Wednesday, April 6, 2011

TUANZE na ligi kuu soka VODACOM-TANZANIA BARA ambapo bingwa mtetezi wa SIMBA leo wameweka rehani ubingwa wao baada ya kulazimisha sare ya MBINDE ya goli MOJA kwa MOJA dhidi ya JKT RUVU STARS katika mechi kali iliyochezwa jioni ya leo katika dimba la UHURU jijini DSM.

SIMBA leo hakika walikuwa na wakati mgumu,kipindi cha kwanza tu walikuwa nyuma kwa goli MOJA kwa bila lililofungwa na HUSSEIN BUNU kufuatia walinzi wa SIMBA kujichanganya wenyewe katika harakati za kuokoa na hivyo kumpa nafasi mfungaji kupachika wavuni bao la kuongoza.

Kipindi cha pili SIMBA walijitahidi kuja juu wakisaka goli la kusawazisha kwa nguvu zote bila ya mafanikio hadi katika dakika za lala salama ambapo mlinzi mmoja wa JKT RUVU aliunawa mpira katika eneo la hatari akiwa katika harakati za kuokoa na EMANUEL OKWI kuukwamisha mpira wavuni kwa mkwaju wa penalty na kuisawazishia SIMBA bao.

Mlinda mlango wa JKT RUVU-SHAABAN DIHILE alionyeshwa kadi ya pili ya manjano na hivyo kutolewa nje kwa kumbwatukia mwamuzi PRIMA KABALA huku GEORGE MINJA naye akionyeshwa kadi ya pili ya manjano pia kwa mchezo wa kibabe na hivyo kutolewa nje.

JKT RUVU wamemaliza mechi wakimtumia mlindamlango aliyemchezaji wa ndani KESSY MAPANDE kutokana na kumaliza idadi ya wachezaji wa akiba.

Kwa matokeo haya SIMBA bado wanaongoza ligi wakiwa na alama 46 ikiwa ni tofauti ya alama TATU nyuma dhidi ya mahasimu wao wa jadi YANGA wenye alama 43.

Timu zote hizi zinatofauti ya magoli 20 ya kufunga na kufungwa zikiwa sawa ambapo SIMBA wamefunga magoli 36 na kufungwa 16 huku YANGA wakifunga magoli 26 na kufungwa 6 tu.

YANGA wao wanashuka dimbani kesho kuwakabili AFRICAN LYON katika mchezo muhimu kwao ambapo wakishinda vita kubwa ya kusaka alama TATU muhimu na magoli mengi ili uwiano wa magoli ya kufunga na kufunga uweze kutangaza bingwa utakuwa mkubwa zaidi katika mechi ya mwisho.

SIMBA watamaliza ligi dhidi ya MAJIMAJI huku YANGA wao baada ya mechi ya kesho wakimaliza ligi na TOTO AFRICANS ya MWANZA.

=====

Katika hatua nyingine KLABU ya SIMBA imefikisha malalamiko yake kwa shirikisho la soka barani Afrika CAF dhidi ya klabu ya LE TOUT PUISSANT MAZEMBE ENGLEBERT kufuatia MAZEMBE kumchezesha mchezaji JANVIER BOKUNGU BESALA aliyekuwa akiichezea timu ya ESPERANCE ya TUNISIA na kujiunga na TP MAZEMBE bila ya kibali cha kimataifa cha uhamisho (ITC).

Mwenyekiti wa SIMBA,ISMAIL ADEN RAGE ameithibitishia TBC akiwa mjini DODOMA kuwa wametuma CAF taarifa za malalamiko dhidi ya TP MAZEMBE baada ya kupata nyaraka za mchezaji huyo kutoka katika klabu yake ya zamani ya ESPERANCE iliyosainiwa na katibu mkuu wa klabu hiyo, MOHAMED ABDELATIF ZARROAK.

Haya yanakuwa malalamiko ya pili ya SIMBA kutumwa CAF dhidi ya TP MAZEMBE katika kipindi cha wiki moja ambapo taarifa ya kwanza ni ile ya madai ya maafisa wa TP MAZEMBE kutaka kuwahonga dola elfu 10 kila mwamuzi,waamuzi WANNE wa MISRI waliochezesha mchezo wa kwanza kati ya TP MAZEMBE dhidi ya SIMBA uliofanyika mjini LUBUMBASHI ambapo waamuzi hao kwa mujibu wa taarifa yao iliyowasilishwa CAF walipokataa kuchukua mlungula huo walitishiwa maisha.

Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka barani Afrika CAF inakutana mapema mwezi huu mjini JOHANESBURG,AFRIKA KUSINI kujadili ripoti ya mwamuzi wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani AFRIKA kati ya ZAMALEK ya MISRI dhidi ya CLUB AFRICAN ya TUNISIA uliovunjika kufuatia kundi la mashabiki kuvamia uwanja na kufanya vurugu kubwa.

Haijulikani iwapo kamati hiyo ya nidhamu ya CAF itajadili suala hilo la SIMBA ama la?

Iwapo CAF kupitia kamati zake itafanya maamuzi ya kujadili malalamiko hayo ya SIMBA dhidi ya MAZEMBE huenda kwa mujibu wa kanuni hasa kwa tuhuma za rushwa MAZEMBE wanaweza kupata adhabu ya kufungiwa miaka MITATU kushiriki michuano yoyote ya CAF na SIMBA kupata ushindi wa chee na hivyo kukutana na WYDAD CASABLANCA katika mzunguko unaofuata.

