Tuesday, November 2, 2010

Michezo ya leo

Shirikisho la soka hapa nchini TFF limewataka wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake TWIGA STARS kucheza kwa bidii ili wapate ushindi katika michezo miwili iliyobaki ya fainali za SABA za kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya MALI na NIGERIA ili waweze kuvuka kwenda mzunguko wa pili.

Kaimu katibu mkuu wa TFF -SUNDAY KAYUNI anasema matokeo ya TWIGA STARS kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya wenyeji BANYANA BANYANA kusiwavunje moyo ila watumie matokeo hayo kurekebisha makosa yaliyojitokeza ili wafanye vyema katika mechi mbili zijazo.

TWIGA STARS inateremka dimbani dhidi ya MALI -ALHAMISI NOVEMBA NNE kabla ya kuivaa NIGERIA –JUMAPILI ya NOVEMBA SABA.

NIGERIA inaongoza kundi la A ikiwa na alama TATU sawa na wenyeji BANYANA BANYANA lakini wakitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa baada ya hapo jana NIGERIA kuwachapa kinadada wa MALI magoli MATANO kwa BILA shukrani kwao zikimuendea PERPETUA NKWOCHA aliyefunga magoli matatu katika mchezo huo.

TWIGA STARS wapo katika nafasi ya pili kwenye kundi hilo huku MALI wakikamata mkia.

Na katika mechi za leo za kundi Be- bingwa mtetezi wa michuano hii EQUTORIAL GUINEA wamelazimishwa sare ya magoli MAWILI kwa MAWILI na CAMEROON huku kinadada wa ALGERIA waki…….. na GHANA.

Kesho ni mapunziko na fainali hizi zinaendelea tena alhamisi ambapo wenyeji BANYANA BANYANA dhidi ya NIGERIA na TWIGA STARS dhidi ya MALI.

= == =

Shirikisho la soka hapa nchini-TFF limetangaza kuanza kwa kipindi cha usajili cha dirisha dogo kwa wachezaji wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara kuanzia jana NOVEMBA MOSI na kumalizika NOVEMBA 30 mwaka huu.

Akizungumza na mwandishi wa TBC jijini DSM, Kaimu katibu mkuu wa TFF -SUNDAY KAYUNI amevitaka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara kutumia muda huu kusajili wachezaji mahiri ili kuimarisha timu zao.

KAYUNI anasema dirisha dogo likitumika vyema litasaidia vilabu husika kusajili wachezaji wazuri ili viweze kufanya vyema katika ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa.

===

SAID SALUMU akabidhiwa tiketi ya kushuhudia mchezo kati ya ARSENAL na EVERTON.

SAID SALUMU RASHID amekabidhiwa tiketi yake na benki ya BARCLAYS itakayomwezesha kushuhudia mchezo wa kukata na shoka wa ligi kuu ya ENGLAND kati ya ARSENAL dhidi ya EVERTON FEBRUARY mosi mwakani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi tiketi hiyo mkuu wa uzalishaji wa BANKI ya BARCLAYS -TANZANIA RAY KAIJAGE amewataka wateja wa benki hiyo kuendelea kutumia huduma mbalimbali za banki hiyo ili waweze kushinda tiketi ya kushuhudia ligi kuu ya ENGLAND na zawadi nyingine kemkem.

Kwa upande wake mshindi huyo SAID SALUMU RASHID anasema hakutegemea katika maisha yake kama ageweza kupata nafasi ya kushuhudia mechi kali kama hiyo ya ARSENAL na EVERTON na kuwataka wateja wengine kujaribu bahati zao kwani wanaweza kuibuka washindi.

Kwa mujibu wa KAIJAGE bado benki ya BARCLAYS ambao ndio wadhamini wakuu wa ligi kuu ya ENGLAND wanatoa tiketi zingine KUMI NA MOJA za kwenda kushuhudia michezo mbalimbali ya ligi kuu ya ENGLAND inayoendelea.

= == =

Katika ligi ya mabingwa barani ulaya leo inaendelea katika viwanja mbalimbali barani humo.

FC COPENHAGEN ya DENMARK itakua nyumbani kuikabili FC BARCELONA.

