Tuesday, July 26, 2011




TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA
Karume Memorial Stadium, Uhuru/Shaurimoyo Rd – Ilala
P.O. Box 1574, Dar Es Salaam, Tanzania
Telefax: +255 22 2861815, Email: tfftz@yahoo.com, Website: www.tfftanzania.com
RATIBA YA LIGI YA TAIFA NGAZI YA TAIFA FAINALI
06 AUGUST, 2011 - 14 AUGUST, 2011

KUNDI A KUNDI B KUNDI C
A Polisi Morani FC A Polisi Central Dar Mlale JKT A
B Mgambo Shooting B Majengo FC Geita Vterans B
C Samaria FC C Sifapolitan FC Rumanyika FC C
D Kasulu United D Small Kids Cosmopolitan FC D

NO. TAREHE MECHI KUNDI TIMU MUDA UWANJA
1 06 Aug. 2011 1 A Samaria FC Vs Kasulu United 2:00 PM Mkwakwani C Vs D
2 Polisi Morani FC Vs Mgambo Shooting 4:00 PM Mkwakwani A Vs B
2 07 Aug. 2011 3 B Sifapolitan FC Vs Small Kids 2:00 PM Mkwakwani C Vs D
4 Polisi Central Dar Vs Majengo FC 4:00 PM Mkwakwani A Vs B
3 08 Aug. 2011 5 C Rumanyika FC Vs Cosmopolitan FC 2:00 PM Mkwakwani C Vs D
6 Mlale JKT Vs Geita Veterans 4:00 PM Mkwakwani A Vs B
4 09 Aug. 2011 7 A Mgambo Shooting Vs Samaria FC 2:00 PM Mkwakwani B vs C
8 Kasulu United Vs Polisi Morani FC 4:00 PM Mkwakwani D vs A
5 10 Aug. 2011 9 B Majengo FC Vs Sifapolitan FC 2:00 PM Mkwakwani B vs C
10 Small Kids Vs Polisi Central Dar 4:00 PM Mkwakwani D vs A
6 11 Aug. 2011 11 C Geita Veterans Vs Rumanyika FC 2:00 PM Mkwakwani B vs C
12 Cosmopolitan FC Vs Mlale JKT 4:00 PM Mkwakwani D vs A
7 12 Aug. 2011 13 A Mgambo Shooting Vs Kasulu United 2:00 PM Mkwakwani B vs D
14 Polisi Morani FC Vs Samaria FC 4:00 PM Mkwakwani A Vs C
8 13 Aug. 2011 15 B Majengo FC Vs Small Kids 2:00 PM Mkwakwani B vs D
16 Polisi Central Dar Vs Sifapolitan FC 4:00 PM Mkwakwani A Vs C
9 14 Aug. 2011 17 C Geita Veterans Vs Cosmopolita FC 2:00 PM Mkwakwani B vs D
18 Mlale JKT Vs Rumanyika FC 4:00 PM Mkwakwani A Vs C








==== ==

MCHEZAJI gofu kutoka Klabu ya Gymkhana Arusha (AGC) Madina Idd anaongoza baada ya raundi ya kwanza ya mashindano maalumu ya kutafuta nafasi nne za kuunda timu ya taifa ya mchezo huo.

Timu ya taifa inatarajia kushiriki michuano ya Kombe la Challenge Afrika Mashariki na Kati iliyopangwa kuanzia Agosti 16 hadi 18 kwenye viwanja vya Klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Dar es Salaam .

Katika mashindano hayo ya siku nne ya viwanja 72 ambayo yalianza jana, Lugalo, Madina anaongoza baada ya kurejea na mikwaju 81.

Alianza vema viwanja tisa vya mwanzo na kupiga mikwaju 36, lakini alikwama tisa ya pili alilopiga 45.

Nafasi ya pili wanakaba koo wachezaji wawili akiwepo Mchezaji wa Gofu Bora wa Mwaka 2010 Hawa Wanyeche kutoka Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam (DGC) na vetereni Sophia Viggo wa Moshi ambao kila mmoja amerejea na mikwaju 85.

Ayne Magombe wa DGC anashika nafasi ya nne akiwa na mikwaju 87, Angel Eaton wa DGC na Neema Olomi wa AGC kila mmoja alirejea na mikwaju 91.

Msimamizi wa mashindano hayo na kocha wa timu ya taifa Mbwana Juma akizungumza mara baada ya raundi hiyo alisema matokeo sio mazuri, lakini huo ni mwanzo.

“Hii ni raundi ya kwanza ngoja kesho (leo) tunaona kwa sababu kila mtu ni mgeni na uwanja,” alisema.

