Monday, January 10, 2011

Bondia wa mchezo wa KICKBOXING wa TANZANIA, KANDA KABONGO amefanikiwa kupata taji la mashindano ya mabingwa kwa mabingwa baada ya kushinda katika mchezo wake wa fainali dhidi ya GORORA MOSES wa UGANDA.

Ilikuwa ni burudani tosha kwa mashabiki wa ndonga ama masumbwi pale bondia KANDA KABONGO alipofanya kweli kumdhibiti GORORA MOSES.

Hata hivyo wakati fulani pambano hilo liliingia dosari baada ya mabondia hao kupandwa na jazba ya mchezo na kugeuza mchezo huo kuwa wa mieleka.

Unaweza kuona jinsi mabondia hawa walivyopambana hadi nje ya ulingo na kusababisha kukata kamba ya ulingo.

katika mchezo mwingine bondia HAMIS MWAKINYO alichapwa na GORORA MOSES na kusababisha apasuke maeneo ya pua na hivyo kushindwa kuendelea na mchezo.

Mchezo mwingine wa uzito wa juu wa ngumi uliwakutanisha ALPHONCE MCHUMIA TUMBO na EDDIE DYLE na kushuhudia MCHUMIA TUMBO akimchapa EDDIE kwa K.O kama ambavyo unaweza kuona mchezo huu.

===

Timu ya taifa ya Tanzania, TAIFA STARS kesho inatupa kete yake ya mwisho dhidi ya timu ngumu ya UGANDA katika mechi za mfululizo za kuwania kombe la bonde la mto NILE huko MISRI.

STARS ambayo haijaonyesha kiwango cha kuridhisha katika mashindano hayo wanapashwa kushinda mchezo huo kama wanataka kusonga mbele kucheza katika hatua ya nusu fainali.

Katika mchezo wa kwanza STARS ilikubali kipigo cha magoli MATANO kwa MOJA dhidi ya wenyeji wa mashindano hayo MISRI.

NA katika mchezo wa juzi jumamosi TAIFA STARS ikalazimisha sare ya kufungana bao MOJA kwa moja na Burundi.

==

JKT RUVU na RUVU SHOOTING STARS leo hii zinashuka dimbani katika kuwania ubingwa wa vijana kwa timu za ligi kuu Tanzania Bara mchezo utakaopigwa kwenye dimba la KARUME jijini DSM.

RUVU SHOOTING imetinga hatua ya fainali baada ya kuifunga ARUSHA FC kwa mabao mawili kwa bila katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa siku ya jumamosi.

kwa upande wa dungu zao JKT RUVU wao wametinga katika hatua ya fainali baada ya kuichapa timu ngumu ya POLISI DODFOMA kwa bao moja kwa bila.

kabla ya mchezo wa fainali kutakuwa na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya POLISI DODODMA dhidi ya AFC.

===

Huko visiwani ZAZIMBAR leo kuna patashika nyingine ya kuwania kucheza fainali ya kombe la mapinduzi wakati mabingwa watetezi wa kombe hilo MTIBWA SUGAR itakapo teremka dimbani kuikabili YANGA katika mchezo wa nusu fainali ya pili itakayopigwa kwenye uwanja wa AMAAM usiku wa leo.

Tayari WEKUNDU wa MSIMBAZI SIMBA wo wametinga hatua ya fainali ya michuano hiyo baada ya hiyo jana kuichapa ZANZIBARS OCEAN VIEW kwa magoli MAWILI kwa MOJA.

Magoli ya SIMBA yalipachikwa wavuni na EMANUEL OKWI katika dakika ya tatu ya mchezo,huku bao la pili likifungwa na HILARY ECHESA katika dakika ya 61 ya kipindi cha pili.

Bao la kufutia machozi kwa OCEAN VIEW lilifungwa na na SADI RAMADHANI katika dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza.

Kocha wa SIMBA PATRICK PHIRI anasema huu ni muda wa kusheherekea ushindi wa mechi ya nusu fainali kwa kuwa wamecheza na timu nzuri yenye wachezaji chipukizi na wanaocheza vizuri.

lakini kocha wa ZNZ OCEAN VIEW yeye amekubaliana na matokeo hayo.