Kocha wa fc COPENHAGEN anasema watafanya kila liwezekanalo kumnyamazisha nyota wa BARCA- LIONEL MESSI ili asizunguke katikati ya viungo wake.

TOTTENHAM HOTSPURS wao watakuwa katika dimba lao la WHITE HART LANE kuwakabili mabingwa watetezi INTER MILAN katika mchezo unaotazamiwa kuwa mgumu na wakusisimua.

MANCHESTER UNITED imesafiri hadi nchini UTURUKI kuikabili BURSASPOR, ambapo nahodha wa timu hiyo RIO FERDINAND pamoja na wachezaji wengine JOHNNY EVANS, MICHAEL OWEN,WAYNE ROONEY na FEDERICO MACHEDA wote wameikosa safari hiyo ya UTURUKI.

Mchezo mwingine ni kati ya VALENCIA ya HISPANIA itakayokuwa nyumbani kuvaana na RANGERS ya SCOTLAND.

RUBIN KAZAN nayo itakua ikiikaribisha PANATHINAIKOS ya UGIRIKI, wakati BENFICA ya URENO ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya OLYMPIC LYON ya UFARANSA, huku SCHALKE 04 ya UJERUMANI Imesafiri hadi nchini ISRAEL kukabili HAPOEL TEL AVIV ya huko.

= = = = = = = =

Meneja wa klabu ya TOTTENHAM HOTSPURS -HARRY REDKNAPP ametishia kuacha kufanya mahojiano na waandishi wa habari endapo ataadhibiwa na chama cha soka cha ENGLAND -FA, kutokana na maelezo yake kuwa goli la pili la MANCHESTER UNITED lililofungwa na LUIS NANI wakati wa mchezo wa ligi kuu ya ENGLAND dhidi ya timu hizo mbili lilikua ni kichekesho na kashfa.

Chama cha soka cha ENGLAND-FA leo kinatoa maamuzi juu ya kumuadhibu ama la kocha REDKNAPP kwa matamshi hayo.

Mechi hiyo ilimalizika kwa matokoe ya MANCHESTER UNITED kuilaza SPURS magoli 2-0.

REDNKAPP anasema anawatakia kila la heri FA iwapo wanataka kuyafanya makuu yale aliyoyasema na kuongeza kuwa hata yeye naye atazua masuala makuu pia.

REDKNAPP ameongeza kuwa kama ataadhibiwa na FA basi waandishi wa habari wasifikirie kuwa atakuja kuonekana tena kwenye Television baada ya mchezo unaoihusu timu hiyo.

Wakati MANCHESTER UNITED ikiongoza kwa goli moja kwa bila zikisalia dakika sita mpira kumalizika, NANI aliutumbukiza mpira kimiani baada ya kipa wa SPURS -HUERELHO GOMES kuweka mpira nchini akidhani alikua ameruhusiwa na mwamuzi kupiga mpira wa adhabu ndogo kufuatia NANI kuunawa mpira huo.

= = = = = = = =

Na kocha wa BLACKPOOL -IAN HOLLOWAY amefurahishwa na ushindi wa jana wa kwanza wa ligi kuu ya ENGLAND katika uwanja wao wa nyumbani.

THE SEASIDERS waliibuka na ushindi wa magoli MAWILI kwa MOJA dhidi ya WEST BROMWICH ALBION waliokuwa pungufu mchezaji mmoja, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa BLOOMFIELD ROAD.

BLACKPOOL ilianza kujipatia goli la kuongoza kwa mkwaju wa penati shukrani zimwendee CHARLIE ADAM aliyetumbukiza kimiani mkwaju wa penati baada ya PABLO IBANEZ kumfanyia madhambi DJ CAMPBELL.

IBANEZ baadaye alioneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya LUKE VARNEY kwa kumrukia miguu miwili.

Alikua LUKE VARNEY aliyehitimisha kitabu cha magoli cha BLACKPOOL, lakini WESTBROMWICH ALBION iliendelea kushambulia na juhudi zao kuzaa matunda kwa kupata goli la kufutia machozi kupitia kwa YUSUF MULUMBU.

= = = = = == =

No comments:

Post a Comment