Tuesday, April 12, 2011

MANYARA STARS kupaa Ijumaa kuikabili UGANDA Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 , MANYARA STARS inatarajiwa kuondoka ijumaa kuelekea jijini KAMPALA , UGANDA kucheza na timu ya taifa ya nchi hiyo katika michuano ya hatua za awali ya kanda ya TANO ya ALL AFRICAN GAMES jumamosi ijayo. Afisa habari wa TFF BONIFACE WAMBURA amesema msafara wa timu hiyo ya MANYARA STARS utakaokuwa na jumla ya watu THELATHINI, utaongozwa na HAFIDH ALLY. Aidha WAMBURA amesema timu hiyo ambayo hivi sasa inaendelea na mazoezi yake huko BAMBA BEACH KIGAMBONI, inatarajiwa kuwasili siku ya Jumapili tayari kujiandaa na mechi ya marudiano itakayochezwa APRIL 30, mwaka huu. Endapo MANYARA STARS itafuzu hatua hiyo ya awali , itacheza na mshindi baina ya KENYA na ERITREA , june 24 ama 26, mwaka huu. Timu hiyo ya MANYARA STARS ilianza vyema katika michuano ya kucheza fainali za OLIMPIKI mwakani kwa timu za vijana, baada ya kuiondosha timu ya taifa ya CAMEROUN kwa jumla ya penati 4-3, baada matokeo ya jumla ya sare ya mabao MATATU kwa MATATU. === mziki wa JAZZ kutumbuiza dar mwishoni mwa juma Tukio la mziki wa JAZZ kwa ajili ya kukuza vipaji vya wanamziki wa jipukizi wa Tanzani litafanyika mwishoni mwa wiki hii jijini DSM. Mratibu wa tukio hilo BOBBY RICKETS ambaye pia ni mwanamziki wa JAZZ toka Marekani amesema wameamua kufanya tukio hilo hapa nchini kwa kuwa bara la Afrika ndio chibuko la mziki huo. Kwa upande wao afisa wa ubalozi wa Marekani nchini anayeshulika na masuala ya utamaduni ROBERTO QUIROZ na mwakilishi wa sumaria THABITI CHIMWENDA wamesema wamedhamini tukio hilo kwa vile linalenga kuinua vipaji vya wanamziki wa Tanzania hasa katika mziki wa JAZZ. Tukio hilo pia litatumika kwa ajili ya kuchangisha fedha ambazo zitatumika kuwasaidia watoto wanaishi katika mazingiara magumu hapa mchini. === kimwana wa TWANGA NA KUPEPETA kutafutwa dsm mashindano ya kumtafuta kimwana wa twanga na kupepeta lilijulikanalo kama manyele kimwana limeanza na fainali zake zitafanyika may sita jijini dsm. Mratibu wa shindano hilo maimatha jese na mwanamziki wa twanga na kupepeta luiz buntu wamesema hiyo ni furusa nyingine kwa akina dada kujitokeza ili kuonyesha vipaji vyao katika kucheza. Mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajinyakulia zawadi ya duka la vipodozi lenye thamani ya shilingi laki tano ili ajiajiri kama mjasiriamali. === Kindumbwe ndumbwe ligi ya mabingwa kuendelea. USIKU leo kutkauwa na michezo miwili ya ligi ya mabingwa barani ULAYA ikiwa ni michezo ya awamu ya pili baada ya ile ya kwanza kufanyika wiki mbili zilizopita. Mchezo unaozungumzwa sana ni kati ya CHELSEA na MANCHESTER UNITED kwani MAN UNITED wii mbili zilizopita iliweza kuibuka na ushindi wa goli MOJA kwa bila katika uwanja wa CHELSEA , STANFORD BRIDGE na leo MAN UNITED ipo nyumbani kucheza na CHELSEA. Kocha wa CHELSEA, CARLO ANCELOTTI, tayari amekanusha kutokuwa na presha yoyote endapo timu yake