Tuesday, July 26, 2011






.Wanariadha wa MKOA WA MJINI MAGHARIBI watamba mashindano ya taifa ya riadha.
Jumla ya mikoa 21 imeshiriki mashindano ya taifa ya riadha lengo lake kubwa likiwa ni kuchangua timu ya taifa mchezo huo itakayoshiriki michezo ya ALL AFRICA GAMES inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi SEPTEMBA 3 hadi 18 jijini MAPUTO,MSUMBIJI.
Wanariadha wa mkoa wa MJINI MAGHARIBI wameonyesha kiwango cha juu na kutwaa medali 33 na hivyo kuwa washindi wa jumla.
Kati ya medali hizi 33, medali 16 ni za dhahabu, 9 za fedha na 8 za shaba.
Mkoa wa ARUSHA umeshika nafasi ya pili baadya ya kunyakua medali 24 kati ya hizo dhahabu zikiwa 8, fedha 9 na shaba 7.
Wenyeji DSM wamemaliza katika nafasi ya SABA.
Katika hatua nyingine naibu waziri wa mambo ya ndani na mbunge wa BUKOBA MJINI –BALOZI KHAMISI KAGASHEKI amewataka wadau wa michezo nchini kuunga mkono mchezo wa riadha.
BALOZI KAGASHEKI alikuwepo uwanjani hiyo jana ambapo pia aliwatembelea wanariadha wa mkoa wake wa KAGERA.
Balozi KAGASHEKI enzi zake alikuwa akitamba katika riadha hususani mbio za mita 100 na 200.
===

No comments:

Post a Comment