Tuesday, December 14, 2010

MICHEZO YA LEO


TFF yamteua JAMHURI KIWELO kufundiasha SERENGETI BOYS
Shirikisho la soka nchini TFF limemteua kocha wa zamani wa SIMBA,JAMHURI KIWELO maarufu JULIO kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, SERENGETI BOYS kinacho jiandaa kushiriki michuano ya CECAFA yatakayoshirikisha nchi za TANZANIA, KENYA na wenyeji RWANDA yatakayoanza kutimua vumbi DECEMBA 17 jijini KINGALI.
Akizungumza jijini DSM kaimu katibu mkuu wa TFF SUNDAY KAYUNI amesema SERENGETI BOYS itacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya wenyeji RWANDA Desemba 17 kabla ya kumaliza na KENYA DESEMBA 22.
KAYUNI pia amewaalika wenyeviti na makatibu wa vilibu vya ligi kuu kufanya mkutano siku ya jumamosi kwa ajili ya maadalizi ya michuano ya UHAI CUP ambayo yanashirikisha timu za vijana chini ya umri wa miaka 20 ya vilabu vya ligi kuu Tanzania bara ili kupanga tarehe ya kuanza kwa michuano hiyo.
Wakati huo huo KAYUNI amevitangaza vilabu TISA vitakavyoshiriki fainali ya ligi daraja la kwanza ambayo fainali zake zitanza kutimua vumbi January 15 mwakani.
Vilabu hiyo kutoka kundi A ni TEMEKE UNITED,VILLA SQUAD, na MORO UNITED,kutoka kundi B ni TANZANIA PRISONS,COASTAL UNION na MORAN FC wakati kutoka kundi C ni JKT OLJORO FC,POLISI MORO,RHINO RANGERS.
==
WANAHABARI WATOA MAONI JUU YA WAJIRIWA TFF
Baada ya kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa TFF ANGETILE ASEAH pamoja na msemaji BONIFACE WAMBURA baadhi ya waandihsi wa habari wamewataka viongozi hao kutenda kazi yao kwa umakini ili kuwapa imani wapenzi wa soka hapa nchini.
Wakizungumza Jijini DSM ALEX LUAMBANO, ZENA CHANDE pamoja na msemaji wa SIMBA CLIFORD NDIMBO wamesema wanaimani na OSEAH pamoja na WAMBURA kwa kuwa walikuwa wafanyakazi waadilifu katika ofisi zao.
OSEAH ameshika nafasi ya ukatibu mkuu baada ya aliyekuwakuu wa TFF FREDRICK MWAKALEBELA kumaliza muda wake huku WAMBURA akishika nafasi ya KAIJAGE ambaye alikuwa msemaji .
Lakini baada ya kuchaguliwa OSEAH amesema anakabiliwa na changamoto nyingi ambazo imejipanga kukabiliana nazo ili kuhakikisha kazi yake anaifanya vizuri.
====
simba na Yanga waunganisha nguvu mashindano ya kimataifa
Vilabu vikongwe vya soka hapa nchini SIMBA na YANGA vimeamua kuunganisha nguvu zao katika michuano ya kimataifa ili kuhakikisha vilabu hivyo vinafanya vyema katika mashindano ya kimataifa.
Wakizunguza kwa pamoja maafisa habari wa vilabu hivyo CLIFFORD MARIO NDIMBO kwa upande wa SIMBA ,na LUIS SENDEU wa YANGA wamesema wameamua kuunganisha nguvu zao kwa vile wanakabiliwa na michuano ya vilabu bingwa barani Afrika na kombe la shirikisho.
NDIMBO na SENDEU wamesema hivi sasa vilabu hivyo vimeweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha mashabiki wao wanaipa nguvu timu ya taifa ama timu yoyote inayoliwakilisha taifa uwanjani bila ya kujali itikadi za mashabiki hao ,hata kama mojawapo ya timu hiyo itakuwa SIMBA ama YANGA.
SIMBA italiwakilisha Taifa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika wakati YANGA ikiiiwalisha TANZANIA katika michuano ya kombe la shirikisho barani AFRIKA michuano hiyo itanza kutimua vumbi mwezi MARCH mwakani.
===
Waziri wanchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa -TAMISEMI-Kapteni GORGE MKUCHIKA amezindua rasmi mashindano ya michezo ya shule za msingi UMITASHUMTA na kuwaagiza wakurugenzi wa halamsahauri za wilaya kote nchini kutenga bajeti itakayoziwezesha shule zote za msingi kushiriki mashindano hayo hapo mwakani.
Uzinduzi wa mashindano ya michezo kwa umoja wa shule za misingi yanafanyika ikiwa imepita miaka kumi tangu aliyekuwa waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi JOSEPH MUNGAI ayafute mwaka 2000 mkoani MOROGORO Mwandishi wetu Joseph Chewale aliyeko mkoani PWANI amehudhuria uzinduzi huo na hii hapa ni taarifa yake…

