Thursday, November 25, 2010

michezo ya leo


CECAFA yaendelea kuwafua waamuzi
Waamuzi KUMI na TANO ambao watachezesha mashindano ya CECAFA TUSKER CHALENJI kwa mwaka huu wameanza kupatiwa mafunzo ambayo yatadumu kwa kipindi chote cha mashindano hayo yanayoanza jumamosi hii katika uwanja wa TAIFA jijini DSM.
Aliyekuwa mwamuzi wa soka nchini , OMAR ABDULKADIR amesema huo ni utaratibu waliojiwekea kila asubuhi kukutana ili kuondokana na makosa ya mara kwa mara mchezoni.
Timu ya ZANZIBAR HEROES na MALAWI zimepangwa kuwasili leo , huku timu nyingine zikitarajia kuwasili nchini kesho tayari kwa mashindano hayo yaliyopangwa kufunguliwa kwa mchezo kati ya KILIMANJARO STARS na ZAMBIA.
= =
BFT yawataka mabondia kupima ukimwi
Shirikihso la ngumi za ridhaa nchini BFT,limekiri kuwa sera ya kupima virusi vya ukimwi kwa mabondia wake ni nzuri ijapokuwa kwa sasa sera hiyo haifuatiliwi.
Katibu mkuu wa BFT, MAKORE MASHAGA ameaysema hayo wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa TBC kuhusiana na mabondia wengi kuwa katika hali ya hatari ya maambukizi kama suala hilo halitajidiliwa na kuwa na sera inayokubalika michezoni.
Amesema kuwa endapo watagundua kuna bondia ana tatizo hilo, watampa ushauri wa namna gani kuendeela na mchezo huo au ikibidi kumweleza kuachana kabisa na mchezo huo .
Katika hatua nyingine, MASHAGA amevitaka vyama vya michezo huo vya mikoa kuhakikisha uthibitsho wao wa mashindano ya taifa yatakayofanyika mwakani ambayo yatapata wachezaji wa timu ya taifa.
= =
BMT yaunda kamati kuendesha SHIMISETA
Baraza la michezo nchini BMT limeundwa kamati maalumu ya kuratibu michezo ya wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania.
baada ya kugundua kuwa viongozi waliokuwepo wamemaliza muda na wanaongoza shirikisho hilo kinyemela.
Afisa habari mwandamizi wa baraza la michezo (BMT) JOHN CHALUKULU amesema kwa sasa jukumu la kusimamia michezo litakuwa chini ya kamati teule na kuzitaka halmashauri kuendelea na maandalizi huku katibu mkuu wa kamati ya muda SALEH LUBANA akisema tayari wameandaa rasimu ya katiba na inatarajiwa kupitishwa na mkutano mkuu utakaofanyika kipindi cha michuano hiyo
Michuano hiyo itakayofanyika mjini MOROGORO itaanza kutimua vumbi NOVEMBA 27 na itafikia tamati yake desemba 5 mwaka huu.
= =
ZANZIBAR HEROES yaichapa DAR ALL STARS
Hapo jana katika Dimba la Amani huko kisiwani Zanzibar kulikuwa na Mechi ya kirafiki kati ya Zanzibar Heroes na Dar es salaam All Star mchezo uliopigwa majira ya usiku na hadi ya kipenga cha mwisho kinapulizwa znz Heroes ilitoka kifua mbele kwa kuichapa Dar All Star Goli moja kwa sifuri.
Ndani ya dakika ya kumi ya mchezo mchezaji wa ZNZ HEROES Ally Ahmed alichezewa vibaya ndani ya eneo la hatari na Meshark Abeir na kupelekea mwamuzi wa mchezo huo kutoa penati kwa znz heroes na kupigwa na Hamis Ncha lakini mlinda mlango wa Dar all star Ivo Mapunda akaipangua penati hiyo kisha ktk piga nikupige mchezaji Suleiman Kassim wa znz heroes akapiga kichwa na mojakwa moja kikaingia kimyani na kuiyandikia znz goli la kuongoza hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa znz heroea 1 Dar All Star 0.

Hii ni mechi ya marudiano kati ya znz heroes na Dar All Star mechi ya kwanza walitoka bila ya kufungana huko jijini Dar na mechi hizi imewajenga vizuri znz heroes ktk kujiandaa na michuano ya challenge cup itakayofanyika huko Dar.
= =
Music Dance competition yazinduliwa Dar
Shindano la kusaka wanamuziki wadansi chipukizi linalojulikana kama MUSIC DANCE COMPETITION limetambulisha leo jijini DSM, ambapo washindi watakaopatikana watazawadiwa zawadi mbali mbali.

