Tuesday, February 22, 2011

TIMU YA TAIFA YA VIJANA MIAKA 23 YATAGAZWA

Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 cha kuivaa CAMEROON chatangazwa.

Kocha mkuu wa timu ya taifa vijana chini ya umri wa miaka 23 JAMHURI KIWELO (JULIO) ametangaza kikosi cha wa chezaji 25 wa kikosi hicho tayari kuikabili CAMEROON katika mchezo wa kuwani kufunzu kwa mashindano ya OLYMPIC jijini LONDON mwakani,mchezo huo wa awali utapigwa mjini YAOUNDE machi 26.

Akitangaza majini ya wachezaji wa kikosi hicho jijini dsm hii leo KIWELO amesema wachezaji wa kikosi hicho wamechanguliwa baada ya kuonyesha viwango vya hali ya juu katika mashindano mbalimbali yakiwemo yale ya timu za vijana chini ya umri wa miaka 20 za vilabu vya ligi kuu na fainali ya ligi daraja la kwanza yaliyomalizika jana jijini TANGA.

Kwa upande wake AFISA habari wa shirikisho la soka nchini TFF BONIFANCE WABURA amesema shirikisho lake linafanya kila jitihada kuhakikisha timu hiyo ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 inacheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa ya kujipima nguvu kati ya MACHI 12 na 13 ama 19 na 20 kabla ya kuivaa timu ngumu ya CAMEROON.

Kikosi hicho kinaanza mazoezi kesho kabla ya kuweka kambi FEBRUARI 26 na kinatarajiwa kuondoka nchini kwenda CAMEROON Machi 22.

===
TFF yavitaka vilabu vilivyopanda daraja kujiandaa kwa ligi kuu

Shirikisho la soka nchini TFF limevitaka vilabu vya vinne vilivyopanda daraja hadi ligi kuu Tanzania bara kujiandaa vilivyo ili kukabili ushindani katika ligi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM Afisa Habari wa TFF, BONIFANCE WABURA amesema baada ya kupanda daraja hadi ligi kuu na kujipongeza kwa viongozi,wachezeja na mashabiki wa timu hizo kazi kwao sasa ni kujipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji watakamudu heka heka za ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.

Timu zilizopanda daraja kutoka ligi daraja la kwanza katika fainali zilizomalizika jana jijini tanga ni VILA SQUAD na MORO UNITED zote za DSM, COASTAL UNION ya TANGA na JKT OLJORO.

===
TIGO YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI
Kapuni ya simu za mkononi ya TIGO leo imekabidhi zawadi ya pessa taslimu zenye thamani ya shilingi miloni 22 kwa washindi 22 walioshinda katika promosheni ya bahatisha na tigo.
Akikabidhi zawadi hizo jijini DSM hii leo mwakilisho wa TIGO MASANJA REDEMPTUS amewataka wateja wa tigo kuendelea kushiriki katika bahati na sibu hiyo kwani zawadi bado ni nyingi.

Kwa upande wao washindi wa zawadi hizo LULU MOHAMED na PIUS MABULA hawakusita kuelezea furaha zao baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

Hii ni mara ya nne kwa TIGO kukabidhi zawadi ya fedha taslimu tangu bahati na sibu hiyo ianze kuchezeshwa na inamalizika MACHI 28.
===

COSOTA Rukwa kufanya msako kusaka wezi wa kazi za wasanii.

Katika kuhakikisha kuwa wasanii wa muziki wananufaika na mauzo ya kazi zai chama cha haki miliki Tanzania (COSOTA)mkoani Rukwa kimeanza msako kwa wenye maduka ya kanda pamoja na wale wanaotembeza mitaani ikiwa pamoja na kuwapa elimu kutokana na wengi wao kutojua sheria za hati miliki.
Akizungumza na TBC mwakilishi wa COSOTA mkoa wa Rukwa Abuu Majeki amesema zoezi hilo limeshafanyika wilaya ya Mpanda huku wengi wa wafanyabiasahara wa kanda wakionyesha mwitikio mkubwa katika kutunza kazi za wasanii ikiwa pamoja na kuzigundua kazi feki wanazoletewa
Kwa upande wake moja ya mfanyabiashara wa kanda katika maduka ya Sumbawanga Godfrey Enock anasena bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwapo ya baadhi ya machinga kudurufu kazi na kuuza kwa bei ya chini tofauti na wao

===

ANCELOTTI ana matumaini na CHELSEA kufanya vizuri

TUANZE na ligi ya mabingwa Ulaya ambapo kocha wa CHELSEA, CARLO ANCELOTTI amesema timu bado ina uwezo mkubwa wa kufanya vizuri katika mashindano ya ULAYA ijapokuwa timu yake ipo katika wakati mgumu kimchezo kwa sasa.

