Tuesday, June 28, 2011

MIichezo ya leo

WEKUNDU wa MSIMBAZI SIMBA katika michuano ya kombe la KAGAME, lazima kieleweke watakapocheza na ZANZIBAR OCEAN VIEW.

SIMBA walioko kwenye kundi A wana pointi MOJA tu bila goli, wakati ZANZIBAR OCEAN VIEW wao ndo vinara wa kundi hili wakiwa na pointi SITA na magoli MATANO ya kufunga na wamefungwa magoli MAWILI tu, na kama watashinda leo ama kutoka sare watakuwa wamekata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali.

SIMBA ni watanzania, ZANZIBAR OCEAN VIEW ni watanzania pia, sasa hapa sijui kutakuwa na udugu ama tikiwa uwanjani hakuna udugu?

= = =

Jana kulikuwa na mechi mbili za Kombe la KAGAME na kule MOROGORO klabu ya soka ya ST.GEORGE ya ETHIOPIA imecheza na ULINZI ya KENYA.

Timu hizi zimefungana goli MOJA kwa MOJA.

Walianza ST.GEORGE kufunga na ndipo wakasawazisha ULINZI na habari zinasema ULINZI walizembea wenyewe katika kipindi cha pili cha mchezo kwasababu walipata nafasi za kufunga wakashindwa kuzitumia.

Jijini DSM BUNAMWAYA ya UGANDA imeionesha kazi ELMAN FC ya SOMALIA kwa kuinyuka kwa magoli MANNE kwa BILA, na hii ni mechi ya kundi Be ambapo hapo kesho ELMAN itakutana na YANGA.

YANGA nao wanakazi ya kufanya kwa kweli kwasababu walitoka sare ya magoli MAWILI kwa MAWILI na klabu tya EL MEREIKH ya SUDAN, klabu inayotajwa kwamba mpaka sasa ndio iliyoonesha soka safi na la kuvutia na ukomavu wa uwanjani.

Wapachikaji wa magoli wa YANGA JERY TEGETE, na KENETH ASAMOAH ni majeruhi mpaka sasa, hivyo kabaki DAVIS MWAPE peke yake japokuwa kuna habari zinazodai mpachika magoli wa YANGA mpya KIZZA HAMIS kutoka UGANDA angefika nchini jana.

= = =

Leo katika jambo SPORTS tunaipongeza KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI ya UMISETA, Umoja wa Michezo Shule za Sekondari kwa kuchaguliwa kuunda timu itakayowakilisha TANZANIA kwenye michezo ya Umoja wa shule za sekondari AFRIKA MASHARIKI itakayofanyika nchini UGANDA mwezi JULAI mwaka huu.

Wachezaji hawa chipukizi wa mikoa ya MBEYA, IRINGA na SONGEA wanaunda timu ya wachezaji 20 wa kandanda na wachezaji WATANO wanariadha.

HOSEA CHEYO kutoka MBEYA amekutana na kikosi hiki kilichorejea nyumbani baada ya kumalizika kwa mashindano pale KIBAHA mkoani PWANI.

= = =

Mama ASHA BARAKA mdau mkubwa wa muziki wa dansi hapa nchini ambaye kwa sasa anaratibu shindano la MALIKIA wa TWANGA PEPETA maarufu kama KIMWANA WA MANYWELE ametangaza neema wa washiriki wa shindano hili akisema mshindi wanataka wamfanye mjasiriamali, na hapa watakuwa wameondoa tatizo la ajira.

Mama ASHA BARAKA ambaye pia ni Mkurungezi wa AFICANS STARS ENTERTAINMENT ameyasema haya alipokuwa akiwatambulisha washindanaji KUMI wa shindano hili la MALIKIA wa TWANGA PEPETA.

Mshindi wa shindano hili la MALIKIA wa TWANGA atapata zawadi ya Duka la kuunza bidhaa mbalimbali za masuala ya UREMBO, na duka lenyewe lina thamani ya shilingi MILIONI TANO.

Mshindi wa pili atapata shilingi LAKI TANO, mshindi wa tatu atapata shilingi LAKI TATU na washiriki wengine watapata kifuta cha shilingi LAKI MOJA kila moja.

= = =

Katika habari za kimataifa kama ulifuatilia kwa uzuri michuano ya WIMBLEDON tenesi ni kwamba kina dada ndugu MOJA, THE WILLIAMS SISTERS, VENUS na SERANA wameondolewa.

Sasa waliowaondoa nao wamepata wababe wao, wote wamefurushwa kwenye WIMBLEDON tenesi.

Mchezaji asiyekuwa amejulikana kama anheweza kusababisha matatizo makubwa kwenye michuano hii MJERUMANI SABINE LISICKI amemuondosha MARION BARTOLI wa UFARANSA.

SABINE amemundosha BARTOLI kwa seti 6-4 6-7 na 6-1.

Kumbuka BARTOLI ndiye aliyemuondosha SERANA WILLIAMS katika robo fainali.

Mwanadada huyu SABINE anasema kwa KIINGEREZA I'm SPEECHLESS, SINA hata cha kuongea kwa furaha niliyonayo.

= =

Kwenye mchezo mwingine TSVETANA PIRONKOVA aliyemuondosha VENUS WILLIAMS naye ameondoshwa na PETRA KVITOVA.

KVITOVA anafika nusu fainali yake ya pili kwenye michuano ya WIMBLEDON kwa kumchapa PIRONKOVA kwa seti 6-3 6-7 na 6-2.

