Tuesday, July 12, 2011

BINSLUM yatoa msaada kwa waendesha pikipiki


Wachukuzi wa abiria kwa kutumia pikipiki maarufu kama BODABODA wameaswa kutumia vifaa vya kujikinga na ajali za barabarani ili waweze kuinuka kiuchumi na kukuza vipato vyao.

Wito huo umetolewa na Msemaji wa kampuni ya BINSLUM TYRES LIMITED, SALIM ALJAABRY wakati alipokuwa akikabidhi majaketi maalum zaidi ya MIA MOJA ya kuzuia upepo kwa madereva wa pikipiki jijini DAR ES SALAAM(PAUSE)

Nao baadhi ya waendesha pikipiki hao YUNUS SAID na ADAM KASIMBA wamesema wamefurahia msaada huo na kusema utawaongezea ufanisi kwa kufanya kazi zao kwa usalama barabarani(VOX POP)

Uhaba wa vifaa vya usalama barabarani umekuwa ni chanzo cha ajali barabarani kwa waendesha pikipiki n hivyo kuweka rehani usalama na afya zao.



No comments:

Post a Comment