Tuesday, March 15, 2011

POULSEN ATANGAZA STARS KUIVAA JAMHURI YA KATI

Dihile Kazimoto Warejeshwa Stars kuikabili Jamhuri Ya Kati
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanza nia TAIFA STARS JAN POULSEN amewarejesha kikosini mlinda mlango SHABANI DIHILE na kiungo mshambuliaji MWINYI KAZIMOTO wote wa JKT RUVU katika kikosi cha STARS kinachojiandaa na mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Africa CAN dhidi ya JAMHURUI YA KATI mchezo utakaopigwa MACHI 26 kwenye dimba la taaifa jijini DSM.

Akitangaza kikosi hicho chenye wachezaji 23 POULSEN amesema STARS inahitaji kupata pointi nne katika michezo miwili ijayo kama inataka kufufua matumaini ya kufunzu kucheza fainali za Afrika mwakani hivyo mchezo ujao dhidi ya JAMHURI YA KATI lazima STARS ishinde.

POULSEN amesema anajivunia nyota wake sita wanaosukuma soka la kulipwa ulaya ambao ni Danny Mrwanda na Abdi Kasim wanaocheza DT Long An ya Vietnam,Nizar Khalifan wa Vancouver White Caps ya Canada,ATHUMAN MACHUPA wa Vasolund Fc ya Sweden,Henry Joseph wa Kongsvinger Il ya Norway na Idrissa Rajab wa Sofapaka Kenya wakichanganyika na wale vyota wanaocheza lingi ya nyumbani anauhakika wa Stars kuibuka na ushindi.

STARS inashika nafasi ya tatu katika kundi la D ikiwa na Alama moja baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja na ALGERIA ugenini kabla ya kufungwa na MOROCCO bao moja kwa bila nyumbani,JAMHURI YA KATI ipo kileleni mwa kundi hilo ikiwa na ALAMA NNE.

===
Viingilio Simba na Yanga Kuchangia Gongo la Bonto hadharani.
Viingilio vya kuziona timu za veteran za SIMBA na YANGA zitakazocheza kuchangi wathirika wa mabumu ya Gongo La Mboto vyatagazwa cha juu ni 10,000/- na cha chini 1000/-,mchezo huo utapigwa kwenye dimba la taifa jijini DSM MACHI 19 siku ya jumamosi.

Wakizungumza wakati wa kutangaza viingilio hivyo Afisa habari wa SIMBA CLIFORD NDIMBO na wa YANGA LIUIS SENDEU wamesema mechi hiyo imepewa baraka zote na viongozi wa timu zote mbili na tayari maadalizi ya matanange huo yamekamilika.

Kwa upande wao wachezaji wa timu zote mbili wakiongea kwa niamba ya wezao MADARAKA SELEMAN wa Simba na BAKARI malima wa YANGA wamesema wamejiandaa vyema kutoa burundani ya kutosha kwa mashabiki watakohudhuria kushuhudia mchezo huo.

Viingilio katika mchezo huo vitakuwa kama ifuatavyo,VIP A 10,000/- VIP B,5000/- VIP C 3000/- viti vya bluu na kijani mzunguko ni shilingi 2000 na 1000/-

===

Wasaanii kutumbuiza tamasha la UZALENDO

katika burundani wasanii mbalimbali kutumbuiza katika tamasha lilopewa jina laTAMASHA LA UZALENDO,TANZANIA KWANZA,SOTE NI NDUGU litakalofanyika MACHI 26 katika viwanja vya biafra jijini DSM.

wakizungumza na tbc jijini DSMn hii leo waadaji wa tamasha hilo ERICK SHIGONGO na mwanamziki wa rage INNOCENT GALINOMA wamesema tamasha hilo limeandaliwa ili kuwakumbusha watanzania kupitia mziki juu ya uzalendo wa kuipenda nchi yao na kuthamini amani.

