Monday, December 6, 2010

Michezo leo

TASWA FC dimbani dhidi ya waandishi wa michezo wa Afrika Mashsriki.

Timu ya waandishi wa habari za michezo ya Tanzania,TASWA FC na ile ya waandishi wa habari wa za michezo wa kimataifa wanoripoti mashindano ya CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP zinateremka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye uwanja wa GYKHANA jijini DSM jioni ya leo.

Mshidi katika mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kali na ya kusisimua atajinyakulia kitita cha shilingi lake NANE huku mshindi wa pili akiondoka na shilingi laki NNE.

Manahodha wa timu zote mbili MAJUTO OMARI wa TASWA FC na FRED AROCHO wa timu ya waandishi wa habari wa kimataifa wote wametamba timu zao kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Mchezo huo umedhaminiwa na wadhamini wa mashindano ya CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP wakishirikiana na MARADI wa kampeni ya kutokomeza Malaria,MALARIA HAIKUBALIKI.

== ==

Robo fainali ya Cecafa Tusker Challenge Cup kuanza kesho

Michezo ya kwanza ya Robo fainali ya Mashindano ya CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP inaanza kesho kwenye dimba la taifa jijini DSM hiyo kesho.

Katika mchezo wa kwanza utakaochezwa majira ya saa nane mchana IVORY COAST itamenyana na MALAWI wakati mchezo wa pili utazikutanisha ETHIOPIA na ZAMBIA.

Michezo ya Robo fainali ya pili itachezwa siku ya jumatano wakati ZANZIBAR HEROES itakapo teremka dimbani kumenyana na UGANDA huku KILIMANJARO STARS ikiikabili RWANDA.

Katika michezo iliyochezwa jana mabingwa watetezi UGANDA walitoka kifua mbele baada ya kuichapa Kenya kwa mabao MAWILI kwa BILA huku timu alikwa katika michuano hiyo IVORY COAST ikiichapa SUDAN kwa magoli MATATU kwa BILA.

= == = === = =

Sunderland yachanua ligi kuu England

Kimataifa,ligi kuu ya ENLANG imeendelea jana kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja viwili tofauti.

SUNDERLAND walitoka kifua mbele kwa ushindi wa BAO MOJA kwa BILA dhidi ya WEST HAM na kupaa hadi katika nafasi ya SABA wakiwa na ALAMA 23 huku wakiwaacha wapinzania wao WEST HAM kuendelea kushika mkia katika ligi hiyo.

Katika mchezo mwingine WEST BROM wakiwa katika dimba lao la nyumbani wamechomoza na ushindi wa mabao matuta kwa MOJA dhidi ya NEWCASTLE na kushika nafasi ya NANE ikiwa na Alama 22.

Msimamo wa ligi hiyo unaonyesha ARSENAL inaongoza ikiwa na Alama 32 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao MAWILI kwa MOJA dhidi ya FULHAM siku ya jumamosi.

MANCHESTER UNITED,wao wanashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na ALAMA 31 licha ya mchezo wao dhidi ya BLACKPOOL kuahirishwa kutokana na theluji.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo CHELSEA wao wanashika nafasi ya tatu baada ya juzi kulazimishwa sare ya kufungana bao moja kwa moja na EVERTON.

Leo kuatakuwa na mchezo mmoja wakati LIVERPOOL watakapo wakaribisha ASTON VILLA katika uwanja wake wa nyumbani wa ARNFIELD.

=====

DORTMUND yajikita kileleni Bundesliga

Huko UJERUMANI vinawa wa ligi ya BUNDESLIGA BORUSSIA DORTMUND wameendelea kujikita kileleni kwa pengo la Alama kumi baada ya hiyo jana kuchomoza na ushindi wa mabao MAWILI kwa BILA dhidi ya NUREMBERG.