Akizungumza jijini DSM,mratibu SULEIMAN MATHEW pamoja na mmmoja wasanii muziki wa dansi EMANUEL FIRI maarufu kama BOB KISSA wamesema kuwa shindano hilo litasaidia kukuza vijapi vya muziki wa dansi.

MATHEW amesema kuwa vikundi mbali mbali vitashindwanishwa na baadaye kupata watakaoingia fainali ambayo itakuwa mwezi wa tatu mwakani .

Na hawa ni moja ya wasaniii ambao wameshaunad kundi lao ambalo litaingia katika shindano hilo na hapa wanatoa burudani ya mwimbo kutoka bendi ya MSONDO NGOMA.
==
Mwanamuziki GYPTIAN awasili nchini
Nyota wa muziki wa Raggae na Dancehall toka Jamaica, Windel Beneto Edwards maarufu kama Gyptian, amewasili nchini jana usiku na kuwaomba wanachuo na wapenzi wa muziki kujitokeza kwa wingi kesho katika tamasha la muziki lijulikanalo kama Str8Muzik Festival Inter-College Special 2010.

Akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, msanii huyo amewataka mashabiki kufurika kwa wingi kuona burudani aliyonayo na hapa Gyptian mwenyewe akatoa kionjo cha burudani.

Tamasha hilo litafanyika viwanja vya TTCL Kijitonyama jijini DSM
= =
Wachezaji wa ARSENAL CESC na EBOUE nje baada ya kuumia
Matumaini ya Arsenal kusonga mbele hatua ya timu 16 ya kuwania Ubingwa wa soka wa Ulaya, yalizidi kuingia mashakani baaday wachezaji wake wakutumainiwa, nahodha Cesc Fabregas na Emmanuel Eboue kuumia wakati wa mchezo .
Nahodha Fabregas aliumia misuli ya paja, wakati Eboue ameumia goti.
Kwa mujibu wa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger Huenda ikamchukua wiki mbili au tatu Fabregas kupona. Aliongeza Nilibahatisha kumchezesha na sasa mambo yameharibika
Wenger alimchagua Fabregas kucheza licha ya kiungo huyo kutokuwa katika hali yake ya kawaida. Amesema ni tatizo la msuli wa paja katika mguu mwengine, ni vigumu sana kutabiri kwa muda gani Cesc hatacheza.
Arsenal ilikuwa inahitaji pointi kuweza kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele hatua ya mtoano, lakini wakazembea na kuruhusu mabao mawili yaliyofungwa na Matheus dakika ya 83 na jingine kutoka kwa Mbrazil huyo katika dakika za nyongeza kwenye uwanja wa Estadio Municipal.

===.
SERENA kutoshiri mashindano ya wazi ya AUSTRALIAN.

Mchezaji wa tenesi kwa upande wa wanawake SERENA WILLAMS hatashiriki mashindano ya wazi ya AUSTRALIAN kutokana na kusumbuliwa na goti .

Mchezaji huyo ambaye anashikiria nafasi nzuri kwa bora DUNIANI katika mchezo wa tenesi amesema hatashiriki mashindano hayo bado anaendelea kutibu goti lake.

Mpaka sasa WILLIAMS anaendelea kuuguza goti lake huku akiendelea na mazoezi mapesi .

Mahindano ya tenesi ya AUSTRALIAN yanategemewa kuanza janualy 17 hadi 30 mwakani.

===.

Nadal ambwaga Djokovic
Mchezaji RAFAEL NADAL amejiweka katika nafazi nzuri ya kufuzu kucheza hatua ya mtoano ya mashindano ya tennis ya ATP WORLD TOUR baada ya kuibuka na ushindi wa seti mbili dhidi ya NOVAK DJOKOVIC.

Baada ya seti ya kwanza kuanza DJOKOVIC alipata matatizo ya jicho na hivyo ilimlazimu atoke nje ya uwanja na baada ya kurudi uwanjani hakuwa mchezaji yule yule wa mara ya kwanza tena.

NADAL alimshinda DJOKOVIC kwa seti mbili zenye matokeo ya 7-5 6-2 katika muda wa saa moja na dakika 51 na hivyo kuongoza kundi A kwa kuwa ameshinda michezo miwili, wakati DJOKOVIC yeye yupo sawa na TOMAS BEDYCH kwa ushindi wa mchezo mmoja baada ya BEDRYCH kushinda katika mchezo wake uliochezwa jana mchana dhidi ya ANDY RODDICK.
= = = = =

No comments:

Post a Comment