW BARO ametoa rai hiyo ikiwa ni kauli yake ya kwanza tangu miezi mitatu ya mashindano ya jumuiya ya madola kumalizika nchini INDIA na TANZANIA kutoambulia hata medali katika mashindano hayo.
Katika mashindano ya MADOLA ya mwaka jana, TANZANIA iliwakilishwa na wanamichezo wa KUOGELEA, TENNIS, NGUMI ZA RIDHAA na riadha.

==
NYOTA wa BRAZIL, RONALDINHO hatimaye amejiunga na klabu iliopo katika mji wa RIO DE JANEIRO nchini BRAZIL ya FLAMENGO na kupoteza ndoto iliyokuwa ikitajwa awali kwamba mchezaji huyo atajiunga na klabu ya BLACKBURN ROVERS ya UINBGEREZA akitokea AC MILAN.
RONALDINHO, mwenye miaka THELATHINI alijiunga na AC MILAN akitokea BARCELONA mwaka 2008 mbali na kuhitajika na klabu hiyo pia klabu za GREMIO na PALMEIRAS nazo zilikuwa zikimuhitaji.
Rais wa klabu ya FLAMENGO, PATRICIA AMORIM alikaririwa katika mtandao wa klabu ya FLAMENGO kuwa wamemsajili RONALDINHO kuchezea klabu yao kwa kipindi cha miaka MINNE.
Hata hivyo tetesi za RONALDINHO kurudi kucheza soka la nyumbani hazikumtia shaka kocha wa MILAN, MASSIMILIANO ALLEGRI ambaye anasema alijiua uamuzi wa RONALDINHO ni kucheza nyumbani tena.
RONALDINHO, ameondoka katika klabu ya AC MILAN ikiwa ni miezi sita imesalia kumaliza mkataba wake wa kuichezea klabu hiyo ya ITALIA.

==

KOCHA mpya wa LIVERPOOL, KENNY DALGLISH ametoa siri kwamba yeye na familia yake wamekuwa wanaipenda klabu ya LIVERPOOL na hivyo kuambiwa kwake achukue jukumu la kuifundisha timu hiyo lilikuwa si jukumu la kusita.
DALGLISH, amechukua jukumu la kuifundisha timu ya LIVERPOOL baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo ROY HODGSON kutimuliwa kutokana na maendeleo mabaya ya LIVERPOOL katika michezo yake.
DALGLISH,aliwahi kuifundisha LIVERPOOL kati ya mwaka 1977 na 1991 na aliwahi kuomba kuifundisha LIVERPOOL wakati ilipotangazwa kazi ya kuifundisha kocha na kocha RAFAEL BENITEZ akapata kibarua hicho.

==
MFULULIZO wa michezo ya kombe la ASIA unaendelea leo kati ya wapinzani wa jadi katika bara hilo IRAN na IRAQ ukiwa ni mchezo wa kundi D wa mashindano hayo .
Kati ya timu hizo ,moja itakayoshinda katika mchezo wa leo atakuwa amejiweka sehemu nzuri ya kwenda raundi ya pili ya mashindano hayo na atakuwa na pointi nzuri.
IRAN inafanya jitihada za kufanya vizuri katika mashindano ya mwaka huu kwani inataka pia kupata tiketi ya kucheza fainali zijazo za kombe la dunia .
Jana INDIA ilicharazwa na AUSTARLIA kwa magoli MANNE kwa BILA, huku Jamhuri ya KOREA ikiibuka na ushindi wa magoli MAWILI kwa MOJA dhidi ya BAHRAIN.
==

No comments:

Post a Comment