Tuesday, November 9, 2010

TFF yang'ang'ana na Kaseja

Shirikisho la soka nchini TFF kupitia kwa kaimu katibu mkuu wake SUNDAY KAYUNI limetoa ufafanuzi kuhusu utata wa suala la kufungiwa kipa wa Simba Juma Kaseja kwa kusema adhabu ya mchezaji huyo ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS iko pale pale ingawa maelezo ya awali yalikosewa.

Kayuni amedai kuwa ni kweli Kaseja alipeana mikono na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mechi kati ya simba na Yanga iliyofanyika mwezi uliopita jijini Mwanza lakini alikwepa kupeana mikono na wachezaji wa Yanga.

Katika maelezo ya awali TFF ilidai kuwa Kaseja alikwepa kupeana mikono na Mkuu wa Mkoa wa Mawanza Abbass Kandoro jambo ambalo lilikanushwa kwa picha na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.



No comments:

Post a Comment