= = =

Huko ENGLAND jana imechezwa michezo kazaa ya kuwania kombe la FA mzunguko wa tatu.

Lakini macho na masikio ya mashabiki kote duniani yalielekezwa kwenye mechi kati ya watani wa jadi MAN UNITED dhidi ya LIVERPOOL mchezo ulipigwa kwenye uwanja wa OLD TRAFORD.

Katika mchezo huo mashetani wekundu wa MANCHESTER, MAN UNITED waliibuka kidedea baada ya kuchomoza kwa ushindi wa bao MOJA kwa BILA bao lilofungwa na mkongwe RYAN GIGGS kwa mkwaju wa penalti.

Kocha mpya wa LIVERPOOL KING KENNY DALGLISH anasema mchezo ulikua ni mzuri kwa timu zote mbili lakini MAN UNITED walicheza vizuri zaidi hasa baada ya kutolewa kwa nahodha wake STEVEN GERARD baada ya kumchezea vibaya MICHAEL CARRICK na kulimwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo HAWARD WEBB.

Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa jana MANCHESTER CITY wakiwa ugenini walilazimishwa sare ya kufungana mabao MAWILI kwa MAWILI dhidi ya vijana wa kocha wao wa zamani SVEN GORAN ERICSSON, LEICESTER CITY.

CHELSEA wakiwa na hasira za kufanya vibaya katika michezo ya ligi kuu ya ENGLAND wao wakatoa kichapo cha mabao SABA kwa BILA dhidi ya watoto wa IPSWICH TOWN ambao kwa sasa hawana kocha mkuu baada ya ROY KEANE kutimka hivi karibuni.

Matokeo mengine TOTTENHAM HOTSPURS imeichapa CHALTON ATHLETIC kwa magoli MATATU kwa BILA.

Mzunguko wa nne wa kuwania kombe la FA utafanyika mwishoni mwa mwezi huu na tayari bingwa mtetezi CHELSEA atacheza na EVERTON.

==

CRISTIANO RONALDO ameendelea kung’ara huko HISPANIA na jana ameiwezesha REAL MADRID kuichapa VILLAREAL kwa magoli MANNE kwa MAWILI.

Katika mchezo wa jana VILLAREAL ndio waliokua wa kwanza kuzifumanuia nyavu za REAL MADRID kwa bao safi lilofungwa na CANI dakika ya SABA.

Dakika mbili baadae CRISTIANO RONALDO akasawazisha.

Dakika ya 18 MARCO REUBEN akaifungia VILLAREAL goli la pili.

Kukuru-kakara za REAL MADRID zikaendelea na RONALDO akafunga goli la pili kusawazisha dakika ya 45.

Dakika ya 79 CRISTIANO RONALDO tena akafunga goli la tatu.

Dakika ya 82 RONALDO akamtengenezea RICRADO KAKA na KAKA hakufanya makosa akafunga goli la NNE.

REAL MADRID sasa wana pointi 47, pointi MBILI nyuma ya vinara BARCELONA.

= = =

Namaliza na michuano ya mataifa ya bara ASIA.

SAUDI ARABIA jana wamemtimua kocha wao wa timu ya taifa wakati michuano ya BARA ASIA inaendelea.

Ni baada ya kupoteza mechi dhidi ya SYRIA, wakifungwa kwa magoli 2-1.

Kocha JOSE PESEIRO kutoka URENO kibarua kikaota nyasi akiwa ugenini huko DOHA na nafasi yake ikachukuliwa na NASSER Al JOHAR.

Aliyewaua SAUDIA ARABIA jana ni ABDULRAZAK Al HUSEIN aliyefunga magoli mawili.

Kwenye mechi nyingine JAPAN nao wameponea chup chup mbele ya JORDAN.

Wamelazimishwa sare ya kufungana goli MOJA kwa MOJA.

Tena JAPAN walipata shida kusawazisha, na walifanya hivyo dakika za lala salama.

kocha wa JAPAN ALBERTO ZACCHERONI amekasirishwa na matokeo haya akisema wamecheza chini ya kiwango bila kujua hata JORDAN nao wamecheza vizuri.

===

No comments:

Post a Comment