Tuesday, December 28, 2010

MICHEZO YA LEO


TAIFA STARS USO KWA USO NA UGANDA ALL AFRICA GAMES
Timu ya taifa ya Tanzania, TAIFA STARS imepangwa kucheza na UGANDA mwezi APRIL mwakani, katika mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki mashindano ya ALL AFRICA GAMES yatakayofanyika MAPUTO MSUMBIJI mwezi SEPTEMBA 2011.

Kaimu katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF SUNDAY KAYUNI amesema jijini DSM hii leo kwamba
TAIFA STARS imepangwa katika hatua ya mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo na shirikisho la soka barani Afrika CAF kutokana na kiwango chake kuwa cha kuridhisha.

KAYUNI amesema michezo ya awali ya michuano hiyo itaanza kutimua vumbi mwezi JANUARI mwakani. TANZANIA ipo katika kanda ya TANO ikiwa na timu za Eritrea, Kenya, Uganda.

Wakati huo huo KAYUNI amesema Kiungo mshambuliaji wa klabu ya soka ya SIMBA RASHID GUMBO ameitwa kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya Tanzania, TAIFA STARS inayojiandaa na mashindano ya maalumu ya NILE BASIN kuziba pengo la HENRY JOSEPH.

KAYUNI amesema HENRY JOSEPH ameshindwa kujiunga na kambi ya taimu ya taifa kutokana na matatizo ya kifaimilia hiyo kocha msadidizi SYLVESTER MASHI ameamua kumuita GUMBO ili kuziba pengo lake.
STARS inajiandaa na michuano maalumu ya NILE BASIN yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao kwa kuzishirikisha timu za Uganda,SUNDAN na wenyeji MISRI.

===

KOCHA WA YANGA ASISITIZA KUWAHITAJI WACHEZAJI WAKE WALIOKO STARS
Kocha mkuu wa klabu Yanga KOSTADIN PAPIC amesema itakuwa ni vigumu kwake kuiandaa timu yake kwa michuano ya kombe la shirikisho kiukamilifu baada ya wachezaji wake SABA kujiunga na mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS inayojiandaa na mshindano maalum NILE BASIN.
Akizumgumza na TBC baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu yake katika uwanja wa kaunda jijini DSM PAPIC amesema michuano hiyo isiyotabulika na shirikisho la soka dunia FIFA wa la CAF kwa kiasi kikubwa imevurunga mpagilio wa programme zake za mazoezi.
Kwa upande wao wachezaji NSA JOB na FRED MBUNA wameesema wao wanajiandaa vyema kuyakabili mashindano yaliyo mbele yao.
Yanga inaendelea na mazoezi yake kujiandaa na michuano ya ligi kuu Tanzania Bara na Kombe la shirikisho jijini DSM.

===

KENNETH MKAPA AWALAUMU WASHAMBULIAJI WAKE
Kocha wa timu ya YANGA B, KENNETH MKAPA amesema kutoka sare kwa timu yake dhidi ya AFRIKA LYON ni uzembe wa washambuliaji wake ambao hawakuwa makini wakati wa umaliziaji.
Amesema mechi hiyo ilikuwa ya msingi kwao kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi katika mashindano ya UHAI CUP lakini pia amesema wanaendelea kujipanga zaidi ili kushinda mechi zinazofuata.
Katika mchezo huo timu ya YANGA imetoka sare ya bila kufungana na timu ya AFRIKA LYON katika mashindano yanaoendelea ya UHAI CUP kwa timu za vijana za ligi kuu Tanzania bara mchezo ulipingwa kwenye uwanja wa KARUME hii leo.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwenye dimba hilo hilo la KARUME kwa mechi mbili kuchezwa, MTIBWA SUKARI watateremka dimbani dhidi ya MAJIMAJI nyakati za asubuhi,huku jioni KAGERA SUKARI wakiikabili JKT RUVU.

====

ZAITUNI HUNT atwaa taji la Urembo Australia
MTANAZANIA anayeishi nchini AUSTRALIA, ZAITUNI HUNT, amenyakua taji la urembo wa AFRIKA baada ya kuwashinda warembo wengine ISHIRINI katika shindano la urembo la MISS AFRICA AUSTRALIA QUEENSLAND 2010.
Katika shindano hilo lililofanyika katika jiji la BRISBANE ZAITUNI ambaye amezaliwa ZANZIBAR na kuhamia AUSTRALIA pamoja na mama yake AMINA BIRAL alitangazwa kunyakuwa taji hilo huku akiwa aamini ushindi wake
Nchi nyingine zilizotowa wawakilishi katika shindano hilo ni KENYA, SUDAN, ETHIOPIA, NIGERIA ZIMBAMBWE na ERITREA.

