Tuesday, March 22, 2011

MICHEZO LEO

Kufutia kutokea kwa ajali iliyohusisha wasanii wa muziki wa taarabu wa kundi la FIVE STARS Mwanamichezo wetu JANE JOHN ametembelea ofisi za kundi hilo pamoja na nyumbani kwa mmoja wa wasanii ambaye amefariki dunia katika ajali hiyo ISSA HASSAN aliyekuwa akifahamika kwa jina maarufu la ISSA KIJOTI na baadae kupata fursa ya kuongea na baadhi ya wasanii na wapenzi wa muziki wa Taarabu.

Safari yangu ilianzia Katika ofisi ya kundi la FIVE STARS, katika ukumbi wa IKWETA GRIR ambapo nakutana na ndugu jamaa na marafiki waliofika katika ofisi hizo kwa lengo la kujua nini kinachoendelea baada ya kutokea kwa ajali hiyo.

Katika eneo hili nakuta huzuni ilitawala kwa wasanii waliokuwa kundi hilo ambao hawakusafirI na kundi hilo kutoka na kuumwa na wengine kuhama katika bendi.

Mwimbaji MARIAM HAMIS ambaye hivi karibuni alihama katika kundi hilo pamoja na mwimbaji HADIJA KOPA na mwimbaji JOHA KASSIM ambaye kutoka na kuumwa hakusafiri na kundi holi wanaelezea jinsi walivyopeka msimba huo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kundi la FIVE STARS FEROUZ JUMA alikuwa na haya ya kusema.

Baada ya hapo nikafika nyumbani kwao msanii ISSA HASSAN TEMEKE hali ya huzini ikitawala na hapa mama yake mzazi AMIN MAHAMOD anasema yote ni mipango ya mungu.

Nikipande kidogo alichoimba msanii ISS HASSAN


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi kutokana na vifo vya wasanii 13 wa Kundi la Muziki wa Taarab la Five Star Modern Taarab.

Rais Kikwete amesema anamwomba Mwenyezi Mungu azilaze mahali pema peponi roho za Marehemu wote huku akiwaomba waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo mbaya kuwa na moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Wasanii hao waliokuwa kwenye gari la kukodi wakitokea Kyela, Mbeya, walipata ajali eneo la Doma, karibu na Mbuga ya Wanyama ya Mikumi, Mkoani Mororogoro usiku wa kuamkia leo tarehe 22 Machi, 2011 wakati gari hilo lilipogongana na gari lingine. Wasanii hao walikuwa wakirejea Dar es Salaam kutoka Mbeya ambako walikuwa wamefanya maonyesho.
==
SERIKALI KUTAFUTA MWEDESHAJI UWANJA WA TAIFA

Serikali imesema itafuta uwezekano wa kumtafuta wakala wa ndani ya nchi kuendesha uwanja wa taifa baada ya kushindwa kumpata mwendeshaji wa uwanja huo katika mchakato uliofanyika mwaka jana.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, EMMANUEL NCHIMBI ameyasema hayo katika Mkutano wake na Jukwaa la wahariri jijini DSM ambapo amesema nia ya serikali ni kuufanya uwanja huo uwe wa kisasa zaidi.

Pia NCHIMBI amesema serikali inatafuta uwezekano wa kupunguza makato ya viingilio ili kuviwezesha vilabu shindani kunufaika zaidi na viingilio hivyo.

Hata hivyo, akaonyeshwa kukerwa na tabia za baadhi ya watu wanaoharibu kwa makusudi baadhi ya samani ndani ya uwanja huo na kusema hiyo siyo tabia ya kizalendo.

====

Makamu M/Kiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya Jamii JUMA NKAMIA amelitaka shirikisho la soka nchini TFF kuhakikisha pesa zinazotolewa na FIFA zinatumika kama ilivyokusudiwa kuleta maendeleo ya soka hapa nchini.

NKAMIA amesema kwamba kwa sasa utaratibu unaotumika kuratibu matumizi ya fedha hizo haouko wazi jambo ambalo amedai linatoa mwanya wa matumizi ya pesa hizo kwa mkoa wa DSM pekee huku mikoa mingine ikiachwa bila kunufaika na pesa hizo. (PAUSE) JUMA NKAMIA - Makamu M/Kiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya Jamii.

