Monday, October 11, 2010

Mnageria na madawa kuongeza nguvu madola

Mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 100 katika michezo ya JUMUIYA YA MADOLA kwa wanawake Mnaigeria OSAYEMI OLUDAMOLA amegudulika kwamba alitumia dawa za kuongeza nguvu zilizokatazwa kwenye michezo baada ya kuchukuliwa vipimo asubuhi ya leo.

Na sasa mwanadada huyu sasa anakabiliwa na adhabu ya kupokonywa medali yake ambayo alipewa baada ya aliyekuwa ameshinda wa mbio hizo SALLY PEARSON wa AUSTRALIA kunyang’anya medali yake ya dhahabu kwa kile kilichaonekana alianza mapema kukimbia katika mstari wa kuanzaia kabla ya wezake jumanne ya wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa rais wa shirikisho la michezo ya JUMUIYA YA MADOLA MIKE FENNELL amesema maamuzi ya kumpokonya ushindi au la mwanaridha huyo wa Nigeria yatajulikana baadae leo baada ya kikao cha kamati ya mashindano kufanyika.



No comments:

Post a Comment