Tuesday, August 2, 2011

Vilabu vinane vya gofu kuchuana Arusha


Vilabu vinane vya mchezo wa gofu vinatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kutafuta klabu bingwa ya taifa ambayo yanatarajiwa kufanyika jijini ARUSHA siku ya jumamosi na jumapili ijayo.
Akizungumza na TBC Afisa Tawala wa chama cha gofu Tanzania (TGU) SOFIA NYANJERE amesema lengo la mashindano hayo ni kuchangua timu ya taifa ya gofu ambayo itashiriki mashindano ya CHALENGE kwa nchi za Afrika Mashariki na kati yatakayo fanyika mwezi NOVEMBA jijini ARUSHA.

Vilabu vitakavyo shiriki katika michuano hiyo ni LUGALO, MFINDI, ARUSHA, MOROGORO, DSM GYMKHANA, TPC, MOSHI na KILOMBERO.
== ==

No comments:

Post a Comment