Mabao ya DORTMUND yakipachikwa wavuni na Mats HUMMELS na ROBERT LEWANDOWSKI

Mahasimu wao ambao wanashika nafasi ya pili timu ya MAINZ yenyewe ilijikuta ikipata kichapo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa FRANKFURT na hiyo kuifanya DORTMUND iendelee kutamba kileleni.

Katika mchezo mwingine uliochezwa jana BAYER LEVERKUSEN ilibuka na ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya COLOGNE.

Msimamo wa ligi hiyo unaonyesha BORUSSIA DORTMUND inaongoza ikiwa na ALAMA 40, MAINZ wapo katika nafasi ya pili wakiwa na ALAMA 30 wakati BAYER LEVERKUSEN inashika nafasi ya tatu ikiwa na ALAMA 29

====

Villarreal na Espanyol zatamba LA LIGA

Huko HISPANIA katika ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama LA LIGA VILLARREAL na ESPANYOL zimeibuka kidedea hiyo jana na kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo.

VILLARREAL wameibuka na ushindi wa bao MOJA kwa BILA dhidi ya SEVILLA na kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa katika uwanja wake wa nyumbani.

ESPANYOL wao wakaibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya SPORTING GIJON.

Mabingwa watetezi BARCELONA wao wanaongoza ligi hiyo wakiwa na 37 baada ya siku ya jumamosi kuibuka na ushindi wa mbao matatu kwa bila dhidi ya OSASUNA.

Mahasimu wao katika LA LIGA REAL MADRID bado wanashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na ALAMA 35 baada ya kuichapa VALENCIA kwa mabao mawili kwa bila.

VILLARREAL wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 30 wakati ESPANYOL wapo katika nafasi ya nne wakiwa na 28 huku VALENCIA wakiwa katika nafasi ya tano wakiwa na alama 24.

====

Seriba mabingwa kombe la DAVIS

SERBIA imenyakua ubingwa wa tenisi wa DAVIS CUP baada ya kuifunga UFARANSA katika fainali iliyochezwa jana mjini BELGRADE.

Shujaa wa SERBIA alikua ni VICTOR TROICKI ambaye alimfunga Mfaransa MICHAEL LLODRA wa UFARANSA kwa seti tatu kwa bila ya ushindi wa 6-2 6-2 6-3.

Katika mchezo wa mwanzo mchezaji wa tennis namba tatu duniani NOVAK DJOKOVIC aliweza kuirudisha SERBIA sawa kwa ushindi wa 6-2 6-2 6-4 dhidi ya GAEL MONFILS wa UFARANSA.

SERBIA ilianza mashindano hayo ya DAVIS kwa mara ya kwanza mwaka 1995 na wote DJOKOVIC na OBRADOVIC walisema kabla ya fainali kuwa ushindi wa taji hilo utailetea SERBIA mafanikio makubwa katika historia ya michezo ya nchi hiyo.

= = = == = = = = =

.

Ndoto za mchezaji nambari mbili kwa ubora wa GOFU duniani TIGER WOODS kuibuka na ubingwa wa kwanza zimezimwa na GRAEME McDOWELL hiyo jana baada ya GRAEME McDOWELL kuibuka na ubingwa wa dunia wa CHEVRON kufuatia mchezo mkali wa marudiano.

McDOWELL aliianza siku akiwa shot nne nyuma lakini alifanikiwa kuweka mambo sawa na kwenda sawa na TIGER WOODS katika hatua ya mwisho hatimaye kuweza kuibuka na ushindi.

Pamoja na WOODS kushindwa katika hatua ya mwisho katika mashinmdano hayo lakini dalili zinaonyesha kwamba ameanza kurejea katika kiwango chake cha uchezaji wa GOFU.

Kwa upande mwingine McDOWELL huu nishindi wake wa nne mwaka huu ikiwa ni pamoja na kunyakua mashindano ya wazi ya golf yaMAREKANI na taji la RYDER ambalo ni taji la kukumbukwa zaidi kwa mwaka mzima kwa McDOWELL.

== = = == = =

No comments:

Post a Comment