Thursday, November 4, 2010

Michezo ya leo

Simba kujenga uwanja wake wa kisasa

KLABU ya SIMBA imeanza mchakato wa kuwa na kiwanja chake ambapo katika taratibu za awali kamati ya utendaji ya klabu hiyo imeamu kufanya mazungumzo na kampuni ya ujenzi wa uwanja ya GIDAS kutoka nchini UTURUKI.

Akizungumza na waandishi wa habari , Mwenyekiti wa klabu hiyo , ISMAIL ADEN RAGE amesema ujenzi wa kiwanja hicho unatarajiwa kukamilika kipindi cha miaka miwili na kitakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki ELFU THELATHINI.

Uwanja huo wa SIMBA ambao RAGE ameutaja kama ni uwanja wa kisasa utajengwa katika maeneo ya BUNJU na utakuwa na maduka makubwa.

Katika hatua nyingine, klabu ya SIMBA imempa madaraka zaidi kocha wake PATRICK PHIRI ambapo yeye atakuwa mkuu wa benchi la ufundi la klabu ya SIMBA.

==

VODACOM yatoa MILIONI 17 kwa mchezo wa Baiskeli

KAMPUNI ya simu za mkononi nchini VODACOM imetoa shilingi MILIONI 17.4 kama zawadi kwa washindi tofauti katika mashindano ya wazi ya mchezo huo yaliyopangwa kufanyika kuanzia NOVEMBA 12 hadi 13 jijini MWANZA.

Afisa mdhamini na matukio wa kampuni hiyo, RUKIA MTINGWA amesema kampuni yake imeamua kutoa msaada huo ili kufanikisha mashindano hayo ambayo pia yatakuwa ni chachu ya kupata timu ya taifa.

Katika mashindano hayo , upande wa wanaume watakimbia kwa kilometa 196 ambapo zawadi ya mshindi wa kwanza itakuwa ni shilingi milioni MOJA na NUSU , mshindi wa pili MILIONI MOJA na mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi laki SABA.

Upande wa wanawake watakimbia kwa mita 80 ambapo mshindi wa kwanza atapata milioni MOJA, mshindi wa pili laki nane na watatu atajipatia laki sita.

Aidha, kutakuwa na mbio za kilometa KUMI ambazo zitawashirikisha watu wenye ulemavu ambapo zawadi zao ni shilingi laki NNE.

==

Tamasha la SWAHILI FASHION WEEK laanza jijini

Wakati tamasha la wabunifu wa mavazi maarufu SWAHILI FASHION SHOW likiwa limeanza katika viwanja vya KARIMJEE jijini DSM wabunifu hao wameelezea changamoto mbalimbali zitakazotokana na onesho hilo

Mbunifu wa Tanzania Ailinda Sawe, John Kavele na Samira Jeizan kutoka Kenya wamesema onesho hilo linatoa fursa kwa wabunifu wachanga kujitangaza kimataifa hatua itakayowainua kiuchumi.

Wabunifu hao kutoka nchi za Afrika mahsraiki wataonesha mavazi mbalimbali ya asili yanayovalia na jamii za Afrika mashariki ambayo pia yanatokana na mali ghafi za Afrika, litafikia kilele chake siku ya Jumapili.

==

Heskey nje kutoka na kuumia goti

MSHAMBULIAJI wa Aston Villa Emile Heskey atakuwa nje ya dimba kwa wiki kadhaa kutoka na kuumia goti .

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32- mchezaji wa zamani wa ENGLAND ambaye amefunga magoli mnne katika msimu huu anatafanyiwa upasuaji wa goti lake.

Heskey amekuwa akionyesha kiwango kizuri katika timu yake baada ya mchezaji Gerard Houllier, kuhama timu hiyo ya ASTON VILLA.

Baada ya mchezaji huyo kuumia sasa amebakia mchezaji mmoja mkongwe katika klabu ya ASTON VILLA John Carew ambaye atacheza siku ya jumamosi.

Kuumia kwa Heskey kumekuja baada wakati mchezaji wa kimatifa wa ENGLAND Gabriel Agbonlahor anaendelea kuuguza maumivu yake.

Heskey alimumia wakati wa mazoezi tore.

===

Wachezaji wa Ghana hawajalipwa bonasi

Mafanikio ya kufika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia yamezua mzozo unaohusu malipo ya ziada waliyoahidiwa wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana.

Hakuna mchezaji hata mmoja aliyelipwa dola 63,000 alizoahidiwa kila mchezaji wa Black Stars kwa sababu taratibu za malipo katika benki ya Ghana.

Benki Kuu ya Ghana inasisitiza kuwalipa wachezaji hao kwa kuwawekea pesa katika akaunti zao.

Lakini wachezaji wamekuja juu kwa vile wanataka walipwe fedha taslimu mkononi kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Taarifa ya Benki Kuu ya Ghana imesema benki hiyo hufanya kazi zake za kuwahudumia wateja kwa taratibu zilizopo na kutofanya hivyo ni kwenda kinyume na shughuli za uendeshaji benki ambapo wakiwalipa fedha taslimu zinaweza kuzidi kwa zaidi ya dola elfu kumi.

Benki Kuu ya Ghana imeiambia Wizara ya Vijana na Michezo watawalipa wachezaji wa Black Stars kwa fedha za kigeni kupitia akaunti zao au kwa hundi.

Mzozo huo wa malipo ya wachezaji uligubika pambano la kufuzu katika michezo ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Sudan.

Tarehe ya mwisho ya kulipwa wachezaji hao ilikuwa 15 mwezi wa Oktoba na hakuna senti hata moja waliyolipwa wachezaji hao.

===

MOURINHO akerwa na sare.

Kocha wa timu ya REAL MADRID Jose Mourinho amefurahiswa na kikosi chake kwa kutofungwa na timu yoyote ile katika michuano ya ligi ya mabingwa lakini hakufurahia sare ya kufungana mbili mbili na timu ya AC MILAN.

MOURINHO amesema kama kikosi chake kingecheza vizuri katika kipindi cha pili wangeibuka na ushindi..

Amesema matokeo ya sare hajamfurahisha kwa sababu timu hiyo ilikuwa na nafasi nyingi za kufunga lakini imeshindw akutumia nafasi hizo..

Katika mchezo huo REAL MADRID walianza vizuri wakafunga goli kupitia kwa GONZALO HIGUAN, kazi nzuri ya DI MARIA.

Kipindi cha pili AC MILAN wakafanya mabadiliko wakamwingiza mkongwe PHILIPPO INZAGI PEOPLE, ambaye akabadilisha hali ya mchezo, akasawazisha goli, kazi nzuri ikifanywa na ZLATAN IBRAHIMOVIC.

PHILIP INZAGI akaendelea kuwaonesha REAL MADRID kwamba yeye si mzee, akapachika goli la pili.

Kimuhemuhe kikamuingia kocha JOSE MOURIHNO,lakini vijana wake wakatulia, na kijana asiyetajwa sana pale BERNABEAU PETRO LEON akampiga doba mlinda mlango wa AC MILAN na kusawazisha goli hilo.

REAL MADRID wamejikatia tiketi ya kucheza hatua ya mtoano.

==

No comments:

Post a Comment