==

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka ISHIRINI na TATU,-MANYARA STARS- JAMHURI KIHWELU JULIO ametamba kikosi chake kuibuka na ushindi dhidi ya CAMEROON katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya OLYMPIKI utakaochezwa jumamosi ya wiki hii katika uwanja wa TAIFA jijini DSM.

Kocha JULIO anasema baada ya kuongeza nguvu ya wachezaji SABA wazoefu katika kikosi chake ana uhakika na imani kubwa ya kuibuka na ushindi(PAUSE)

Wakijiamini wachezaji THOMAS ULIMWENGU, MRISHO NGASSA, na AMOOR SULEIMAN wanasema kulingana na mazoezi wanayofanya wana uhakika wa kufanya vizuri wakati wa mchezo huo dhidi ya CAMEROON.

MANYARA STARS inahitaji ushindi wa goli MOJA kwa BILA ili kuitupa nje CAMEROON kufuatia kufungwa magoli MAWILI kwa MOJA katika mechi ya awali iliyofanyika mjini YOUNDE.

===

Nao wapinzani wa MANYARA STARS-timu ya taifa ya vijana ya CAMEROON ipo jijini huku ikijiwinda kuikabili MANYARA STARS.

Katika kikosi hicho kina wachezaji watono wanao shukuma soka ya kulipwa Ulaya katika nchi za Italia na Ufaransa.

Kikosi hicho pia kina mchezaji mmoja wa timu ya taifa ya wakubwa ya CAMEROON wakati kitamkosa kiungo ALEX SONG anayechezo katika klabu ya ARSENAL kwakuwa anamatatizo na chama cha soka cha CAMEROON CFF.

===

Katika burudani tunatupia jicho muziki wa INJILI kwani kila KILA MWENYE PUNZI NA AMSIFU BWANA,sasa huko WANAMUZIKI wa nyimbo za injili wametakiwa kutunga nyimbo za injili zenye viwango vya kimataifa ili kukabiliana na soko la ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM wakati wa kutambulisha albamu mpya ya SOTE na TUIMBE , mwimbaji wa muziki wa injili nchini MIRIAM MAUKI anasema nyimbo nyingi za injili bado hazifikii kiwango cha kimataifa kwa vile wanamuziki wake wengi hawazingatii viwango vya kimataifa.

Katika hatua nyingine zaidi ya watoto yatima 200 kutoka katika mikoa ya MWANZA, SHINYANGA, SINGIDA watafaidika na fedha zitakazopatikana katika tamasha la muziki wa injili la PASAKA litakalofanyika katika mikoa hiyo mwishoni mwa mwezi huu.

Mratibu wa tamasha hilo ALEX MSAMA amesema hiyo ni michakato ya kufikia mikoa ya TANZANIA pindi tamasha la PASAKA linapokuwa linafanyika ambapo kwa mwaka jana mchakato huo ulianzia katika mikoa ya MWANZA na MUSOMA.

==


Mkoani IRINGA,Wananchi wa kata ya KIYOWELA iliyopo wilaya ya MUFINDI wamesema ukosefu wa vifaa vya michezo katika maeneo ya vijijini umesababisha vijana kutopenda michezo na kushindwa kukuza vipaji vyao.

Pamoja na changamoto hizo vijana hao hawajakata tamaa ya kusakata kabumbu kama walivyokutwa na mwandishi wetu IRENE MWAKALINGA huku baadhi yao wakicheza bila ya viatu (PEKUPEKU) ili mradi kukidhi kiu yao.

= =

INTER MILAN yafungwa magoli matano

KATIKA anga za kimataifa,ligi ya mabingwa barani ulaya timu ya SCHALKE 04 ya UJERUMANI jana imetoa kipigo cha aina yake kwa bingwa mtetezi INTERNATIONAL MILAN cha magoli MATANO kwa MAWILI mechi ikichezwa nyumbani kwa INTER -GUSEPE MEAZA.

DEJAN STANKOVIC alichokoza moto kwa bao la kuongoza kabla ya JOEL MATIP kusawazisha bao hilo na DIEGO MILITO akachokoza tena na ndipo mvua ikawa kubwa kwa INTER MILAN.

EDU akasawazisha bao hilo, mkongwe RAUL GONZALES akapachika la tatu,likiwa ni bao lake la 70 katika ligi ya mabingwa barani ULAYA.

Mlinzi wa INTER,ANDREA RANOCHIA Alijifunga bao la nne na EDU akamaliza bao la TANO.

KATIKA mechi nyingine REAL MADRID wameinyuka TOTTENHAM HOTSPURS magoli MANNE kwa BILA mjini MADRID.

EMANUEL ADEBAYOR alifunga magoli MAWILI,ANGEL DI MARIA na CHRISTIANO RONALDO wakifunga goli MOJA kila mmoja.

Leo ni kivumbi kati ya CHELSEA dhidi ya MANCHESTER UNITED,huku FC BARCELONA wakicheza na SHAKTAR DONETSK.

===

No comments:

Post a Comment