Wasanii watakao konga nyoyo za mashabiki ni Profesa J,Ay,H Baba,H.Mbizo wakati kwa uapande wa bendi zitakuwepo MSONDO NGOMA,DDC MLIMAN PARK,TOT BAND na African Stars.
==

MAN UNITED VS MARSEILLE, BAYERN VS MILAN

USIKU huu ligi ya mabingwa barani ulaya UEFA inaendelea kwa michezo miwili ambapo, MANCHESTER UNITED ikiwa nyumbani leo inaikaribisha timu ya MARSEILLE ya UFARANSA katika mchezo mgumu kwa timu zote kwani katika mchezo wa awali uliochezwa nchini UFARANSA timu hizo zilitoka suluhu.

Kocha wa MARSEILLE, DIDIER DESCHAMPS amesema kikosi chake leo kitaingia uwanjani katika dimba la OLD TRAFFORD ikiwa na lengo la kutafuta ushindi.

DESCHAMPS amesema anakiamini kikosi chake kitapata tiketi ya kwenda hatua nyingine ya mashindano ya UEFA ijapokuwa MAN UNITED haijawahi kufungwa na timu ya UFARANSA katika uwanja wa Old Trafford basi leo timu yake itavunja mwiko huo.

Nayo BAYERN MUNICH ya UJERUMAN itakuwa nyumbani kuikabili INTER MILAN ya ITALIA.

Kesho michezo hiyo itaendelea ambapo CHELSEA itakuwa katika uwanja wake wa nyumbani wa STANFORD BRIDGE kucheza na FC COPENHAGEN na REAL MADRID itacheza na LYON.

==
JOHN TERRY kurejeshewa Unahodha

KOCHA wa timu ya taifa ya UINGEREZA anafikiria kumrejeshea unahodha JOHN TERRY baada ya sasa RIO FERDINAND kuwa majeruhi.

FERDINAND atakosa mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza mashindano ya EURO 2012 dhidi ya WALES mchezo utakaochezwa machi 26 ambapo pia nahodha msaidi wa FERDINAND, STEVEN GERRALD naye hatokuwepo katika mchezo kufuatia kusumbuliwa na HERNIA.

katika hatua nyingine klabu ya ARSENAL ina mpango wa kumsaji golikipa wake wa zamani mwenye miaka 41 sasa JENS LEHMANN.

Hali hii inatokana na timu ya ARSENAL kukabiliwa na magolikipa wake ambao ni majeruhi kama WOJCIECH SZCZESNY, LUKASZ FABIANSKI na VITO MANNONE na hivyo kusalia na kipa mmoja tu MANUEL ALMUNIA.
Wakati akiwa ARSENAL kati ya mwaka 2003 na 2008, LEHMANN aliichezea timu yake michezo MIA TISINI na TISA.
Kama masuala ya kusainishwa kwa golikipa huyo hayatakuwa na utata , LEHMANN anaweza akawemo katika kikosi chqa ARSENAL kitakachocheza mchezo wa jumamosi dhidi ya WEST BROM.
==
NADAL aanza vizuri mashindano ya BNP PARIBAS

RAFAEL NADAL amefanikiwa kuanza vizuri mashindano ya wazi ya TENNIS ya BNP PARIBAS kwa kumfunga RYAN SWEETING kwa seti 6-3, 6-1.
NADAL ameweza kufanya vizuri katika mchezo huo baada ya kuanza vibaya kwenye mashindano hayo yanayofanyika nchini INDIA.
Matokeo mengine upande wa wanawake CAROLINE WOZNIACKI wa DENMARK amefanikiwa kumchapa 6-1, 6-3 mpinzani wake MARIA JOSE MARTINEZ SANCHEZ wa Hispania.
Naye DINARA SAFINA amemfunga SAMANTHA STOSUR kwa seti 7-6, 6-4, ushindi wa SAFINA umekuja baada ya mchezaji huyo kuwa nje ya ya mashindano kutokana na kuwa na maumivu ya mgongo.
==
Tiketi za Olympiki 2012 zaanza kuuzwa
TIKETI zinakazotumika kuingia katika mashindano ya OLYMPIKI ya LONDON mwakani zimeanza kuuzwa siku MIA TANO kabla ya mashindano hayo kuanza.
Zaidi ya tiketi milioni 6.6 zitanunuliwa kwa kipindi cha wiki SITA.
Bei za tiketi hizo ni kuanzia paundi ISHIRINI hadi paundi ELFU MBILI.
==

No comments:

Post a Comment