Monday, June 27, 2011

Serikali kurekebisha sera ya michezo

Serikali kurekebisha sera ya michezo

Wizara ya habari utamaduni vijana na michezo imekamilisha rasmu ya marekebisho ya sera ya maendeleo ya michezo nchini ambayo itatoa mwelekeo wa maendeleo ya michezo nchini.

Akijibu swali Bungeni mjini DODOMA hii Leo Naibu Waziri Wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo DKT FENELLA MKANGARA amesema serikali inaandaa mkakati maalumu wa uendeshaji wa michezo kuanzia ngazi za vijini ambao utashirikisha watoto,vijana na wazee.

DKT MKANGARA amasema Tanzania imekuwa ikifanya vyema katika mashindano mbalimbali ya kiamataifa hasa katika mchezo wa soka pamoja na sekta ya michezo kukubwa na matatizo mbalimbali ikiwepo ufinyu wa banjeti ya serikali katika kuendesha michezo nchini.

===

Michuano ya KAGAME kuendelea leo DSM

Michuano ya kuwania kombe la KAGAME hatua ya makundi inaendelea leo kwa michezo miwili ya kundi A kuchezwa katika uwamja wa taifa jijini DSM.

Mchezo wa kwanza utazikutanisha RED SEA ya ERETRIA dhidi ya ZANZIBAR OCEAN VIEW ambayo inaongoza katika kundi la A ikiwa na Alama Tatu ilizojikusanyia baada ya kushinda katika mchezo wa kwanza ilipoifunga ETINCELLES ya RWANDA mabao MATATU kwa MAWILI katika mchezo wa ufunguzi.

Mchezo mwingine unazikutanisha mabingwa wa Burundi Vital O’ ambayo itateremka dimbani dhidi ya ETINCELLES ya RWANDA, Vital O’ ina ALAMA MOJA hadi hivi sasa baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana na SIMBA katika mchezo wa ufunguzi wa kundi la A mchezo ulipingwa juzi kwenye uwanja wa Taifa.

Katika michezo iliyochezwa jana mechi za kundi la B, YANGA iligawana ALAMA na EL- Mereikh ya SUDAN baada ya kufunga mabao MAWILI kwa MAWILI wakati katika kundi la C mabingwa watetezi timu ya APR ya RWANDA imeanza vyema kutetea ubingwa wake baada ya kuichapa PORTS ya JIBUTI kwa mabao MANNE kwa BILA.

===

Mwanamuziki wa Jamaica akonga nyoyo za mashabiki DSM

Mwanamuziki nyota wa Jamaica -ELEPHANT MAN usiku wa kuamkia leo alikonga nyoyo za wapenzi wa burudani hapa nchini pale alipoongoza wanamuziki kutoka Jamaica , Kenya na Tanzania kutumbuiza katika tamasha la ufukweni la STRAIGHT MUSIC BEACH PARTY 2011 lililofanyika katika klabu ya MBALAMWEZI.(UPSOUND)

Wasanii kutoka nchi za Kenya na Tanzania kama vile Fid Q, Cpwa, Red San na P-Unit nao wakatumbuiza (UPSOUND)

==

Ecuador yaichapa Burkinabe kombe la dunia la vijana

Timu ya taifa ya ECUADOR imetinga katika hatua ya KUMI NA SITA BORA ya fainali ya kombe la FIFA la dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 baada ya kuifunga mabingwa wa Afika BURKINA FASO kwa mabao MAWILI kwa BILA nchini MEXICO.

Katika mchezo mwingine wa kundi la E mabingwa watetezi wa fainali ya kombe la dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 timu ya taifa ya UJERUMANI nayo imetinga katika hatua hiyo ya KUMI NA SITA BORA baada ya kuitandika PANAMA mabao MAWILI kwa BILA.

Matokeo mengine yanaonyesha timu ya taifa ya MAREKANI imelazimishwa sare ya bila kufungana na New Zealand na sasa itakutana na UJERUMANI katika hatua ya mtoano ya KUMI NA SITA BORA’

Katika mchezo mwingine, UZBEKISTAN imeibuka kidedea baada ya kuifunga JAMUHURI ya CZECH mabao MAWILI kwa MOJA.

LEO kutakuwa na mchezo mwingine wakati AUSTRALIA itavaa na DENMARK.

=====

Ujerumani Yaanza Vyema Kombe La Dunia Kwa Wanawake

Timu ya taifa ya wanawaka ya UJERUMANI imaanza vizuri fainali za kombe la dunia kwa wanawake baada ya kuichapa CANADA kwa mabao MAWILI kwa MOJA katika mchezo wa ufunguzi ulichezwa jana kwenye uwanja wa OLYMPIC nchini UJERUMANI.

Katika mchezo mwingine mabingwa wa Afrika timu ya taifa ya NIGERIA imeambulia kichapo baada ya kufungwa Bao moja kwa bila na UFARANSA.

Ratiba ya michuano hiyo inaonyesha hii leo JAPAN itamenyana na NEW ZEALAND katika mchezo wa kwanza wakati MEXICO itakutana na ENGLAND katika mchezo wa pili.

Kesho kutakuwa na michezo mingine miwili wakati COLOMBIA itakapocheza na SWEDEN, MAREKANI itacheza na KOREA KUSINI huku NORWAY ikipepetana na wawakilishi wengine wa Afrika GUINEA YA ikweta.

===

River Plate ya ARGETINA imeteremka DARAJA

Mabingwa mara 33 wa ligi kuu ya ARGETINA timu ya RIVER PLATE imeshuka daraja baada ya kudumu katika ligi kwa miaka 110.

Ilikuwa ni kilio kwa mashabiki wa RIVER PLATE baada ya FILIBI ya mwisho kupulizwa katika uwanja wa MONUMENTAL jana huku ubao wa magoli ukisomeka RIVER PLATE MOJA na BELGRANO

Mashabiki walishindwa kuvumilia na kuanza kurusha vyuma na mawe kwa wezao na kusababisha watu 25 kujeruhiwa wakiwepo askari SITA wa vikosi vya usalama.

Katika mchezo wa kwanza RIVER PLATE ilichapwa mabao MAWILI kwa BILA na BELGRANO na hivyo kushushwa daraja kwa jumla ya MABAO MATATU kwa MOJA.

RIVER PLATE sasa itacheza katika ligi ya NACIONAL B msimu ujao.

===

No comments:

Post a Comment