Mashindano hayo yanayoendeshwa na Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU) yanaendelea leo na kutarajia kumalizika Ijumaa.
====

MTIHANI WA UWAKALA WA WACHEZAJI
Mtihani wa Uwakala wa Wachezaji wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Septemba 29 mwaka huu. Mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili; maswali kutoka FIFA na kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utafanyika saa 4 asubuhi.

Kwa Watanzania wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wafike TFF ili waweze kupewa taratibu za mtihani huo ambao ada yake ni dola 50 za Marekani.

Wahusika wa mtihani huo ni wale wanaotaka uwakala kwa mara ya kwanza. Kwa wale wenye leseni za uwakala wanatakiwa kuziuhisha (renew) kila baada ya miaka mitano.

Mpaka sasa Tanzania ina mawakala saba wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni Ally Mleh wa Manyara Sports Management, Damas Ndumbaro, John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.

RHINO SPORTS YAUZWA MBEYA
Halmashauri ya Jiji la Mbeya (Mbeya City Council) imeinunua timu ya daraja la kwanza ya Rhino Sports Club ya Arusha. Hivyo timu hiyo sasa makao makuu yake yatakuwa Mbeya na itaitwa Mbeya City Council Sports Club- MCC.

Pia uongozi wa Halmashauri hiyo umemteua Kocha Juma Mwambusi kuwa Meneja wa timu hiyo na amepewa idhini ya kushughulikia usajili na taratibu nyingine za ushiriki wa MCC katika Ligi Daraja la Kwanza na mashindano mengine.

Boniface Wambura
Ofisa HabariShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
== ==== ==== ===
PRESS RELEASE
TANZANIA JUNIOR GOLF FOUNDATION
We are pleased to announce the formation of the Tanzania Junior Golf Foundation which is under the auspice of the Tanzania Golf Union.
The newly elected Junior Golf Foundation Executive Committee consists of:-
Mr. Jaffary Ally Omari – Chairman
Mr. Alfred Kinswaga – Vice Chairman
Mr. Sam Mowo – Hon. Secretary
Mr. Godfrey Kilenga – alternate Hon. Secretary
Mr. Jatin Sonecha – Hon. Treasurer
Mr. Ali Ismail –Sponsorship/Tournament Executive
Mr. Joseph Tango – Alternate, Sponsorship/Tournament Executive
Trustees:-
Mrs. Sherida Chilipachi
Mr. Titus Murage

The Committee has promised to work very hard to ensure that even children from less privileged families have access to golf. They will also work hand in hand with schools to make sure that golf is acknowledged as a curriculum sport.

We are inviting parents from all walks of life to bring their kids for the junior clinics to any golf course closer to them every Saturday morning.

Dioniz Malinzi
Chairman
Tanzania Golf Union

= =
MSAMA AUCTION MART yakamata maharamia wa muziki
Kampuni ya udalali wa mahakama ya MSAMA AUCTION MART hii leo imefanikiwa kuwatia mikononi mwa sheria wakazi watatu wa TANDIKA kwa tuhuma za kudurufu kazi za wasanii zenye thamani ya shilingi milioni tisa, laki tano na elfu thelathini na sita.
Mkurugezni wa MSAMA AUCTION MART, ALEX MSAMA amesema mbali na kuwakamata watuhumiwa hao pia wamegundua mtandano mkubwa unaojihusisha na usambazaji wa CD feki za wasanii
Watuhumiwa hao ambao wamefikishwa katika kituo cha polisi cha CHANG’MBE jijini DSM ni pamoja na FRED JUMBE, MARTIN MKINGA na MUSTAFA RASHID
Aidha MSAMA amesema kampuni yake itaendelea na oparesheni hiyo kwa nchi nzima ambapo pia ameomba ushirikiano mkubwa kutoka kwa wasanii ambao ndiyo kazi zao zimekuwa zikiibiwa.
==
J SISTERS kuzindua ALBUM JUMAPILI
Kundi la Muziki wa Injili la J SISTERS linatarajia Kuzindua albamu yao inayojulikana kama CHUKUA USHINDI Jumapili hii katika ukumbi wa DIAMOND JUBILEE.
Kiongozi wa kundi hilo JENNIFER MSHAMA amesema wamejiandaa kutoa burudani tosha katika uzinduzi huo ambapo mgeni rasmi atakuwa Mke wa RAIS MAMA SALMA KIKWETE
MSHAMA amesema Uzinduzi wa albam hiyo utasindikizwa na waimbaji wengine kama vile FROLA MBASHA na BONNY MWAITEGE.
Kundi hilo la J SISTERS ambalo linaundwa na wanamuziki ndugu ambao ni JENNFFER, JESSICAR , JAQUILLINE na JULIET kwa pamoja walionyesha utaalam wao katika kupangilia ala za sauti
= =
Warembo watano waingia fainali ILALA
Katika sanaa ya UREMBO, walimbwende watano wameingia fainali ya kumtafuta MREMBO mwenye vipaji kwa wilaya ya ILALA katika onesho litakalofanyika katika viwanja vya MNAZI MMOJA jijini DSM siku ya IJUMAA.
Warembo hao walipatakana hapo jana katika mchujo uliofanyika ukumbi wa SAVANNA LOUNGE uliopo katika jengo la QUALITY PLAZA baada ya kuonesha vipaji mbali mbali ikiwemo kucheza muziki pamoja na sanaa za asili
Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano hayo JACKSON KALIKUMTIMA maandalizi ya kumsaka MREMBO wa ILALA yamekamilika na warembo wako katika hali nzuri baada ya kumaliza ziara ya kiutalii jijini NAIROBI KENYA.

