Monday, December 20, 2010

MICHEZO LEO

Marefu wafunzu mafunzo FIBA

Washiriki wanane wa kozi ya ukufunzi ya urefa wa mpira wa kikapu iliyokua inafanywa na shirikisho la mchezo huo dunia FIBA leo wanakabidhiwa vyeti vyao baada ya kufunzu mafunzo hayo na kuwa wakufunzi wa kitaifa.

Kwa upande wake mkufunzi wa FIBA aliyeendesha mafunzo hayo FIBA ZULFIKA amesema ana matumaini makubwa na wakufunzi hao na kuwataka watumie taaluma waliyoipata kufundisha waamuzi wengine.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania TBF PHARES MAGESA amesema mafunzo haya yaliyotolewa na FIBA yatasaidia kuongeza idadi ya waamuzi wa mchezo wa kikapu hapa nchini kwasababu wahitimu wa mafunzo haya nao watawafundisha wenzao.

===

MWANAMZIKI WA TWANGA ABUU SEMHANDO AZIKWA TANGA

Aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa bendi ya muziki wa dansi ya TWANGA PEPETA- ABUU SEMHANDO amezikwa jana huko MUHEZA mkoani TANGA ambapo maziko hayo yamehudhuriwa na mamia ya watu.

Marehemu ABUU SEMHANDO amezikwa kijijini kwao KIBANDA wilayani MUHEZA.

Ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzake wa wanamuelezea marehemu ABUU SEMHANDO kuwa alikuwa mchapakazi, mtu wa watu na alikuwa mfano wa kuigwa.

Marehemu SEMHANDO alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi kwa kugonjwa na gari ndogo aina ya MERCEDEZ BENZ wakati akiwa anaendesha pikipiki huko MBEZI-TANGI BOVU jijini DSM.

MAREHEMU -ABUU SEMHANDO amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 68 na ameacha mjane na watoto.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMINA.

= = =

CAF KUTOA TUZO MBALIMBALI LEO

SHIRIKISHO LA soka barani afrika CAF leo linaendesha zoezi la utoaji wa tuzo mbalimbali za wachezaji bora,timu bora na kocha bora wa AFRIKA huko CAIRO,MISRI.

Tuzo hizo zimegawanywa katika vipengele NANE.

Vipengele hivyo ni MWANASOKA BORA WA AFRIKA,MWANASOKA BORA ANAYECHEZA AFRIKA,MCHEZAJI BORA WA KIKE,MCHEZAJI BORA ANYECHIPUKIA,KLABU BORA YA MWAKA,TIMU BORA YA TAIFA YA MWAKA,TIMU BORA YA TAIFA YA WANAWAKE YA MWAKA na KOCHA BORA WA MWAKA.

Mshambuliaji wa timu ya INTER MILAN ya ITALIA na CAMEROON- SAMUEL ETOO anapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji la mwanasoka bora barani AFRIKA ikiwa ni kwa mara ya NNE kwake.

ETOO ametwaa taji hilo mwaka 2003, 2004 na 2005.

Wengine wanaopewa nafasi hiyo ni pamoja na mtetezi wa tuzo hiyo DIDIER DROGBA ambaye ametwaa tuzo hiyo mara MBILI na ASAMOAH GYAN wa GHANA anayewania tuzo hiyo kwa mara ya kwanza.

Pia leo ndio ratiba ya michuano ya vilabu barani AFRIKA itatolewa huko CAIRO.

====

Real Madrid waibuka kidedea la liga

LIGI KUU ya HISPANIA maarufu kama LA LIGA iliendelea jana kwa michezo mitatu kucheza katika viwanja tofauti.

REAL MADRID wakiwa katika dimba lao la SANTIAGO BERNABEU walitoka kifua mbele baada ya kuichapa SEVILLA kwa bao MOJA kwa BILA.

Goli pekee la REAL lilipachikwa wavuni na muargeritina ANGEL DI MARIA

Mchezo mwingine ulishuhudia ALMERIA ikilala baada ya kukubali kipingo cha mabao MATATU kwa MAWILI kutoka kwa GETAFE.

ATLETICO MADRID ikaifunga MALAGA magoli MATATU kwa BILA na OSASUNA ikienda suluhu dhidi ya REAL ZARAGOZA.

Mabigwa watetezi BARCELONA bado wanaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na alama 43 akifuatiwa na REAL yenye alama 41, Villarreal inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 33, Valencia ipo katika nafasi ya nne ikiwa na alama 28.

===

BAYERN MUNICH yatamba BUNDES LIGA

Ligi kuu ya UJERUMANI BUNDES LIGA mabingwa watetezi wa ligi hiyo BAYERN MUNICH waliteremka dimbani dhidi ya VFB STUTTGART katika uwanja wa MERCEDEZ BENZ ARENA.

Katika mchezo huo BAYERN MUNICH wakaibuka kidedea kwa ushindi mnono wa mabao MATANO kwa MATATU dhidi ya VFB STUTTGART

Mabao ya BAYERN yalifungwa na MARIO GOMEZ THOMAS MULLER na FRANK RIBBERY.

Katika muchezo mwingine Bayer Leverkusen ikatoka sare ya kufungana mabao mawili kwa mawili na Freiburg

Lakini pamoja na ushindi huo bado BAYERN wapo katika nafasi ya TANO katika msimamao wa ligi hiyo wakati BORUSSIA DORTMUND inaongoza ikiwa na alama 43 na kufuatiwa na Mainz yenye alama 33.

===

CARLOS TEVEZ kutimuliwa unahodha MANCHESTER CITY.

Kocha wa timu ya MANCHESTER CITY ya ENGLAND ROBERTO MANCINI huenda akamyang’anya unahodha wa timu hiyo CARLOS TEVEZ.

KWA mujibu wa habari zilizonukuliwa katika tovuti ya shirika la utangazaji nchini UINGEREZA-BBC,MANCINI na TEVEZ walikutana kwa mazungumzo siku ya ijumaa katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo ili kujadili juu ya ombi la TEVEZ la kutaka kuihama timu hiyo.

MAN CITY wanavaana na EVERTON leo katika mechi ya ligi kuu ya ENGLAND na MANCINI anajiandaa kumnyang’anya kitambaa cha unahodha TEVEZ na kumkabidhi nahodha msaidizi KOLO TOURE au VINCENT KOMPANY.

Mancini bado hajauarifu uongozi wa klabu hiyo juu ya maamuzi yake hayo ingawa tayari habari hizo zimeufikia uongozi japo si rasmi.

KOLO TOURE alikuwa nahodha wa MAN CITY wakati ikiwa na kocha MARK HUGHES lakini akanyang’anywa nafasi hiyo na kupewa TEVEZ kwa nia ya kumshawishi nyota huyo kubakia katika timu hiyo.

===

ERNIE ANYAKUA UBINGWA WA gofu

Katika GOFU Ernie Els amenyakua ubingwa wa wazi wa GOFU wa AFRIKA KUSINI hiyo jana baada ya kumaliza mzunguko wa nne akiwa mshindi katika uwanja wa DURBAN COUNTRY CLUB.

Ernie Els huu utakua ni ubingwa wake wa tano katika mashindano hayo na alimshinda mpizanai wake wakaribu Retief Goosen.

Ernie Els alimaliza mzunguko wa mwisho kwa 25-under-par alipofanikiwa kupinga mpira vyema katika shimo la nne.

Mchezo huo ulihusisha mashimo 36 na wachezaji walishindana kwa muda wa siku nne.

No comments:

Post a Comment