Tuesday, October 26, 2010

SIMBA na YANGA viwanjani kesho

Ligi kuu Tanzania bara Yanga na Simba viwanjani kesho

Ligi kuu Tanzania bara kuendele kesho katika viwanja vinne kuwaka moto huku watani wa jadi SIMBA na YANGA wakisaka ALAMA mhimu ili kujikita kileleni mwa ligi hiyo.

Mabingwa watetezi SIMBA wao wamesafiri hadi mkoani kagera kuivaa KAGERA SUKARI katika dimba la KAITABA wakati YANGA wao watakuwa wenyeji wa AFRICAN LYON katika dimba la JAMHURI MKOANI MOROGORO.

MICHEZO MINGINE wauza lambalamba AZAM FC watakuwa wageni wa MAAFADE wa POLISI TANZANIA katika uwanja wa JAMHURI mkoani MOROGORO huku wakata miwa MTIBWA SUKARI wataikaribisha timu inayoburuza mkia katika ligi hiyo ARUSHA FC katika uwanja wa MANUNGU huko turiani mkoani MOROGORO.

YANGA ipo kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na Alama 21 sawa na bingwa mtetezi SIMBA lakini YANGA inaogoza kwa sababu ya tofauti ya magoli ya kufunga na kufunga na SIMBA.

Timu ya taifa ya Gofu kutamba michuano ya dunia

Wachezaji watatu wa timu ya taifa ya GOFU ya TANZANIA wanaotarajiwa kuteremka dimbani kupeperusha bendera ya taifa katika michuano ya dunia ya GOFU inayofanyika kesho kutwa siku ya ALHAMISI huko ARGERTINA wanamatumaini ya kufanya vema katika michuano hiyo.

Akizungumza na TBC Afisa tawala wa chama cha GOFU Tanzania TGU, SOPHIA NYANJERA amesema wachezaji hao wamefika salama ARGERTINA na wamefanya mazoezi katika viwanja yatakapo fanyika mashindano hayo ya GOFU ya dunia ili kuzoea hali ya hewa kabla ya kuanza kinyang’anyiro cha kutafuta ubingwa wa Dunia.

Wakati timu ya taifa ya GOFU kwa wanaume ikijiandaa kucheza katika mashindano hayo wezao akina dada wametoka kapa baada ya kumaliza katika nafazi ya 51 katika nchi 52 zilizoshiriki mashindano ya GOFU ya dunia kwa wanawake yaliyomalizika mwishoni mwa wiki huku ARGERTINA.

====

Stingrays yatwaa medali sabini na nne nchini Malawi.

Klabu ya kuogelea ya STINGRAYS aliyoshiriki mashindano ya MWALIKO WA MALAWI Kuanzia October 22 hadi 23 nchini MALAWI imerudi na medali SABINI na Nne na kufanikiwa kuwakilishwa vyema TANZANIA katika mashindano hayo.

Akizungumza mara baada ya kuwasili wakitokea nchini MALAWI mkuu wa msafara wa timu hiyo RAMADHANI NAMKOVEKA amesema haikuwa kazi ngumu kutwaa medali hizo kwani waogeleaji kutoka nchini zilizoshiriki mashindano hayo zilikuwa zimejiandaa vizuri.

Mchezaji CHRISTIAN OPPERMAN amejinyakulia medali saba peke yake akishiriki katika staili tofauti katika mashindano hayo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa ufundi wa chama cha kuogelea TSA MARCELINO NGALIOMA amesema kwa medali walizopata waogeleaji hao zimeiletea sifa TANZANIA hivyo ni jukumu la timu zingine kuiga mfano wa klabu ya STINGRAYS.

Kocha wa klbu hiyo LEILANI CORREIA amesema kiwango walichoonyesha wachezaji hao kinampa matumaini ya kufanya vizuri katika mashindno ya muungano nay a kimataifa yatakayofanyika nchini BOSTWAN.


No comments:

Post a Comment