Wednesday, June 15, 2011

SIMBA kuondoka kesho
Klabu ya soka ya SIMBA itaondoka kesho kuelekea JAMHURI YA KIDEMOKRASI YA KONGO kuumana na DARING CLUB MOTEMA PEMBE,katika michuano Ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
TBC ilitembelea katika viwanja vya CHANG’OMBE na kukuta baadhi ya wachezaji wa SIMBA wakifanya mazoezi ya mwishomwisho, ambapo kocha MOSES BASENA amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri wakiwemo wachezaji tegemeo MOHAMED BANKA na EMMANUEL OKWI.
SIMBA ilicheza na DC MOTEMA PEMBE wiki moja iliyopita ambapo SIMBA iliibuka na ushindi wa bao MOJA kwa BILA dhidi ya wakongo hao .

======
BULEMBO kuchukua hatua za kisheria baada ya kuzuiwa kugombea Uongozi katika klabu ya VILLA SQUAD.

Mmoja wa wagombea walioenguliwa kugombea katika nafasi ya Uenyekiti katika klabu ya soka ya VILLA SQUAD , ABDALLAH MAJURA BULEMBO, amesema endapo shirikisho la soka hapa nchini TFF litaendelea na msimamo wake wa kumzuia kugombea atachukua hatua zaidi za kisheria ili kupata haki yake ya kimsingi.
BULEMBO amesema hatua ya kamati ya uchaguzi ya TFF kumuengua kugombea nafasi ya uongozi ndani ya klabu ya VILLA imeangalia zaidi maslahi ya baadae ya baadhi ya viongozi wa TFF wanaotaka kugombea nafasi ya URAIS wa shirikisho hilo katika siku za usoni(PAUSE).

Hapo jana shirikishop la soka nchini TFF , lilitoa msimamo wake juu ya hatua ya VILLA SQUAD kubadili baadhi ya vipengele vinavyohusu sifa za wagombea akiwemo BULEMBO ambavyo ni ukosefu wa vielelezo vya elimu inayotakiwa kama kigezo cha uongozi.

Klabu ya soka ya VILLA SQUAD iliagizwa na TFF kufanya uchaguzi baada ya kupanda katika ligi kuu soka ya VODACOM msimu ujao.

Wakati huo huo Uongozi wa juu wa TFF hapo kesho utakutana na kamati ya uchaguzi ya TFF pamoja na kamati ya uchaguzi ya VILLA SQUAD katika makao makuu ya shirikisho la soka hapa nchini .


=====

POULSEN afurahia vipaji COPA COCA COLA

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka KUMI na SABA KIM POULSEN amesema TANZANIA ni nchi iliyojaa vipaji na kinachotakiwa sasa ni kuwapa mwongozo wa mchezo wa soka.
Kocha POULSEN amesema maendeleo ya kukua kwa mchezo wa soka popote duniani hutegemea na misingi iliyowekwa katika kukuza soka la vijana

KIM POULSEN amesema kazi anayofanya hivi sasa katika michuano hiyo ni kuangalia wachezaji watakaofaa katika timu ya taifa ya vijana na ataweka hadharani majina yao muda utakapofika.

===

MICHUANO ya mpira wa Pete Taifa kuanza julai.

Chama cha Mchezo wa Netiboli nchini CHANETA, kimesema mashindano ya ligi ya taifa kwa mchezo huo yako pale pale na yanatarajiwa kufanyika jijini ARUSHA Julai TATU, Mwaka huu.

Katibu Msaidizi wa CHANETA ROSE MKISI amesema jumla ya timu sita zimethibitisha kushiriki katika michuano hiyo

MKISI amezitaka timu zote ISHIRINI zinazotarajiwa kushiriki michuano hiyo kuthibitisha Ushiriki wao ifikapo JUNI 20, Mwaka huu.

====

Mshindi wa MISS AFRICAN CROWN SCANDNAVIA awasili

MICHELLE JENG Mshindi wa taji la MISS AFRICA CROWN SCANDNAVIA amewasili nchini hii leo na kupokewa Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya HABARI, UTAMADUNI , na MICHEZO Bi ANGELA NGOWI.

Mara baada ya kutua hapa nchini MICHELLE JENG ambaye amekuwa Mrembo wa Kwanza kutoka TANZANIA kutwaa taji hilo atafanya shughuli za kijamii hususani kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, waathirika wa mabomu ya Gongolamboto,na watoto yatima na kuwapa misaada.

Baada ya shughuli hizo ambazo pia amezifanya katika nchi za KENYA NA UGANDA,JENG ataondoka nchini JULAI MBILI kuelekea nchini SWEDEN
==
AKUDO kutambulisha ALBUM mpya.
Bendi ya AKUDO IMPACT ya jijini DAR ES SALAAM itatambulisha ALBUM yake mpya ijulikanayo kama STORY NO CHANGE julai PILI mwaka huu katika ukumbi wa VATICAN CITY sinza jijini DAR ES SALAAM.

Mkurugenzi wa kampuni ya BIG ONE ENTERTAINMENT , ABOUBAKARY MWANAMBOKA ambayo ni waratibu wa onesho hilo amesema maandalizi yote yamekwishakamilika huku akiwataka wapenzi wa muziki wa dansi kujitokeza kwa wingi kushuhudia ALBUM hiyo mpya yenye jumla ya nyimbo SABA.

Nao baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo wakiongozwa na CHRISTIAN BELLA walitoa chachandu
===

No comments:

Post a Comment