itatolewa na MANCHESTER UNITED katika mashindano hayo ya ULAYA. Ancelotti tayari amehakikishiwa na mmiliki wa klabu hiyo, ROMAN ABRAMOVICH kuwa kibarua chake kipo pale pale na kitaheshimiwa hadi utakapomalizika mwakani. == Ni SHAKHTAR na BARCELONA. Nayo timu ya SHAKHTAR DONETSK inaingia dimbani leo kucheza na BARCELONA katika mchezo ambao ni mgumu kwa SHAKHTAR, kwani tayari imechapwa magoli MATANO kwa MOJA na BARCELONA. Mbali na suala hilo pia SHAKHATAR itamkosa nahodha wake DARIO SRNA ambaye ni majeruhi tangu alipocheza mchezo wa awali huko HISPANIA. Wengine ambao ni majeruhi ni OLEXANDR KUCHER na beki wa zamani wa BARCELONA anayechezea SHAKHTAR hivi sasa DMYTRO CHYGRYNSKIY. Nao BARCELONA inakabiliwa na majeruhi kama akina CARLES PUYOL, ERIC ABIDAL na BOJAN KRKIC, huku ANDRES INIESTA akiwa na adhabu hivyo hatocheza leo. KESHO ligi hiyo itaendelea kati ya SHAKA SIFURI NNE ya UJERUMAN inaikaribisha INTER MILAN ya ITALI Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya TOTTENHAM HOTSPURS ya UINGEREZA inaikaribisha REAL MADRID. == Mashindano ya olympiki ya 2018 yaingia katika ushindani PILIKA PILIKA kutafuta uandaaji wa mashindano ya nyakati za baridi ya Olympiki kwa mwaka 2018, ambayo yanafahamika kama mashindano ya ISHIRINI na TATU ya Olympiki ya majira ya baridi. Mashindano hayo yamepangwa kufanyika mwaka 2018 kuanzia Februari TISA hadi 24 na tayari nchi TATU zimeomba kuandaa mashindano hayo. Nchi hizo ni UFARANSA ambao wanataka kuandaa katika mji wake wa ANNECY, nchi ya UJERUMAN ambayo inataka kuandaa mashindano hayo katika mji wake wa MUNICH bna KOREA ya KUSINI ambayo inataka kuandaa mashindano hayo katika mji wake wa PYEONG-CHANG. Tayari, KOREA ya KUSINI imeanza mchakato wa kutangaza jinsi ambavyo imejiandaa na matayarisho ya mashindano hayo kwa mwaka 2018. Kamati ya kimataifa ya OLYMPIKI, JULAI SITA mwaka huu itataja mshindi wa atakayeandaa mashindano hayo. MUNICH iliwahi kuandaa mashindano hayo mwaka 1972, wakati PYEONGCHANG kwa kuandaa mara mbili na kukosa mara moja kuandaa mashindano hayo. == CHICAGO BULLS uso kwa uso na NEW YORK CITY LIGI ya mpira wa kikapu nchini MAREKANI ya NBA, imeendelea jana kwa michezo mbalimbali kuchezwa. MIAMI ikiwa nyumbani iliweza kuicharaza ATLANTA kwa vikapu 98 kwa 90, huku MIAMI ikiongoza tangu katika QUARTER ya kwanza na ya pili wakati ATLANTA nayo ikafanikiwa kuopngoza katika QUARTER ya TATU na ya NNE lakini kwa uwiano wa vikapu vidogo. Mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya ORLANDO ambayo ilifanikiwa kushinda mchezo wake dhidi ya PHILADELPHIA kwa vikapu 95 kwa 85. Mchezo wa TATU ulikuwa ni kati ya BOSTON ambao waliikaribisha WASHINGTON WIZARD na katika mchezo huo WASHINGTON ilifanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya BOSTON wa vikapu 95 kwa 94, CHARLOTTE ikaifunga NEW JERSEY 105 kwa 103. Ligi hiyo inaendelea leo kati ya wakongwe katika ligi hiyo CHICAGO na NEW YORK. ==

No comments:

Post a Comment