Thursday, February 24, 2011

MICHEZO LEO


Kuelekea pambano la ngumi la uzito wa juu TAMIMU atamba kuchapa ASHIRAFU.

Bondia AWADHI TAMIM ambaye amerejea kutoka nchini SWEDEN amesema anaendelea kujifua vilivyo kwa ajili ya pambano la uzito wa juu kuwania ubingwa wa AFRIKA MASHAIRIKI dhidi ya ASHRAF SULEIMAN litakalofanyika MACHI 11.

Akizungumza na TBC ONE, TAMIM amesema kuwa ana uhakika kuwa atamtwanga mpinzani wake katika hatua za mwanzo .

TAMIM amesema kuwa kwa sasa anajifua chini ya kocha wake SHOMARI KIMBAU ambapo amesema kabla ya kurejea hapa nchini alicheza mechi za kujipika nguvu .

Kwa upande wake mratibu wa pambano hilo ALLY SULUEIMAN,amesema mshindi wa pambano hilo atakwenda nchini MAREKANI kupigana na bondia mwingine ambaye anatafutwa .
= =

Ligi daraja la pili netiboli kumalizika leo.

Mashindano ya netiboli ligi daraja la pili yamefungwa leo hii katika uwanja wa JAMHURI mkoani MOROGORO na tayari timu tatu zimeshapanda daraja.


Baadhi ya viongozi wa timu zinazoshiriki mashindano hayo kocha wa timu ya LINDI ALICE CHIWAJI pamoja na kocha wa BLACK SISTER ya PWANI FARAJA JUMA wamesema mashindano ni mazuri lakini kunamapungufu ambayo yameweza kujitokeza katika mashindano hayo

Timu ambazo zimeshuka ni MINGA MOROGORO, TUPENDANE LINDI na BLACK SISTER ya PWANI.

Mashindano hayo ya ligi daraja la pili yanashirikisha timu kumi na moja kutoka mikoa tofauti ya TANZANIA BARA.

====.
KIFA yashindwa kuandaa mashindano ya soka la wanawake.

Katibu mkuu wa soka wilaya ya KINONDONI FRANK MCHAKI amesema Wilaya ya KINONDONI haitaweza kuandaa mashindano ya soka la wanawake kama ilivyokuwa zamani kutoka na ukukata wa fedha katika chama hicho.

Akizumgumza Jijini DSM FRANK MCHAKI amesema KIFA ilikuwa akiandaa mashindano ya soka la wanawake kwa lengo la kukuza soka hilo na kupata wachezaji watakaounda timu ya TAIFA lakini kwa kipindi hiki haitawezekana.

MCHAKI amesema sasa mashindano ya soka la wanawake yatakuwa yansimamiwa na chama cha soka la wanawake mkoa wa DSM .

Mpaka sasa mashindano ya soka la wanawake ya kutafuta timu ya bingwa ya mkoa .

=====
BAYEN MUNCHEN yaichapa INTER MILAN ulaya.

Ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea jana ambapo kule nchini ITALIA katika uwanja wa SAAN SIRO kulikua na mchezo kati ya wenyeji INTER MILAN dhidi ya BAYEN MUNCHEN ya nchini UJERUMANI.

Katika mchezo huo BAYEN imeibuka kidedea kwa kushinda bao moja kwa bila ikiwa ugenini.

INTER ndio walioanza kulerta kashikashi langoni mwa BAYEN MUNICH kabla ya BAYEN kujibu mapigo haraka kwa krosi iliyopigwa na ARJEN ROBBEN kupigwa kichwa na FRANK RIBERY kilichokwenda kugonga mwamba wa juu.

Kwenye dakika ya 62 ARJEN ROBBEN aliwatoka mabeki wa INTER MILAN na kupiga mpira uliokwenda kugonga mwamba wa pembeni na kutoka nje.

INTER nayo ikafanya mashambulizi ambapo SAMUEL ETOO alipiga shuti lililookolewa na kipa wwa BAYEN lakini ESTEBAN CAMBIASO alishindwa kumalizia mpira huo uliokua umeokolewa na kipa wa BAYEN.

Hata hivyo katika dakika ya 90 MARIO GOMES aliwanyanyua mashabiki wa BAYEN MUNCHEN kwa kufunga goli pekee la mchezo huo akimalizia shuti lililopigwa na ARJEN ROBBEN ambalo liliokolewa na kipa wa INTER CESAR na kushindwa kuudaka vizuri.

= = = = =

MARSEILLE sare na MANCHESTER UNITED.

Nchini UFARANSA MARSEILLE chini ya DIDIER DESCHAMP imeshindwa kuutumia uwanja wake vyema baaada ya kutoka suluhu ya sifuri bin sifuri dhidi ya MANCHESTER UNITED.

