Wednesday, October 20, 2010

habari za tz

WANAMITINDO chipukizi WANANE watakuwa miongoni mwa wanamitindo 32 kutoka katika nchi za AFRIKA ya MASHARIKA ambao watampambana katika shindano la maonyesho na ubunifu la SWAHILI FASHION 2010 .

Mratibu wa onyesho hilo MUSTAFA HASANALI amesema kati ya wanamitindo hao wanamitindo 24 ni wale wenye uzoefu katika fani ya ubunifu kutoka mataifa ya RWANDA , TANZANIA , BURUNDI , KENYA na UGANDA

Mbali na masuala ya ubunifu , pia onyesho hilo litahusisha utamaduni wa vyakula na mavazi ya makabila mbalimbali nchini.

=

MWANAMZIKI wa miondoko ya BONGO FLEVA, ALLY KIBA anaondoka nchini keshokutwa kwenda nchini MAREKANI ambapo anaungana na wanamuziki wengine SABA kutoka AFRIKA ambao wataimba na nyota wa MAREKANI.

Maratibu kutoka kampuni ya ROCKSTAR, CHRISTINE MOSHA amesema msanii KIBA na wenzake wa Afrika wataunda kundi linalojulikana kama ONE-EIGHT

Katika kundi kila msanii ataimba kwa lugha yake ambapo ALI KIBA yeye ataimba kwa lugha ya Kiswahili.

Wanamuziki wengine ni AMANI kutoka KENYA, NAVIO kutoka UGANDA , FALLY IPUPA kutoka DR CONGO , 2FACE kutoka NIGERIA, JK kutoka ZAMBIA, FOUR TIMES kutoka GHANA na MOVAIZHALEINE kutoka GABON.

==

Wakazi wawili wa jijini la DSM, GRACE BIKO na MUSA SULEIMAN kwa nyakati tofauti wameendelea kushinda katika shindano la bahati nasibu la SUPA PESA.

Mkazi GRACE BIKO yeye amejishindia kiasi cha shilingi MILIONI KUMI, wakati SELEMAN yeye akizoa kitita cha shilingi MILIONI MOJA.

GRACE BIKO anakua ni mshindi wa nne kujinyakulia kitita cha shilingi MILIONI KUMI katika bahati nasibu ya SUPA PESA.

===

No comments:

Post a Comment