Kombe la ligi ya mabingwa barani ULAYA ndio kimbilio la CHELSEA kwa sasa kwani imeondolewa katika mashindano ya kuwania kombe la FA na kwa sasa ipo katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu nchini humo.

CHELSEA leo ipo ugenini kucheza na timu ya FC COPENHAGEN ya DENMARK katika mashindano ya ligi ya mabingwa barani ULAYA.

==
MOURINHO na kibarua kigumu dhidi ya LYON
HUKO UFARANSA, kocha wa REAL MADRID ya HISPANIA, JOSE MOURINHO, ana kibarua cha kuikabili timu ya UFARANSA ya OLYMPIC LYON.
Yenyewe REAL MADRID ina lengo la kucheza robo fainali ya mashindano hayo kwa msimu huu.
Katika kikosi cha MOURINHO amemjumuisha SERGIO CANALES na PEDRO LEON.
Lakini kuna mjadala kuwa ni nani atachezeshwa katika kambi ya ushambuliaji kati ya EMANUEL ADEBAYOR au KARIM BENZEMA.
Huku mlinda mlango IKER CASILLAS, akitarajia kurudi katika mchezo wa leo kuchukua nafasi ya ANTONIO ADAN, ambaye alikaa langoni jumamosi iliyopita baada ya CASILLAS kutumikia adhabu.
Michezo mingine itachezwa kesho kati ya INTER MILAN ya ITALIA itaikaribisha BAYERN MUNICH ya UJERUMAN na MARSEILLE ya UFARANSA itacheza na MANCHESTER UNITED ya UINGEREZA.
==
GATTUSO afungiwa mechi NNE

MCHEZAJI wa AC MILAN, GENNARO GATTUSO amefungiwa kutocheza michezo MINNE baada ya kuzozana na kumpiga kocha msaidizi wa timu ya TOTTENHAM, Joe Jordan wakati wa mchezo wao wa raundi ya kwanza ambapo AC MILAN ilifungwa.

Kiungo huyo alimpiga kichwa kocha huyo baada ya kipigo cha kufungwa goli MOJA kwa Sifuri katika uwanja wa SAN SIRO.

UEFA imepotoa adhabu hiyo jana , na tayari GATUSSO amekiri kosa lake na AC MILAN imesema haitakata rufaa kupinga maamuzi ya UEFA.
==
MONTELLA ateuliwa kocha wa muda ROMA

TIMU ya ROMA imemteua VINCENZO MONTELLA kuwa kocha wa timu hiyo hadi mwisho wa msimu huu baada ya kocha CLAUDIO RANIERI kujiuzulu.

MONTELLA, awali alikuwa ni kocha wa klabu hiyo upande wa vijana ambapo kocha huyo ataanza kibarua chake kwa kucheza ugenini dhidi ya timu ya BOLOGNA kesho katika mchezo wa ligi kuu soka nchini ITALIA.
Kujiuzulu kwa RANIERI,kunatokana na timu hiyo kufungwa mechi nne mfululizo na hivyo kuifanya timu hiyo kushikilia nafasi ya NANE katika msimamo wa ligi nchini humo.
MONTELLA amewahi kucheza katika klabu za FULHAM ya UINGEREZA.

==
WEST HAM yairarua BURNLEY

WEST HAM UNITED imeicharaza BURNLEY magoli MATANO kwa MOJA katika mashindano ya kombe la FA ya UINGEREZA.

Lakini leo kutakuwa na michezo miwili ya ligi kuu nchini UINGEREZA kati ya BLACKPOOL ambayo itacheza na TOTTENHAM.

Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya ARSENAL ambayo itacheza na STOKE CITY.

==

No comments:

Post a Comment