Katika hatua nyingine NKAMIA ameitaka TFF kufikiria uamuzi wake wa kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni katika ligi kuu kutoka wachezaji watano hadi watatu, hatua ambayo amesema inaweza kuathiri maendeleo ya soka hapa nchini kutokana na mchango wa wachezaji hao katika ukuaji wa soka la Tanzania.

===
MANYARA STARS kuondoka Alhamisi tayari kuikabili CAMEROON
Timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23 MANYARA STARS kuondoka keshokutwa siku ya Alhmisi tayari kuikabili CAMEROON katika mchezo wa awali kuwani kucheza fainali ya OLYMPIKI itayofayika LONDON mwakani.
Akizunguza jijini DSM hii leo Afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF BONIFACE WAMBURA amesema msafara wa timu hiyo utakuwa na wachezeja 18 na viongozi watano.
Wakati huo huo WAMBURA amesema wachezaji wa timu ya taifa ya AFRIKA ya KATI wamewasili kwa mafungu usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo wao dhidi ya TAIFA STARS mchezo uliopangwa kuchezwa jumamosi wiki hii na kuongeza kwamba idadi ya wachezaji wengine wanategemewa kuwasili mchana huu.
Jioni ya leo timu ya AFRIKA ya KATI inategemewa kufanya mazoezi yake katika uwanja wa KARUME wakati TAIFA STARS yenyewe itakuwa katika uwanja wa TAIFA jijini DSM.
===
TP MAZEMBE YACHONGEWA JENEZA DSM
Mashabiki wa soka wa SIMBA katika eneo la bandari jijini DSM wamechonga jeneza na kuliandika jina la TP MAZEMBE wakiashiria kuzikwa kwa timu hiyo itapocheza na mabingwa wa soka nchini SIMBA katika mchezo wa marundiano wa ligi ya mabingwa Afrika utakaoipigwa wiki mbili zijazo kwenye uwanja wa taifa jijini DSM.
Wakizungumza na TBC kwa niamba ya mashabiki wezao MOSSES AMBROSS na SAID MBEGA wamesema wametegeneza jeneza hili wakiashiria kwamba SIMBA itaibuka kidedea dhidi ya TP MAZEMBE katika mchezo wa marundiano.
Katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa Afrika uliopigwa jumapili iliyopita katika uwanja wa KENYA mjini lumbumbashi SIMBA ililala kwa kufungwa mabao matatu kwa moja hiyo inatakiwa kushinda kwa mabao mawili kwa bila ili ishonge mbele.
==
RAGA YAANZA KUFUNDISHWA SHULE ZA MSINGA DSM.
Vijana 12 wa shule ya msingi Mapambanano jijini DSM wameanza mafunzo ya mchezo wa RAGA yanayotolewa na mkufunzi kutoka UINGEREZA RICHARD BENETT.
Akizungumza na TBC BENETT kutoka katika taasisi ya kimichezo ya BHUBESI PRIDE amesema wameamua kuazisha mchezo huo katika shule za msingi za Tanzania kwa lego la kukuza mchezo huo hapa nchini.

