Saturday, October 2, 2010

Watoto mafunzoni


Zaidi ya watoto Arobani wenye umri kati ya miaka 5 hadi 14 wameendelea na mafunzo ya awali ya mchezo wa tenisi katika viwanja vya POSTA jijini dsm.
Akizungumza na TBC wakati wa mafunzo hayo kocha anayewanoa vijana hao, BOAZI KASIBA amesema mafunzo hayo yemeanzia kwa kuendeleza vipaji vya wachezaji chipukizi wa tenisi katika jiji laDSM na baadaye mafunzo hayo yetaendelea Mikoani.
Kwa upande wake mchezaji jipukizi HAPPYNESS PASCAL amesema aliingia akiwa hajui kambiza mchezo huo lakini sasa kiwango chake kimeanza kupanda.
Mafunzo hayo yanaedeshwa na klabu ya Kijitonyama chini ya shirikisho la mchezo wa tenisi nchini TTA.

No comments:

Post a Comment