Wednesday, October 13, 2010

CBA Nyerere Open Gofu

WACHEZAJI wa mchezo wa gofu kutoka MOROGORO, ARUSHA, DSM na MOMBASA watapambana katika MASHINDANO ya mchezo huo yenye lengo la kumuenzi marehemu baba wa taifa mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE.

Afisa Tawala wa chama cha gofu Tanzania TGU, SOPHIA NYANJERA amesema mashindano hayo yamepangwa kufanyika jumamosi wiki hii katika viwanja vya GYMKHANA jijini DSM.
Mashindano hayo yanatumiwa na wachezaji wa timu ya taifa kujinoa kabla ya kwenda kushiriki mashindano ya dunia yaliyopangwa kufanyika nchini ARGERTINA mwisho wa mwezi OCTOBA

No comments:

Post a Comment