Wednesday, June 15, 2011



NYAMLANI ATEULIWA MJUMBE CAFMakamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani iliyotumwa kwa Nyamlani jana, kikao kinachofuata cha Kamati hiyo kitafanyika Septemba 25 mwaka huu makao makuu ya shirikisho hilo jijini Cairo, Misri. Nyamlani ambaye kitaaluma ni mwanasheria anakuwa Mtanzania wa kwanza kuingia katika kamati hiyo. Pia ni kiongozi wa mpira wa miguu kwa muda mrefu akianzia Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Temeke (TEFA), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) sasa TFF.

====
TFF, VILLA SQUAD KUKUTANA KESHORais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kesho (Juni 16 mwaka huu) atakutana na wadau mbalimbali ili kuangalia mustakabali wa klabu ya Villa Squad ambayo msimu huu itashiriki Ligi Kuu ya Vodacom. Mkutano huo utafanyika makao makuu ya TFF kuanzia saa 9 kamili. Mbali ya Rais Tenga na Sekretarieti yake, wadau wengine katika mkutano huo ni wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya Villa Squad na viongozi wa klabu hiyo. Boniface WamburaOfisa Habari
=====

MICHUANO YA KOMBE LA KAGAMEShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekubali kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Kagame yanayoshirikisha klabu bingwa za nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Klabu 12 zitashiriki katika mashindano hayo yatakayofanyika nchini kuanzia Juni 25 hadi Julai 9 mwaka huu. Tumechukua uamuzi huu mgumu wa kuandaa mashindano haya kwa lengo la kuyaokoa. Awali mashindano hayo ambayo yalianzia nchini mwaka 1974 yalikuwa yafanyike Zanzibar ambayo ilijitoa. Baadaye yalihamishiwa Sudan ambapo napo yalikwama baada ya Serikali ya nchi hiyo kutokuwa tayari kuwa mwenyeji kwa sasa kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo tunaziomba kampuni mbalimbali nchini zijitokeze kwa ajili ya udhamini ambao utawezesha kufanyika kwa ufanisi. Jumatatu (Juni 20 mwaka huu) tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuelezea taratibu za mashindano hayo ikiwemo timu zitakazoshiriki. Tanzania kwa kuwa mwenyeji itaingiza timu mbili.

No comments:

Post a Comment