= =
MADINA aongoza michuano ya gofu ya ARUSHA OPEN
MCHEZAJI gofu kutoka Klabu ya Gymkhana Arusha (AGC) Madina Idd anaongoza baada ya raundi ya kwanza ya mashindano maalumu ya kutafuta nafasi nne za kuunda timu ya taifa ya mchezo huo.
Katika mashindano hayo ya siku nne ya viwanja 72 ambayo yalianza jana, Lugalo, Madina anaongoza baada ya kurejea na mikwaju 81.
Nafasi ya pili wanakaba koo wachezaji wawili akiwepo Mchezaji wa Gofu Bora wa Mwaka 2010 Hawa Wanyeche kutoka Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam (DGC) na vetereni Sophia Viggo wa Moshi ambao kila mmoja amerejea na mikwaju 85.
Ayne Magombe wa DGC anashika nafasi ya nne akiwa na mikwaju 87, Angel Eaton wa DGC na Neema Olomi wa AGC kila mmoja alirejea na mikwaju 91.
= =
ALIYEKUWA mpinzani katika uchaguzi wa shirikisho la soka duniani FIFA na rais wa shirikisho la soka huko ASIA , MOHAMED BIN HAMMAM anapanga mkakati wa kukata rufaa katika chombo cha michezo cha COURT OF ARBITRATION FOR SPORT (CAS) kupinga kufungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka.
BIN HAMMAM anasema kufungiwa kwake kuonaonyesha dhahiri ni cha kulipiza kisasi baada ya yeye kujitosa kupambana na SEPP BLATTER katika uchaguzi uliofanyika JUNE MOSI mwaka huu.
Hadi jana usiku, BIN HAMMAM alikuwa bado yupo katika orodha inayoonyesha kuwa BIN HAMMAM bado ni rais wa shirikisho la soka la bara la ASIA.
Kamati ya maadili ya FIFA imebainisha kuwa BIN HAMMAM alitoa na kupokea rushwa kwa nyakati tofauti.
==
TIMU ya CHELSEA imewasili HONG KONG tayari kwa michezo maalum ya mashindano ya ASIA.
CHELSEA itacheza kesho na mabingwa wa ligi ya soka ya HONG KONG timu ya KITCHEE katika mchezo wa NUSU fainali ya mashindano hayo maalum huko ASIA.
Huku timu ya ASTON VILLA nayo ikitarajia kucheza na BLACKBURN ROVERS katika michezo itakayochezwa katika uwanja wa HONG KONG.
CHELSEA inashiriki katika mashindano haya huku ikiwa imeifunga Magoli MANNE kwa BILA tiomu ya THAILAND ikiwa ni mwendelezo wa mashindano ya ASIA.
Mashindano haya hufanyika kila baada ya miaka MIWILI kupita .
==
MCHEZAJI wa zamani wa mpira wa kikapu katika ligi ya MAREKANI ya NBA ambaye ni anatokea nchini CHINA, YAO MING ameagwa rasmi baada ya kutangaza kustaafu kucheza mchezo huo.
YAO anapongezwa kwa jitihada zake za kuhamasisha wachezaji chipukizi kuiga mfano wa kuwa na haja ya kucheza mpira wa kikapu katika kiwango cha kimataifa.
YAO mwenye miaka 31, mapema JULY 20 mwaka huu alitangaza kustaafu katika klabu ya HOUSTON ROCKETS ya MAREKANI mbele ya mashabiki wa CHINA waliokusanyika katika uwanja wa SHANGHAI kushuhudia kupongezwa kwa mchezaji huyo aliyechezea misimu NANE ligi ya NBA.
Lakini YAO hakuweza kusema chochote kama atashiriki katika mashindano ya 2012 ya OLYMPIKI akiwa na timu ya taifa ya kikapu ya CHINA katika mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment