Tuesday, July 26, 2011

DROO ya ligi ya taifa yawekwa hadharani




Shirikisho la soka nchini TFF, limefanya droo ya fainali ya ligi ya taifa kutafuta timu itakayopanda daraja la kwanza msimu huu, ambayo inatarajiwa kuanza AUGUST NANE hadi KUMI na NNE.
Afisa habari wa TFF, BONIFACE WAMBURA amesema Jumla ya timu KUMI na MBILI zitashiriki ligi hiyo iliyopangwa kufanyika Mkoani TANGA, ambapo ametoa sababu zilizoufanya mji wa TANGA kuchaguliwa kuwa kituo cha fainali hizo.
WAMBURA amesema katika kundi A , kutakuwa na timu za MLALE JKT, GEITA VETERANS, RUMANYIKA na KASULU UNITED.
Kundi B litakuwa na timu za POLISI MORANI, SAMARIA FC, MGAMBO na COSMOPOLITAN
Kundi C litakuwa na timu za POLISI CENTRAL, SIFA POLITAN, MAJENGO na SMALL KIDS.
Wakati huo huo jumla ya timu TANO zimethibitisha kuutumia Uwanja wa AZAM ulioko MBANDE, CHAMAZI.
Timu zilizothibitisha kuutumia uwanja huo katika mechi za ligi ni pamoja na AZAM FC, AFRICAN LYON,VILLA SQUAD, MORO UNITED na JKT RUVU.
Aidha Uwanja huo hautatumika katika mechi za SIMBA na YANGA dhidi ya vilabu hivyo.


= =

No comments:

Post a Comment