Up sound….
Wimbo wa taifa ndio ulioanza kuashiria uzalendo kwa mamia ya wanafunzi wa shule za msingi kutoka mikoa kumi na moja TANZANIA BARA ambao wwamekusanyika katika viwanja vya shirika la elimu KIBAHA kushuhudia uzinduzi wa umoja wa michezo kwa shule za misingi UMITASHUMTA ambapo mara baada ya wimbo huo waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa -TAMISEMA -kapteni GORGE MKUCHIKA anatoa maagizo ya serikali kwa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya juu ya kufufua michezo kwa vijana(PAUSE)
Pamoja na na maagizo hayo waziri MKUCHIKA pia hakusita kuinyoshea kidole wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi huku akiitaka isitoe vibali vya kusajili shule ambazo hazina viwanja vya michezo

Mashindano ya umoja wa shule za msingi UMITASHUMTA yanazinduliwa tena ikiwa imepita miaka kumi kamili tangu yafutwe mjini MOROGORO na aliyekuwa waziri wa elimu na ufundi wakati huo JOSEPH MUNGAI kwa madai kuwa yalikuwa yanawanyima muda wa kusoma wanafunzi.
Mwisho
==
Watano kuchuana fainali BONGO STARS SEARCH
Katika burundani waandaaji wa BONGO STARS SEARCH BENCHMARK PRODUCTION wametangaza wanamziki watano chipukizi wataochuana katika fainali ya shindano hilo ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni thelathini,fainali hiyo inafanyika siku ya ijumaa desemba 17 katika ukumbi wa MLIMANI CITY jijini DSM.
Wakizungumza wakati wa kutangaza majina hayo mkurungezi wa BENCHMARK PRODUCTION RITA POULSEN ambao ndio waandaaji wa shindano hilo na meneja wa bia ya KILIMANJARO GEORGE KAVISHE ambao ni wadhamini wa shindano hilo wamesema lengo la shindano hilo ni kuibua vipaji kwa wanamziki chipukizi na kuvifikisha katika kilele cha mafanikio.(VOX POPS)
Vijana waliongia katika fainali hiyo ni MARIAM MOHAMED, JAMES MARTIN, WAZIRI SALUM, BELLA KOMBA na JOSEPH PAYNE,na hapa wakaonyesha vipaji vyao kwa kuimba, hebu pata uhondo.
Katika fainali hiyo pia kutakua na wanamziki kwa ajili ya kutoa burundani kwa mashambiki watakaohudhuria kushuhudia fainali hiyo ambao ni pamoja na wanamziki wa kizazi kipya DIAMOND,TEMBA na CHEGE,MWASITI,JOHNMAKINI,IMANI,MARLAW,KIBONDE na CINDY kutoka UGANDA.
==
Mazishi ya Mwanamuziki REMMY kufanyika kesho kutwa
Mazishi ya Mwanamuziki mkongwe nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya CONGO DRC, RAMADHAN MTORO ONGALA maarufu Dokta REMMY aliyefariki dunia jana usiku yanatarajiwa kufanyika kesho kutwa siku ya ALHAMIS jijini DSM.

