Thursday, November 4, 2010

Twiga yafungwa na Mali

Twiga stars yafungwa na Mali mabao matatu kwa mawili na kuyaanga mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake yanayofanyika Afrika kusini.

Twiga Stars imesalia na mchezo mmoja kwa kukamilisha ratiba dhidi ya Nigeria mchezo ambao utachezwa Novemba saba.

Katika mchezo wa kwanza katika kundia la A Twiga ililala mbele ya wenyeji Banyana banayana baada ya kufungwa mabao mawli kwa moja.

===

Timu ya taifa ya wanawake ya Afrika Kusini BANYANA BANYANA imefungwa magoli mawili kwa moja na wanawake wa Nigeria, Super Falcons katika mchezo wa kundi A uliopigwa katika dimba la Sinaba mjini Daveyton.

Magoli ya Nigeria yamewekwa kimiani na Perpetua Nkwocha dakika ya 14 na dakika nane baadae Nkwocha aliongeza goli la pili kwa kichwa.

Banyana Banyana walifuta machozi kwa goli la Janine van Wyk aliyepiga mpira wa adhabu ndogo uliojaa moja kwa moja wavuni na kumshinda mlinga mlango wa Nigeria Uzoaru Dede.

Baada ya mchezo, kocha wa Banyana Banyana Augustine Makalakalane amesema vijana wake wameonesha kiwango kizuri na ana faraja kuwa watafika mbali licha ya kichapo hicho na wanataraji kufanya vema mchezo ujao dhidi ya Mali

Katika michezo yao ya kwanza Banyana Banyana iliifunga Tanzania magoli mawili kwa moja huku Nigeria ikitoa kichapo kwa Mali cha magoli matano kwa bila

No comments:

Post a Comment