Wednesday, October 10, 2012


Klabu ya SIMBA yawasili jijini TANGA.
KATIKA hatua nyingine mabingwa wa soka nchini SIMBA ya DSM imewasili mjini TANGA tayari kwa mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya wenyeji wa COSTAL UNION mchezo utakaochezwa katika uwanja wa MKWAKWANI mjini humo siku ya jumamosi.
Msemaji wa klabu ya SIMBA, EZEKIEL KAMWAGA amewataka mashabiki wa klabu hiyo kutojiingiza katika vitendo vitakavyosababisha klabu hiyo kutozwa faini.
Kiungo wa simba RAMADHANI CHOMBO REDONDO hakuondoka na kikosi cha SIMBA kwenda TANGA kwa kuwa anasubuliwa na MALARIA,lakini akaeleza kurejea kwa mshambuliaji wa timu hiyo MRISHO NGASSA ambaye atacheza katika mchezo huo.
Michezo mingine itakayochezwa jumamosi ni katika uwanja wa JAMHURI mjini MOROGORO ambapo POLISI MORO itacheza na AZAM FC, TANZANIA PRISONS itacheza na JKT OLJORO.
Michezo mingine RUVU SHOOTING itacheza na AFRICA LYON na MTIBWA SUGAR itacheza na MGAMBO JKT.
====
Wagombea sita soka la wanawake wapingwa
WAGOMBEA sita wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) wamewekewa pingamizi na wadau wa mchezo huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, wagombea hao ni JOAN MINJA anayewania nafasi ya Mwenyekiti ambaye amewekwa pingamizi na wadau sita. Pia ISABELLAH KAPERA ambaye anagombea uenyekiti amewekewa pingamizi moja.

Wagombea watatu wa nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nao wamewekewa pingamizi.

Wagombea hao ni JULLIET MNDEME ana pingamizi sita , Zena Chande ana pingamizi NNE na Jasmin Soud mwenye pingamizi tatu.

Naye Rahim Maguza anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji amewekewa pingamizi moja.

Licha ya pingamizi hizo, wagombea wote wanatakiwa kuhudhuria usaili wakiwa na vyeti vyao halisi vya kitaaluma utakaofanyika Oktoba 12, 13 na 14 mwaka huu kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi.
 ===

No comments:

Post a Comment