Tuesday, August 2, 2011

Baada ya TWIGA STARS kufanya vizuri sasa COSAFA yaialika NGORONGORO HEROES katika michuano ya VIJANA.
Baada ya kufanya vizuri kwa timu ya taifa ya wanawake ya TANZANIA, TWIGA STARS katika michuano ya COSAFA na kushika nafasi ya tatu, Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, NGORONGORO HEROES nayo imealikwa katika michuano ya vijana ya ukanda huo wa kusini mwa AFRIKA yatakayoanza DECEMBER MOJA hadi KUMI NA MBILI mwaka huu.
Afisa Habari wa TFF , BONIFACE WAMBURA amesema timu hiyo ambayo inaendelea na mazoezi chini ya kocha KIM POULSEN akisaidiwa na ADOLF RISHARD huku gharama zote zikitolewa na COSAFA.
NGORONGORO HEROES hivi karibuni iliweza kufanya vizuri dhidi ya USHELISHELI katika mechi mbili za kirafiki jijini ARUSHA ambapo iliweza kushinda mechi zote.
=== ==
TFF yatoa ratiba ya VPL
Wakati huo huo ,Shirikisho la soka nchini TFF , limetoa ratiba ya ligi kuu soka ya Vodacom raundi ya kwanza ambapo jumla ya timu zote KUMI na NNE zitashuka dimbani ambapo ratiba inaonyesha timu hasimu za SIMBA na YANGA zitakutaka OCTOBER 29 katika mzunguko wa kwanza na APRIL MOSI katika mzunguko wa pili.
Katika za raundi ya kwanza ya Ligi hiyo inayoanza AUGUST 20 na 21, JKT OLJORO watakuwa wenyeji wa SIMBA mjini ARUSHA , ilhali YANGA watakuwa wenyeji wa JKT RUVU katika mechi ambayo itachezwa katika uwanja wa TAIFA jijini DAR ES SALAAM AUGUST,21.
Katika siku ya ufunguzi AUGUST 20, TOTO AFRICANS ya MWANZA itafungua dimba katika UWANJA WA CCM KIRUMBA dhidi ya VILLA SQUAD,COASTAL UNION ikichuana na MTIBWA SUGAR,KAGERA SUGAR itaialika RUVU SHOOTING,nao maafande wa POLISI DODOMA wakiikaribisha AFRICAN LYON katika uwanja wa JAMHURI mjini DODOMA.
Mechi nyingine ya ufunguzi itakuwa ni baina ya AZAM FC ambayo itaikaribisha JKT RUVU katika UWANJA WA CHAMAZI.
= =

No comments:

Post a Comment