Tuesday, October 19, 2010

Michezo leo

TFF kuwapinga msasa makocha wa ligi kuu Tanzania bara.
Shirikisho la soka nchini TFF kuwapinga msasa makocha wa ligi kuu Tanzania bara na wakufunzi wa mikoa ili kuwaweze kufika viwango vya shirikisho la soka barani Afrika CAF mwezi ujao.
Akizungumza na waandishi habari katika ofisi za TFF kaimu katibu mkuu wa TFF SUNDAY KAYUNI amesema, kozi hiyo ni kutekeleza maagizo ya CAF yaliyotolewa wiki iliyopita katika mkutano wa CAF na FIFA nchini MISRI ambapo CAF imetoa miaka minne tu kwa makocha kuhakikisha wamefiki madaja ya A,B na C ili waendelea kufundisha soka hapa nchini.
KAYUNI ameasema FIFA na CAF makocha wa timu za taifa wametakiwa kuwajumuisha wachezaji chipukizi katika timu zao za taifa ili kufanya vema katika michuano mabalimbali na kutolea mfano kwa timu za GHANA na Ujerumani kwamba zilifika mbali katika fainali za kombe la dunia kutokana na kutumia wachezaji chipukizi.
Mkutano wa FIFA na CAF uliomalizaika jijini CAIRO MISRI wiki ilyopita ulikuwa wa kutathimini fainali za kombe la dunia zilizomalizika AFRIKA KUSINI mwezi JULY.
====
TFF kuendesha ligi ya soka kwa shule za sekondari DSM
Shirikisho la mpira wa mguu nchini TFF limeamua kuendesha ligi maalumu ya soka kwa shule za sekondari za mkoa wa DSM ikiwa ni jaribio lake la kukuza kiwango cha soka hapa chini na yataanza kutimu vumbi jumamosi ya wiki ijayo katika viwanja vitatu jijini dsm.
Akizungumza jijini DSM hii leo kaimu katibu mkuu wa TFF SUNDAY KAYUNI amesema,shirikisho hilo limeamua kufanya hivyo ili kuonyesha mfano wa kuibua na kundeleza vipaji vya wachezaji chipukizi hapa nchini.
Kayuni amesema michuano hiyo itachezeshwa na marefa chipukizi na wasoni kwa lego la kuinua viwango vyao ili kuwa na marefa wenye ujuzi kwa faida ya soka la tanzania.
Shule 12 za wanaume na sita za wasichana kutoka kutoka katika mikoa ya kisoka ya KINONDONI,ILALA na TEMEKE.
====
BFT yasema ukosefu wa michezo ya kimataifa chazo cha kuboronga Madola
Ukosefu wa michezo za kimataifa na matumizi ya kopyuta vyatajwa kama sababu zilizosababisha mabondia wa Tanzania kuboronga katika michezo ya Jumuiya ya Madola iliyomalizaka wiki iliyopita nchini INDIA.
Akizungumza jijini DSM hii leo, Makamu rais wa BFT MICHEAL CHANGARAWE amesema ukosefu wa michezo ya kimataifa na matumizi ya kopyuta wakati wa mazoezi ndio zimekua sababu kubwa za kushindwa kutamba kwa mabodia wa Tanzania katika michezo ya MADOLA.
Changarawe amesema uongozi uliopita wa BFT ulipewa kopyuta na shirikisho la ngumi la dunia AIBA lakini haijulikani ilipo mpaka sasa kwani uongozi mpya haujakabidhiwa.
Changarawe amesema ili kuondokana na aibu iliyotokea India isitokea katika mashindano yajayo ya OLMPIKI yatakayofanyika UINGEREZA mwaka 2012 watafanya michuano ya kitaifa ili kutafuta mabondia chipukizi.
Ni kukumbushe tu kwamba timu ya Tanzania iliyoshiriki katika michezo ya YUMUIYA ya MADOLA haikuabulia medali hata moja.

====
Mrembo YARA wa PURTO RICO angara na vazi la ufukweni
MREMBO wa PURTO RICO, YARA SANTIAGO ameibuka mshindi katika shindano la dunia la ufukwe lililofanyika katika mji wa SANYA nchini CHINA ikiwa ni mwelekeo wa kuelekea fainali ya shindano hilo la dunia mwisho wa mwezi huu.
YARA SANTIAGO, amewashinda warembo wengine ISHIRINI waliongia fainali na mshindi wa pili ni kutoka MAREKANI, ambapo mrembo ALEXADRIA MILLS alimfuata kwa karibu mrembo YARA.
Mshindi wa tatu katika shindano hilo ni MARIANN BIRKEDAL kutoka nchini NORWAY.
Mrembo wa Tanzania katika mashindano hayo GENEVIVE MPANGALA hakufanikiwa kuingia katika AROBAINI BORA kwani ni mrembo wa GHANA na CAPE VERDE walipata tiketi ya kuingia hatua ya AROBAINI BORA na kushindwa kufua dafu katika hatua ya nusu fainali.
Ushindani wa ufukwe ni moja ya vitu vinavyofuatiliwa na waandaaji hao kwani inatoa alama zinazoweza kusaidia hatua ya fainali.

