Thursday, February 17, 2011

Michezo mbalimbali duniani

YANGA uso kwa uso na KAGERA.

YANGA leo inajarabu kutoa machungu ya kuondolea katika kombe la shirikisho barani Afrika na DEDEBET ya ETHIPIOA itakapo teremka dimbani kumenyana KAGERA SUKARI katika dimba la KAITABA jioni ya leo.

Iwapo YANGA itaibuka kidedea dhidi ya KAGERA itareja kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara kwani itakuwa imejikusanyia ALAMA 35 nyuma ya SIMBA ambayo inaongoza ligi hiyo kwa sasa ikiwa na Alama 34.

Mabingwa wa kandanda WEKUNDU wa MSIMBAZI SIMBA wamepunguzwa kasi ya kuongeza ligi kuu ya kandanda Tanzania Bara baada ya sare ya magoli MAWILI kwa MAWILI na TOTO AFRIKA ya MWANZA.

Magoli ya SIMBA yamepachikwa wavuni na MBWANA SAMATA na goli la pili ni la kujifunga mwenyewe mlinda mlango wa TOTO AFRIKA WILBERT MWETA.

Magoli ya TOTO yamefungwa TETE KANG’ANG’A na goli la pili likifungwa na MOHAMED SUDI katika dakika ya lala na buriani.

AZAM FC jana nao waliendeleza ubabe wao wa kushinda michezo yake baada ya kuibungiza bila huruma AFRICAN LYON mabao matatu BILA.

Magoli ya AZAM yamefungwa na MRISHO NGASA, MAO MKAMI, na RAMADHANI CHOMBO RIDONDO

===

ARSENAL yaichapa BARCELONA

Ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea jana katika viwanja viwili tofauti jijini LONDON kwenye uwanja wa EMIRATES ambapo ARSENAL waliwakaribisha BARCELONA na kwenye uwanja wa STADIO OLIMPICO nchini ITALI kati ya AS ROMA na SHAKHTAR DONETSKY.

Tuanzie EMIRATES ambapo kulikua na mchezo wa kukata na shoka ARSENAL imewashangaza mashabiki wa BARCELONA baada ya kutoka nyuma goli moja na kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya 16 bora.

ARSENAL ndio waliokua wa kwanza kuanza kuleta kashikashi langoni mwa BARCA lakini shuti la ROBIN VAN PERSIE liliokolewa na kipa wa BARCA VICTOR VALDES.

LIONEL MESSI almanusura aipatie BARCA goli la kuongoza lakini mpira alioupiga ulikwenda nje sentimeta chache.

LIONEL MESSI tena aliendelea kuisumbua ngome ya ARSENAL safari hii akipenyeza pasi safi iliyomkuta DAVID VILLA ambaye hakufanya hajizi na kuandika goli la kuongoza kwa BARCA katika dakika ya 25.

BARCA tena wakapata goli la pili lakini mwamuzi wa pembeni alionesha kibendera juu kuashiria kuwa mfungaji alikua tayari ameshaotea.

Kipindi cha pili ARSENAL ilikuja juu kutaka kusawazisha goli hilo na juhudi zao zikazaa matunda katika dakika ya 77 pale GAEL CLISHY alipompa pasi ROBIN VAN PERSIE ambaye aliachia shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Dakika ya 82 ANDREI ASHARVIN aliwanyanyua tena mashabiki wa ARSENAL kwa kuandika goli la pili na la ushindi kwa timu yake baada ya kutokea shambulizi la kushitukiza ambapo NASRI alimpatia ASHARVIN pasi ya goli.

Hii ni mara ya kwanza kwa ARSENAL kushinda dhidi ya BARCELONA na timu hizi zitakutana tena katika mchezo wa pili wa hatua hii ya 16 bora baada ya wiki tatu CAMP NOU.
= = = = = = =

Kwenye uwanja wa STADIO OLIMPICO AS ROMA wakiwa nyumbani wameshindwa kuutumia vyema uwanja wao baada ya kupata kichapo cha goli 3 kwa 2 dhidi ya SHAKHTAR DONETSKY.

ROMA walianza walikosa goli kwenye dakika ya 20 baada ya mchezaji wake kupiga kichwa kilichokwenda nje.