Marehemu Dokta REMY alifariki dunia katika hospitali ya Regency baada ya kuzidiwa ikiwa ni siku mbili tu tangu kuondolewa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alilazwa.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake SINZA KWA REMI ambapo Taarifa zaidi kuhusu mazishi zitatolewa baadaye.
Upsound wimbo wa kifo
= =
Waanza kuponda QATAR kuandaa kombe la dunia
RAIS wa shirikisho la soka duniani FIFA, SEPP BLATTER ameshindwa kuzungumzia suala la mashabiki wa soka wanaume wenye jinsia moja wanaojihusisha na mapenzi kutokuwa na nafasi ya kwenda nchini QATAR wakati wa mashindano ya kombe la dunia 2022.
Kulingana na sheria za QATAR, watu hao hawaruhusiwi kujihusisha na mahusiano pindi watakapokuwepo nchini humo humo.
Mbali na hilo pia choko choko nyingine zimejitokeza kwa kupinga QATAR kuandaa mashindano hayo zikidai kuwa wakati wa mwezi wa mashindano hayo kwa kawaida joto linakuwa na sentigredi AROBAINI hadi HAMSINI na kwa sheria ya sasa ya QATAR inakataza watu kutokunywa pombe hadhari.
Desemba Mbili mwaka huu wajumbe wa FIFA waliichagua QATAR kuandaa mashindano hayo ya dunia ya 2022, kwa kuzishinda nchi za AUSTRALIA, JAPAN, SOUTH KOREA na UNITED STATES.
==
TP MAZEMBE kucheza nusu fainali.
MABINGWA wa AFRIKA, TP MAZEMBE leo wanacheza mchezo wao wa nusu fainali ya mashindano ya FIFA ngazi ya vilabu kutoka mabara tofauti ulimwenguni.
MAZEMBE itacheza na timu ya INTERNATIONAL ya BRAZIL baada ya TP MAZEMBE ya CONGO kuirarua timu ya PACHUCA ya MEXICO.
Wadadisi wa soka tayari wamebainsha kuwa kiwango cha TP Mazembe katika mashindano hayo kimekuwa cha juu kwani timu hiyo imeweka rekoditangu iwekwe mara tatu na timu nyingine za Afrika kwenye mashindano hayo kama AL-AHLY 2006 na ETOILE DU SAHEL ya TUNISIA mwaka 2007.
==
MANCHESTER UNITED yairarua ARSENAL
BAADA ya kipigo cha goli MOJA kwa SIFURI dhidi ya MANCHESTER UNITED, kocha wa timu ya ARSENAL, ARSENE WENGER amekosoa uwanja wa OLD TRAFFORD eneo la kuchezea PITCH kuwa ni moja ya sababu iliyosabaisha wachezaji wake kufanya vibaya katika mchezo huo.
Mchezaji JI-SUNG PARK wa MANCHESTER UNITED ndiye aliyepachika goli pekee katika mchezo huo.
Katika mchezo huo ARSENAL kupitia kwa mchezaji wake MAROUANE CHAMAKH,waliweza kukosa nafasi kadhaa za kupachika magoli .

==
HISIA za makocha katika mashindano ya CECAFA
Ama kwa hakika mashindano ya CECAFA TUSKER CHALENJI yaligubikwa na kashi kashi nyingi hususani za makocha.
Nimefuatilia makocha hawa walivyokuwa wakihamasisha timu zao wakati wa mechi zao
==
OBAMA akutana na LOS ANGELES
RAIS wa MAREKANI, BARACK OBAMA amekutana na kikosi cha timu ya LOS ANGELES inayoshiriki ligi ya mchezo wa kikapu ya NBA ya MAREKANI akiwemo KOBE BRYANT.
Hiyo ilikuwa ni ziara ya pili kwa kikosi cha LOS ANGELES kumtembelea rais OBAMA na safari hii walikutana na wasichana na wavulana wadogo waliopo katika eneo la WASHINGTON DC.
Rais Obama ambaye ni shabiki mkubwa wa timu ya CHICAGO BULLS ameipongeza timu hiyo kwa kutumia muda wake mwingine kusaidia katika huduma za kijamii.
Mbali na Kobe Bryant pia OBAMA alikutana na wachezaji wengine wa sasa na wazamani .
Hii ni moja ya huduma ambayo LOS ANGELS inafanya baada ya kunyakuwa kombe la NBA mwaka huu na inakadiriwa zaidi ya mashabiki MILIONI MOJA na NUSU walikusanyika kuishangilia timu hiyo.
==



No comments:

Post a Comment