Monday, October 11, 2010

MICHEZO DUNIANI

Katika michezo ya JUMUIYA YA MADOLA inayondelea mjini NEW DELHI nchini INDIA wakenya wameendelea kutamba baada ya BOAZ LALANG kunyakua medali ya DHAHABU katika mbio za mita 800 hiyo jana
Mwingereza LEON BAPTISTE akajinyakulia medali ya dhahabu baada ya kushinda mbio za mita 200 kwa wanaume.
Katika mbio za mita 400 kuruka viuzi,DAI GREENE wa WALES amejinyakulia medali ya dhabu baada ya kumaliza wa kwanza katika mbio hizo akimshinda LOUIS VAN ZYL wa AFRIKA kusini.
Kwa upande wa akina dada,Mnigeria MUIZAT ODUMOSU akajinyakulia medali ya dhahabu baada ya kumaliza wa kwanza akiwashinda MSCOTLAND EILIDH CHILD na MJAMAICA NICKIESHA BODEN.
Katika michezo hiyo watanzania hawajaambulia medali yeyote.
=====

Mshambuliaji wa Ghana na SUNDELAND ya EGLAND, ASAMOH GYAN ameonyesha kadi nyekundu na mwamuzi JEROME DAMIAN kutoka Afrika ya Kusini katika dakika ya 82 na kushindwa kuisaidia GHANA kuchomoza na ushindi ilipolazimishwa kutoka suluhu na SUDAN mjini Kumasi hiyo jana
Katika matokeo mengine CONGO akaifunga SWAZILAND mabao 3-1,Ghana inaongoza kundi hilo la I ikiwa na Alama 4 sawa na Sudan yenye Alama NNE,CONGO wanashika nafasi ya tatu wakiwa na Alama 3 WAKATI Swaziland wanaburuza mkia katika kundi hilo wakiwa hawana Alama.
Matokeo mengine ya kushangaza katika harakati hizo za kuwania tiketi ya kucheza fainali za komba la mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini GABON mabingwa watetezi MISRI wamejikuta wakichapwa bao moja kwa bila na vibonde katika kundi la G NIGER.
Mchezo mwingine wa kundi la G ulishuhudia waandalizi wa finali za kombe la FIFA la dunia 2010 zilizomalizika Afrika Kusini nao wakishindwa kutamba ugenini baada ya kulazimishwa suluhu na SIERRA LEONE.
Matokeo mengine ya kushangaza NIGERIA imepata kichapo baada ya kufungwa na bao moja kwa bila na GUINEA jijini LAGOS, wawakilishi wengine katika fainali zilizopita za kombe la dunia ALGERIA wakapata kichapo cha mabao MAWILI kwa bila kutoka kwa JAMHURI ya Afrika ya kati katika kundi la D.
Morocco wanaongoza kundi D baada ya kuichapa TAIFA STARS bao moja kwa bila jijini dsm mwishoni mwa wiki,michuano hiyo ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za komba la mataifa ya Afrika 2012 yataendelea mwezi MARCH mwakani.

======

KATIKA MPIRA WA WAVU, timu ya mpira wa wavu ya wanaume ya BRAZIL imetawazwa mabingwa wa dunia baada ya kuifunga CUBA kwa mabao 25 kwa 22 katika mchezo wa fainali uliofanyika jana huko ITALI.
Hii itakua ni mara ya tatu kwa BRAZIL kushinda ubuingwa huo wa mpira wa wavu kwani ilishatwaa taji hilo katika miaka ya 2002 and 2006
Serbia ambayo inashika nafasi ya nne kwa ubora wa mchezo wa wavu dunia yenyewe imeshika nafasi ya tatu na kupata medali ya shaba baada ya kuwafunga wenyeji ITALI kwa ushindi wa seti 3 kwa 1.
===

Katika mbio za pikipiki MHISPANIA JORGE LORENZO amenyakua ubingwa wa dunia baada ya kumaliza wa tatu MALAYSIA GRAND PRIX.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mbio hizo JORGE LORENZO ambaye ndi kwa mara ya kwanza anabyakua ubingwa huo wa dunia alisema amefurahi sana kunyakua ushindi huo na anamini ataendelea kutamba katika mashindano yajayo ya mbio za pikipiki dunia
Katika mbio hizo za MALAYSIA GRAND PRIX, VELENTINO ROSI wa ITALI akiedesha pikipiki aina ya YAMAHA alimaliza wa kwanza akimshinda muitaliano mwezake ANDREA DOVIZIOSO aliyemaliza wa pili.
Pamoja na mvua kunyesha lakini alikuwa ni ROSSI aliongoza katika mzunguko wa 11 baada ya kuwapita washindani wake LORENZO na DOVIZIOSO.

=====

SEBASTIAN VETTEL ameibuka kidedea katika mashindano yam bio za magari ya JAPAN GRAND PRIX,huku MARK WEBBER akimaliza katika nafasi ya pili na kujiongezea Alama 14 zaidi katika kuwania ubingwa wa dunia wa mashindano ya magari ya FOMULA ONE .
Dereva wa FERRARI FERNANDO ALONSO akamaliza katika nafasi ya tatu,huku JENSON BUTTON wa maclaren akimaliza katika nafasi ya NNE na nafasi ya tano ikanyakuliwa na dereva mwingiene wa MACLAREN LUIS HAMILITON.
Matokeo ya jumla yanonyesha kuwa dereva wa RENULT MARK WEBBER anaongoza maderava wezake akiwa na Alama 220 na kufuatiwa na dereva wa FERRARI FERNANDO ALONSO akiwa na Alama 206 akifungana na Derevamwingine wa RENULT sebestian vettel AMBAYE PIA ana alama 206, DEREVA WA MAC LAREM mwingereza LUIS HAMILTON yeye yupo katika nafasi ya NNE akiwa na alama 192,jenson button yeye anashika nafasi ya tano wakati FILIPE MASSA wa FERRARI anashika nafasi ya SITA.
==

No comments:

Post a Comment