Kwenye dakika ya 28 ROMA walipata goli la kuongoza baada ya mchezaji wa SHAKHTAR RAZVAN RAT kujifunga.

SHAKHTAR walisawazisha goli hilo kwenye dakika ya 29 ikiwa ni dakika moja tu mfungaji akiwa ni JADSON.

Wageni hao hawakutosheka kwani walipata goli la pili kwenye dakika ya 36 mfungaji akiwa DOUGLAS COSTA kabla ya LUIS ADRIANO kufunga goli la tatu kwenye dakika ya 41.

Katika kipindi cha pili ROMA walifanikiwa kupata goli la pili JEREMY MENEZ akiachia shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Hadi mwisho wa mchezo SHAKHTAR 3 AS ROMA 2.
= = = = = = = =

FIFA yataka vilabu kutimiza vigezo ili kushiriki mashindano ya kimataifa

Vilabu vya soka hapa nchini vimetakiwa kuanza mchakato wa kutekeleza vigezo vinavyotakiwa na shirikisho la soka la kimataifa FIFA ili viweze kupewa leseni ya kushiriki kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Moja ya wakufunzi wanaoendesha semina ya FIFA kwa viongozi wa vilabu hapa nchini HENRY TANDAU anasema FIFA imejiwekea malengo ya miaka michache ijayo ya kuhakikisha kila klabu inakidhi vigezo 13 vya FIFA ili vilabu hivyo viweze kutambuliwa na chombo hicho cha juu cha soka duniani.

TANDAU ametaja baadhi ya vigezo vinavyotakiwa kutekelezwa na vilabu kuwa ni pamoja na ukaguzi wa mahesabu, klabu itambuliwe kisheria, klabu iwe na ofisi inayotambulika, klabu iwe watendaji wa kuajiriwa, iwe na uwanja, shule ya kukuza vipaji na masuala mengine.

Baada ya somo hili baadhi ya wasemaji wa vilabu akiwemo ANDREW CHATWANGA wa MAJIMAJI na LEONARD KIJANGWA wa POLISI TANZANIA wanasema wana imani vilabu vyao vitatekeleza maagizo haya FIFA.

Hata hivyo cha ajabu ni kwamba kati ya vilabu 12 vinavyoshiriki ligi kuu, ni vilabu sita tu vya SIMBA, YANGA, MAJIMAJI, POLISI TANZANIA,AFRICAN LYON,na AZAM FC vinashiriki.
= = =

CONTADOR arejea kwenye mbio za baiskeli.

Bingwa wa mbio za TOUR DE FRANCE ALBERTO CONTADOR amerejea katika mashindano ya kuendesha baiskeli katika mbio za TOUR DE ALGARVE hapo jana baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya kufungiwa mwaka mmoja kutokana na madawa.

CONTADOR alifungiwa kwa muda baada ya kugundulika ametumia madawa ya kuongeza nguvu katika mbio za TOUR DE FRANCE za mwaka jana.

CONTADOR amesema anafurahia kurejea tena katika mashindano hayo na kuongeza kuwa kurejea kwake kumeleta faraja sio tu kwake bali pia kwa timu pamoja na wadhamini wake.

CONTADOR mwenye miaka 28 amekua akisema kuwa hana hatia na kudai kuwa nyama aliyokula iliyokua imechanganywa na vitu ndio sababu ya kushindwa kwa kipimo chake.

= = = = == ===
MURRAY AJITOTA KUWANIA UBINGWA WA TENESI WA DUBAI

Mchezaji nambari moja wa tenesi wa UINGEREZA ANDY MURRAY amejitoa kushiriki katika mashindano ya wazi ya tenesi ya Dubai kutokana na maumivu ya kiuno.

Murray ambaye amecheza fainali mara moja ya US Open na mara mbili Australian Open alipanga kupumzika baada ya kushindwa katika mchezo wa fainali ya Australian Open mwezi uliopita lakini akaona ageweza kucheza mashindano hayo ya DUBAI lakini maumivu yamemzuia kufanya hivyo.

Murray ambaye ni mchezaji namba tano kwa ubora wa tenesi duniani alishiriki mashindano hayo ya DUBAI mwaka jana ikiwa ni baada ya kupoteza mchezo wake wa fainali ya mashindano ya wazi ya AUSTRALIA.

===

No comments:

Post a Comment