Tuesday, October 12, 2010

Kiingilio YANGA na SIMBA


Viingilio vya mechi ya watani wa jadi SIMBA na YANGA utakapigwa kwenye dimba la CCM KIRUMBA siku ya JUMAMOSI vimetangazwa na Kiingilo cha juu kitakuwa elfu thelathini na cha chini 3000/-

Akizungumza na TBC katika ofisi za shirikisho hilo zilizopo katika uwanja wa kumbukumbu ya karume jijini DSM kaimu katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF SUNDAY KAYUNI amesema VIP kiingilio kitakuwa ELFU THELATHINI,jukwaa kuu ELFU ISHIRINI na mzunguko ELFU TANO.

Wakati huo huo KAYUNI amesema msafara wa viongozi watatu wa TFF wameondoka leo kwenda CAIRO MISRI kuhudhuria mkutano wa shirikisho la soka Afrika, CAF wa kutadhimini michuano ya fainali za kombe la mataifa Afrika CAN zilizofanyika Angola mwaka 2008.

Viongozia waliondoka ni rais wa TFF leodiger tenga,kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday kayuni na kocha wa timu ya taifa JAN PAULSEN.


No comments:

Post a Comment