KVITOVA mwishoni akasema nina furaha nimefika nusu fainali kwasababu kabla ya mechi nilikuwa na hofu sana.

= = =

Sasa nakuletea mama wa milio katika court za WIMBLEDON.

Huyu ni MARIA SHARAPOVA,mrembo na mwanamitindo wa URUSI aliyevuma sana mwaka 2000 mpaka 2006.

Sasa amerudi tena.

Amemchapa DOMINIKA CIBULKOVA kwa seti za moja kwa moja za 6-1 6-1 na sasa atakutana na SABINE LISICKI kwenye mechi ya nusu fainali.

CIBULKOVA alimuondosha mchezaji nambari moja kwa ubora duniani CAROLINE WOZNIACKI, lakini hapa kwa SHARAPOVA wala hakufurukuta.

Kwa hali inavyokwenda akiendelea hivi SHARAPOVA huenda akatwaa GRAND SLAM hii, na kwa kweli ndiye anayepewa nafasi kubwa.

= = =

Na mwisho ni VICTORIA AZARENKA ambaye naye amesonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali.

AZARENKA amemchapa TAMIRA PASZEK kwa seti 6-3 6-1.

Huyu naye ni moja ya wachezaji ambao wanapewa nafasi ya kufanya vizuri.

AZARENKA atacheza nusu fainali na PETRA KVITOVA.

= = =

Na sasa ni kandanda ambapo wachezaji TISA wa timu ya taifa ya MEXICO,wametimuliwa kwenye kambi ya timu ya taifa inayojiandaa na michuano ya COPA AMERIKA.

Wachezaji hawa si tu kwamba wametimuliwa, lakini pia wamelimwa tozo(faini)na wamefungiwa miezi SITA katika timu ya taifa.

Sababu ya adhabu hii ni utovu wa nidhamu walipokuwa kambini.

Wao waliona ni halali kuingiza wasichana ambao ni madada poa, ama kwa majina ya kisasa TAKE AWAY,kwenye vyumba vyao kinyume na taratibu.

Wale wasichana kwa vile walikuwa kibiashara zaidi wakawaibia vito vya dhamani wachezaji hawa wa MEKIKO, na fedha pia wakakomba.

Shirikisho la soka ya MEKIKO likaamua liwaarudishe nyumbani haraka sana ili wafaidi hicho wanachokitaka.

Sasa cha ajabu kuna habari hata bwana mdogo wa MAN.UNITED CHICHARITO naye yumo kwenye mkumbo, hizi ni tetesi,tutazifuatilia tuwajuze jamani,lakini kama itakuwa ni kweli, bado RYAN GIGGS wa MAN.UNITED ambaye kwa sasa yuko kwa wataalamu wakumtibu tabia ya kupenda ngono sanaaaa!

Aibu kweli MEKIKO.

==

Kombe la dunia la FIFA kwa wanawake, linaendelea UJERUMANI.

Na timu nyota duniani kwa soka la wanawake MAREKANI jana wameshuka dimbani wakicheza na KOREA ya KASKAZINI.

Ilikuwa kazi kweli hapa kwasababu WAKOREA ni wabishi kweli.

MAREKAN walisoteswa mpaka dakika ya 54 ndipo walipopata goli la kuongoza kwa kichwa kilichopigwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Kwenye dakika ya SABINI MAREKANI wakafunga goli la pili na wakatoka kifua mbele kwa magoli hayo MAWILI kwa BILA.

= =

SWEDEN nao walikuwa dimbani wakicheza na COLOMBIA.

Kwa kweli SWEDEN wanaonekana wamepikwa kwelikweli safari hii.

Lakini na wao walitolewa jasho na COLOMBIA.

Baada ya kusumbuka sana walifanikiwa kupata goli MOJA tu.

Kwa hiyo sasa katika kundi Che,MAREKANI wanaongoza wakiwa na pointi TATU na magoli MAWILI, SWEDEN wao wana pointi TATU na GOLI MOJA.

= =

Katika masumbwi bila shaka jumamosi hii kuna pambano la kufa mtu ulingoni kati VLADIMIR KLITSCHKO na DAVID HAYE,pambano la uzito wa juu la WBA.

Hapa patachimbika ama mtu atapigwa kirahisi sana.

Lakini sasa mwezi wa TISA mwaka huu mzee wa mapesa asiyepigika, FLOYD MAYWEATHER JUNIR atazichapa na

Alipokutana na wanahabari kwa mara ya kwanza FLOYD akaulizwa mbona una mkwepa MANNY PACQUIO?

Akawajibu uzuri.

Kwa kifupi tu FLOYD anasema hamwogopi MAN PACQUIO wala nani,yuko tayari ili mradi sharti lake la kutolewa damu apimwe kuhusu dawa za kuongeza nguvu kwanza.

= =

Unajua TUSKER PROJECT FAME imerejea na Tanzania tuna wawakilishi wawili, HEMED na MSECHU.

Hili ni shindano linalowakutanisha wale nyota wa miaka miwili iliyopita.

MSECHU aliyaaga mashindano haya mwaka jana kwa kilio kwa JULIANA, moja ya majaji wa shindano hili.

Sasa MSECHU amerudi tena na wimbo wa kwanza alioimba jumapili iliyopita bado anamuota JULIANA.

No comments:

Post a Comment