==
CHELSEA VS SPARTAK MOSCOW
MICHEZO ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA) inaendelea leo ambapo CHELSEA ipo ugenini nchini URUSI kucheza na SPARTAK MOSCOW katika mchezo wa kundi F.
Kocha wa CHELSEA, CARLO ANCELOTTI amebainisha kuwakosa akina DIDIER DROGBA ambaye anaumwa pamoja na FRANK LAMPARD ambaye anasumbuliwa na HERNIA.
Huku ANCELOTTI, akisema washambuliaji wake DANIEL STURRIDGE na SOLOMON KALOU kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo.
==
ANCELOTTI akanusha kutaka kumsaini ROONEY
Katika hatua nyingine kocha ANCELOTTI amekanusha tetesi kuwa klabu yake inataka kumchukua mshmabuliaji wa MANCHESTER UNITED, WAYNE ROONEY.
Mkataba wa ROONEY ambaye ana miaka 24, unamalizika mwaka 2012 na imeripotiwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanywa kati yake na mshambuliaji huyo wa MANCHESTER UNITED.
Mbali na CHELSEA ambayo ilikuwa ikidhaniwa kumnyemelea mshambuliaji huyo , pia MANCHESTER CITY na REAL MADRID ni vilabu ambavyo vimetajwa kuwa na nia ya kumnyakuwa mshambuliaji huyo, ijapokuwa kocha wa REAL MADRID , JOSE MOURINHO ametabiri kwa kusema kuwa hafikirii kama ROONEY ataiacha klabu yake.
==
FABREGAS yupo fiti mchezo wa leo
NAHODHA wa timu ya ARSENAL, CESC FABREGAS amerejea uwanjani na leo atakuwepo katika kikosi cha ARSENAL kitakaocheza na SHAKHTAR DONETSK katika uwanja wa nyumbani wa Emirates.
Kiungo huyo wa HISPANIA, hajacheza tangu awe majeruhi tangu septemba 18 pale alipoichezea timu yake na kuumia wakati wa mchezo dhidi ya SUNDERLAND.

Wachezaji wengine ambao wako fiti kwa mchezo wa leo ni pamoja na NICKLAS BENDTNER na THEO WALCOTT.

Huku ARSENAL ikiwa na majeruhi lukuki kama LAURENT KOSCIELNY, BACARY SAGNA na THOMAS VERMAELEN.

Wengine majeruhi ni AARON RAMSEY na ROBIN VAN PERSIE, ila kocha WENGER anategemea kumchezesha JACK WILSHERE.

==
RANIERI asema ana uhusiano mzuri na TOTTI
Naye Kocha wa timu ya AS Roma CLAUDIO RANIERI amemsifia nahodha wa timu yake FRANCESCO TOTTI kwamba bado ana umuhimu wake katika timu ijapokuwa TOTTI inaelezwa kuwa na umri mkubwa kwa kuwa kiwango chake kimekwisha.
RANIERI, ameyasema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambpo timu yake leo inacheza na FC BASEL.
Pia amekanusha kutokuwa na uhusiano mzuri na mchezaji wake TOTTI pamoja na wachezaji wengine wa timu hiyo.
Michezo mingine ya kundi E, BAYERN MUNICH itacheza na CFJ CLUJ, MALSEILLE itacheza na ZILINA katika mchezo wa kundi F.
Kundi G, AJAX inaikaribirisha AUXERRE, REAL MADRID inacheza na AC MILAN na kundi H kutrakuwa na mchezo kati ya SPORTING BRAGA itacheza na PARTIZAN BELGRADE.
==
Mwanaridha LASHAWN MERRITT afungiwa
MWANARIADHA bingwa wa OLYMPIC na wa dunia wa mita 400, LASHAWN MERRITT amefungiwa kwa miaka miwili baada ya kukutwa akitumia dawa za kuongeza nguvu michezoni.
MERRITT, kutoka MAREKANI alipimwa mara tatu na kukutwa anatumia dawa hizo katika kipindi cha OKTOBA 2009 hadi JANUARI mwaka huu.
Kutokana na kufungiwa huko sasa, mwanariadha huyo huenda akarejea tena mwakani wakati wa mashindano ya dunia yatakayofanyika mwezi wa NANE.
MERRITT, alishinda mita 400 wakati wa mashindano ya OLYMPIC yaliyofanyika BEIJING.
==

No comments:

Post a Comment