Naye mkuu wa shule ya msingi Mapambano IDDA UISSO amesema mafunzo hayo yamekuja wakati mwafaka na yatasaidia kukuza vipaji kwa wachezaji chipukizi wa RAGA kwa faida ya timu ya taifa kwa siku za usoni.
Tanzania ni miongoni mwa nchi nyingine kumi za Afrika ambazo zitafaidika a mafunzo ya mchezo wa RAGA kutikakatika taasisi hiyo ya BHUBESI PRIDE ya UINGEREZA.
==
WASANII KUTUMBUIZA KATIKA Tuzo za Kili Music
Wasanii wa kizazi kipya na wale wa taarabu kutumbuiza wakati wa onyesho la Tuzo za Muziki za Kili ambazo zitafanyika katika ukumbi wa wa Diamond Jubilee Jumamosi ya MACHI 26.
Akizungumza wakati wa kutambulisha tuzo hizo jijini DSM hii leo Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, David Minja amesema utoaji wa Tuzo za mwaka huu utapambwa na burudani tofauti kutoka kwa wasanii mbalimbali ili lionekane la kisasa zaidi mwaka huu tofauti na miaka mingine.
Minja akawataja wasanii watakaotumbuiza katika utoaji wa Tuzo hizo ni Ali Kiba, THT, Banana Zoro, Linah, Diamond, Joe Makini, C Pwaa, 20%, Mzee Yusuf pamoja na Mapacha Watatu na Stara Thomas.
Baadhi ya tuzo zinazoshindaniwa kwa mwaka 2010/ 2011 ni Msanii wa kike bora wa Muziki, Msanii wa Kiume Bora wa Muziki, Mwibaji bora wa Kike, Mwimbaji Bora wa Kiume, Wimbo Bora wa Taarab, Wimbo bora wa Mwaka.
===
BLACK STARS imewasili jana nchini Kenya kuweka kambi
Nayo timu ya GHANA, BLACK STARS imewasili nchini KENYA jana kuweka kambi ya siku NNE kabla ya kuelekea CONGO BRAZZAVILLE ambapo timu hiyo ya GHANA itakuwa mgeni katika mechi hiyo.
Hii ni mara ya NNE kwa BLACK STARS kuweka kambi huko NAIVASHA nchini KENYA, ambapo timu hiyo kabla ya kwenda nchini AFRIKA KUSINI kushiriki mashindano ya kombe la dunia iliweka kambi nchini KENYA.
Hata wakati wa mashindano ya wachezaji wanaocheza mashindano ya ndani yaani CHAN, timu ya GHANA iliweka kambi yake nchini KENYA na baadae kwenda kushiriki mashindano ya CHAN yaliyofanyika nchini SUDAN.
==
MOHAMED BIN HAMMAM aendelea kumpinga BLATTER
MGOMBEA wa kiti cha urais katika shirikisho la soka duniani FIFA, MOHAMED BIN HAMMAM ambaye anapinga sera za rais wa sasa wa shirikisho hilo , SEPPY BLATTER , amesema akichaguliwa ataweka mipango ya uwazi wakati wa kuchagua nchi itakayoandaa mashindano ya kombe la dunia.
Bin Hammam , amesema FIFA haitaki rushwa ila shirikisho hilo linahitaji kuwa na uwazi katika kiwango kikubwa katika kuamua mambo yake.
Rais wa sasa wa FIFA , SEPPY BLATTER alikuwa katika wakati mgumu baada ya wajumbe wa kamati ya utendaji wa shirikisho hilo mwaka jana kuchagua URUSI na QATAR kuandaa mashindano ya dunia ya mwaka 2018 na 2022.
Wakati ambapo kazi hiyo ikifanyika kulikuwa na tuhuma za rushwa kwa wajumbe wawili wa shirikisho hilo kwamba walitumiwa kutaka kuuza kura zao ili nchi fulani ifanikiwe kuandaa mashindano hayo ya dunia.
==
NOVAK afurahia kupata nafasi ya pili ya ubora duniani.
MCHEZAJI wa TENNIS, NOVAK DJOKOVIC ambaye amempiku ROGER FEDERER na kuchukua nafasi ya pili kwa ubora duniani amesema hajawahi kuwa katika kiwango cha juu kama hivi sasa tangu aanze kucheza mchezo huo.
DJOKOVIC, alimfunga RAFAEL NADAL katika fainali za mashindano ya INDIAN WELLS ATP na kunyakuwa ubingwa wa mashindano hayo.
Djokovic mwenye miaka 23, alimpiku ROGER FEDERER baada ya kupata ushindi wa 6-3 3-6 6-2 dhidi ya RAFAEL NADAL.
Nafasi ya NNE ya ubora ulimwenguni inashikiliwa na ROBIN SODERLING kutoka SWEDEN na ya TANO inashikiliwa na ANDY MURRY kutoka UINGEREZA.
==

No comments:

Post a Comment