==
ARSENAL yaichabanga CHELSEA
USIKU wa kuamkia leo kumefanyika mchezo mmoja wa ligi kuu soka nchini UINGEREZA, EPL kati ya wenyeji ARSENAL dhidi ya bingwa mtetezi CHELSEA mchezo uliochezwa katika uwanja wa EMIRATES.
ARSENAL waliingia dimbani katika mechi hiyo wakiwa wanyonge kwa CHELSEA katika mechi TANO zilizopita ambazo zote walikuwa wamefungwa huku DIDIER DROGBA akiwa mwiba mkali kwao.
Jana mtazamaji ilikuwa ni mechi ya 148 kwa timu hizi kukutana katika ligi huko ENGLAND,wakiwa wametoka sare mechi 44,CHELSEA wakishinda mechi 44 na ARSENAL wakiwa wameshinda mechi 59 na jana ni ya 60 baada ya kuibugiza CHELSEA magoli MATATU kwa MOJA wakitumia dakika TISA tu katika mchezo huo kuifanyizia CHELSEA.
Mambo yalianza katika dakika ya 44, ambapo ALEXANDER SONG aliipachikia timu yake goli la kwanza.
Goli la pili la ARSENAL lilifungwa katika dakika ya 51 kulikutokana na uzembe wa walinzi wa CHELSEA ukaipa ARSENAL goli la pili lililofungwa na CECS FABREGAS baada ya kupenyezewa pasi na THEO WALCOT.
Na dakika mbili baadaye THEO WALCOT akamalizia hesabu za ARSENAL kwa kupachika bao la tatu,kisha BRANISLAV IVANOVIC akaipatia CHESLEA bao la kufuta machozi.
Ushindi huu mnono wa ARSENAL umewarejesha katika nafasi ya pili kimsimamo wakiwa na alama 35 zikiwa ni alama MBILI tu nyuma ya vinara MANCHESTER UNITED, HUKU CHELSEA wakiporomoka hadi nafasi ya NNE.
===
WENGER na ANCELLOTI wazungumza
Mara baada ya mechi yenyewe makocha wa timu zote mbili walikuwa na yao ya kunena huku tabasamu kubwa zaidi likiwa kwa kocha ARSENE WENGER wa ARSENAL.
WENGER anasema nidhamu ya vijana wake katika kucheza kitimu na kujituma ndio kumepelkea ushindi huo na anasema ushindi huo umezidi kuwatia imani kuwa wanaweza kutimiza malengo yao ya ubingwa na lamsingi kwao sasa ni KUtizama mbele tu.

CARLO ANCELLOTI yeye kwanza amewapongeza ARSENAL kwa ushindi huo na anasema hakika hajafurahishwa kabisa na matokeo hayo na japo vijana wake wamejitahidi lkn haikuwa siku nzuri kwao.

CARLO anasema wana wakati mgumu sana katika kutetea ubingwa wao lakn wangali wanapambana.

===
EPL kuendelea usiku leo na kesho
MFULULIZO wa Ligi hiyo unaendelea tena leo kwa michezo kadhaa ambapo moja kati ya mechi ya kutizamwa zaidi ni ya vinara MANCHESTER UNITED wanasafiri kuwafuata BIRMINGHAM CITY.
MAN wao wanajivunia ushindi wao wa juzi dhidi ya SUINDERLAND na watakuwa na nia moja tu ya kuendeleza ushindi katika mechi hiyo.
BIRMINGHAM nao sio wa kubeza,na japo kuwa hawakucheza mechi yao ya jumapili dhidi ya EVERTON kutokana na hali mbaya ya hewa,kocha wao ALEX MCLEISH anasema wamejipanga vyema kwa ajili ya kutoa upinzani kwa MAN U na kupata alama tatu muhimu.
A
Mechi nyingine za leo ni kati ya MAN CITY dhidi ya ASTON VILLA,stoke city na FULHAM,SUNDERKAND na BLACKPOOL,TOTENHAM dhidi ya NEWCASTLE,WESTBROMWICH ALBION na BLACKBURN na WAGONGANYUNDO WA LONDON-WESTHAM UNITED wakiwa dhofli hali wanawaaliaka EVERTON.

Kesho ni CHELSEA na BOLTON, LIVERPOOL na WOLVERHAMPTON WANDERERS na ARSENAL watakuwa wageni wa WIGAN ATHLETIC.

==


No comments:

Post a Comment