Timu zote mbili zilipiga mashuti ndani ya goli MAWILI TU katika dakika zote tisini.
Kocha wa MANCHESTER UNITED SIR ALEX FERGUSON amesema matokeo hayo ni mabaya lakini hakusita kuipigia upatu timu yake kuibuka na ushindi katika mchezo wa marudiano utakaochezwa kwenye uwanja wa OLD TRAFFORD majuma matatu yajayo.

FERGUSON amekubali pia kuwa haukuwa mchezo mzuri wa kuangalia kwa kuwa ulikua hauna masham masham mengi kutokana na kila timu kushindwa kutengeneza nafasi za wazi za kufunga.

FERIGE amesema matokeo kama hayo ni mabaya kama utafungwa goli hata moja nyumbani kwako lakini pia yatakua mazuri kama utashinda kwa kuwa utasonga mbele.

Aidha upande mwingine wa shilingi DIDIER DESCHAMP amewapongeza wachezaji wake kwa juhudi walizozifanya na kusema kuwa wageni hao ambao ni UNITED watakua wamefurahia matokeo hayo.

DESCHAMP amekubali kiwango kilichooneshwa na UNITED na kuongeza kuwa matokeo hayo ya suluhu so mabaya kwao lakini ni mazuri kwa upande wa MANCHESTER UNITED.

= = = =
PORTO yasonga mbele EUROPA LEAGUE
Katika UEFA ndogo ama EUROPA LEAGUE FC PORTO ikiwa nyumbani imefungwa bao MOJA kwa BILA lakini imefuzu kusonga mbele katika ligi hiyo kwa faida ya goli la ugenini.

Shuti lililopigwa na mchezaji wa PORTO lilikwwenda kugonga mwamba wwa pembeni kabla ya ALVARO kupiga shuti lililokwenda nje.

PORTO waliendelea kuliandama lango la SEVILLA safari hii tena mpira uligonga mwamba baada ya kupigwa kichwa na FALCAO.

Kwenye dakika ya 70 LUIS FABIANO mchezaji wa zamani wa PORTO aliipatia SEVILLA goli la pekee la mchezo huo.

Dakika chache baadaye PORTO walipunguzwa mchezaji mmoja baada ya ALVARO kucheza ndivyo sivyo.

SEVILLA nao wwakapunguzwa mchezaji mmoja baada ya ALEXIS kupewa kadi ya njano ya pili.

Sasa PORTO imefuzu kucheza hatua ya 16 bora ya ligi hiyo na itakutana na CSKA MOSCOW ya URUSI.

= = ==.
ARSENAL yaichapa STOKE EPL.

Wakati ligi ya mabingwa barani ulaya ikichezwa jana usiku, ligi kuu soka ya ENGLAND pia ilichezwa jana usiku kwa mchezo mmoja tu kati ya ARSENAL wakiwa EMIRATES dhidi ya STOKE CITY.

ARSENAL imeisogelea MANCHESTER UNITED sasa ikiwa nyuma kwa pointi moja baada ya kushinda goli MOJA kwa bila dhidi ya STOKE.

Goli la ARSENAL limepatikana katika dakika ya 7 mfungaji akiwa SEBASTIAN SQUILACHI aliyefunga kwa kichwa kufuatia kona iliyopigwa na JACK WILSHERE na NICKLAS BENDTNER kumtengenezea SQUILACHI.

Kwenye dakika ya 13 ARSENE WENGER alilazimika kumtoa nahodha CES FABREGAS ambaye alikua ameumia msuli wa mguu na kumwingiza ANDREI ASHARVIN.

STOKE ilijaribu kusaka bao la kusawazisha lakini ngome ya ARSENAL ilikua imara kuhakikisha inaokoa hatari zote zilizokua zinapelekwa langoni mwake.

ARSENAL ilipata pigo tena katika dakika ya 68 pale winga wake THEO WALCOT alipoumia kifundo cha mguu na kutolewa nje kwa machela.

Juhudi za STOKE kutaka kusawazisha bao hilo hazikuzaa matunda kwani mpaka dakika tisini zinamalizika bao hilo ndilo lilikua pekee katika mchezo huo.

Hata hivyo meneja wa ARSENAL ARSENE WENGER amesema kuwa winga wake THEO WALCOT ataukosa mchezo wa fainali ya kombe la CARLING siku ya Jumapili dhidi ya BIRMINGHAM kutokana na majeraha hao aliyoyapata.

Kuhusu nahodha wake CESC FABREGAS WENGER amesema ni ngumu kugundua mapema kuwa ameumia kiasi gani kwani wanatazamia kumfanyia uchunguzi leo.

= = =







No comments:

Post a Comment