Monday, October 11, 2010

Ligi ya TFF kondoa

Timu ya KINGALE FC ya KONDOA leo inateremka dimbani kumenyana na TOTO FC ya KONDOA mjini katika mchezo wa ligi ya taifa ya TFF ngazi ya wilaya KONDOA,mchezo huo utachezwa kwenye dimba la KONDOA mjini.

KINGALE FC mpaka sasa inashika usukani katika kundi B ikiwa na Alama SITA, baada ya kuteremka dimbani mara mbili na kushinda michezo yote.

Katika mchezo wa kwanza KINGALE FC ilichomoza na ushindi wa mabao matatu kwa mawili kabla ya kutoa kipigo cha mabao mawili kwa bila kwa bingwa mtetezi wa ligi hiyo CHINGA FC ya Kondoa mjini.

Kundia B lina timu za KINGALE FC, CHINGA FC, MUGURI, TUGUFU na TOTO FC,wakati kundi A baadhi ya timu ni Kondoa city na Mnadani

No comments:

Post a Comment