Tuesday, August 2, 2011

Timu ya taifa ya Kuogelea yarudi mikono mitupu


Ukosefu wa uzoefu na vifaa vya kisasa vya michezo pamoja na maandalizi duni , imetajwa kama sababu ya kushindwa kufanya vizuri kwa Timu ya taifa ya mchezo wa kuogelea ambayo imewasili leo ikitokea CHINA ambapo ilikuwa ikishiriki katika mashindano ya KUMI NA NNE ya mchezo huo duniani .
Mmoja wa wachezaji wa timu hiyo AMAR GHADIARI pamoja na kocha wa timu hiyo RAMADHAN KHAMIS wamesema ili TANZANIA iweze kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa ya kuogelea katika siku za usoni , serikali inabidi itilie mkazo katika michezo mingine ukiwamo mchezo wa kuogelea , huku akieleza changamoto alizozipata katika michunao hiyo.
Timu ya taifa ya TANZANIA haikuwerza kupata medali hata MOJA katika michuano hiyo ambapo kwa upande wa nchini za AFRIKA , AFRIKA YA KUSINI , TUNISIA na MISRI ndio nchi pekee zilizonyakua medali huku wenyeji CHINA na MAREKANI zikifanya vizuri.
==

No comments:

Post a Comment